MBOKA NA NGAI
JF-Expert Member
- Jan 31, 2025
- 350
- 576
Pichani, ni aliekuwa kiongozi wa kundi la wapiganaji TWIRWANEHO(TUJIRINDE), la wanyamulenge huko Kivu kusini.
Ameuwawa akiwa na wenzie wa 5,wanaosemekana kuwa walinzi wake, katika shambulio la drone, lililoandaliwa na jeshi la serikali ya Congo, FARDC.
M23, kwa sasa inaelekea katika maeneo ya TWIRWANEHO, na Kiongozi huyo, alikuwa ametangaza kuwa punde tu M23 itakapowasili maeneo yake, watajiunga na kuongeza nguvu.
Makanika alitoroka jeshi akiwa na cheo cha kanali, na kurudi huko alikozaliwa katika jimbo la FIZI, kuhakikisha anakusanya vijana wa Kinyamulenge waliokuwa wakiuliwa na kupolwa mali zao na jeshi la FARDC na washilika wake, ambao ni FDLR,wazalendo, na mwishoe jeshi la serikali ya Burundi, lililokuja kwa lengo la kukabiliana na waasi wa serikali hiyo, wajulikanao kama RED-TABARA.