Colin Powell anaonekana kuwe mtu mwenye busara sana katika nyakati zetu

Colin Powell anaonekana kuwe mtu mwenye busara sana katika nyakati zetu

Limbukeni

Senior Member
Joined
Feb 27, 2009
Posts
117
Reaction score
1
AKIWA KATIKA WATU WALIOTUMIA KUAZISHA VITA, ALIPOJUA HILO ALISIKITIKA AKAJIUZULU NA AKAJUTIA NA KUAMINI AMESAMEHEWA. WAKATI ALIPOAMUA KUMUUNGU MKONO OBAMA KWA KUVUKA MIPAKA YA CHAMA CHAKE ALISHUTUMIWA SANA LAKINI ILIONEKANA ANATAKA KIONGOZI BORA NA SIO BORA KIONGOZI. KAMA UCHAGUZI ULIVYOKUWA REPUBLICAN HAWAKUWA NA MGOMBEA IMARA KWA HIYO ILIKUWA KAMA BORA LIENDE. INGAWA MATOKEO YALIKUWA KAMA KUKARIBIANA. HIVI KARIBUNI ALIHOJIWA JUU YA KUFUNGWA KWA GBAY HUKO KWA RAUL AMBALO RAIS OBAMA ALILIPELEKA BUNGENI LIKAPATA KURA NNE TU KATI YA 90. LILIPINGWA VIKALI NA WABUNGE WAKATAKA MPAGO KAMILI ILI WAPITISHE. POWEL AKASEMA OBAMA ALIHARAKISHA MNO ALITAKIWA APELEKE MPANGO KAMILI SIO KUOMBA PESA TU BILA MPANGO. UKIMSIKILIZA UTAJUA HUYU MTU ANAONGEA KWA DHATI KUTOKA MOYONI. NI HATARI SANA KUWA NA KIONGOZI AU RAFIKI ANAYEONGEA KWA MDOMO TUU HUKU AKIWA PEKE YAKE ANAFIKIRIA VINGINE. JE NI LINI TANZANIA ITAKUWA NA UKOSEFU WA VIONGOZI NJAA NA WAOGA WAKUONGEA UKWELI MPAKA LINI?.

CNN Political Ticker: All politics, all the time Blog Archive - CNN Poll: Powell vs. Cheney and Limbaugh « - Blogs from CNN.com
 
Kaka, Ni Mwalimu Nyerere tu aliyekuwa na uwezo wa kufanya hivyo, wengine wote Kwishnehi, Choka Mbaya . . . . Itatuchukua muda kupata kiongozi Mkweli na wa dhati.

Wengi wanaegemea katika maslahi yao binafsi na ya chama.
 
Asante unaweza kukadiria labda ni miaka mingapi maana ukimtaja nyerere ni miaka -12 mana hatunaye mungu amesaidia wewe upo. Pia labda miaka mingapi bado +10 au +100 au haitawezekana kabisa. Asante sana mkuu
 
Mkuu; anything can happen soon or later;

Jessey Jackson alilia Obama aliposhinda kwa kuwa hakutegemea ndoto ya Martin Luther itatimia so soon.

Mnapokuwa na vijana wenye uthubutu na Wazee wenye nia ya kweli all the time, ni rahisi kupata watu kama akina Powel.

Ngoja tuone 2010 kuna maajabu kidogo yataanza kutokea. By 2025 kutakuwa na Tanzania mpya kabisa. Mimi na wewe sijui kama tutakuwepo.

Mungu Ibariki Tanzania.
 
Asante unaweza kukadiria labda ni miaka mingapi maana ukimtaja nyerere ni miaka -12 mana hatunaye mungu amesaidia wewe upo. Pia labda miaka mingapi bado +10 au +100 au haitawezekana kabisa. Asante sana mkuu
Hiyo ita tegemea. Hauwezi kutabiri kitu kama hicho. Ina wezekana kiongozi kama huyo kasha zaliwa, ina wezekana yupo hata sasa ila haja pewa nafasi.
 
viongozi wazuri wenye uzalendo na inchi yao na wakweli kabisa wapo ila hawawezi kupenya kwenye ngome ya mafisadi wa ccm.
 
Hiyo ita tegemea. Hauwezi kutabiri kitu kama hicho. Ina wezekana kiongozi kama huyo kasha zaliwa, ina wezekana yupo hata sasa ila haja pewa nafasi.
tumsake huyo mnyima nafasi fast watanzania wajivunie kuwa kizazi cha kwanza ulimwenguni hata babu yetuzinjathropas ashangilie
 
viongozi wazuri wenye uzalendo na inchi yao na wakweli kabisa wapo ila hawawezi kupenya kwenye ngome ya mafisadi wa ccm.
pls consult me for a penetrative path on fraudulant checheme or both parties on private msg
 
Back
Top Bottom