Combination na Ephraim Kibonde, Gadner Habash na George Bantu, tayari imeyumba

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2014
Posts
7,427
Reaction score
10,905
Kwa wapenzi nguli wa kipindi pendwa cha mazungumzo ya jioni redioni cha JAHAZI katika redio MAWINGU FM watakubaliana nami kwamba muunganiko wa watangazaji hao watatu niliowataja ulifanya kipindi hiki kunoga...sasa kuondoka duniani kwa Kibonde tayari kumeleta Pengo kubwa sana kwenye kipindi hiki...nafahamu fika hakutapatikana mbadala wa Kibonde aamshe vyema hasa pale kwenye MASTORI YA TOWN...

To God be all the glory. Lala salama Kibonde shabiki wako nguli katika JAHAZI nitakukosa sana.
 
True that..ameondoka kibonde kuliziba pengo lake ni kazi..
 
Alikuwa anatuvusha sana kwenye foleni za barabarani na jahazi lake. Pumzika kwa amani Kibonde. MUNGU awalinde watoto wake.
 
Alikuwa anatuvusha sana kwenye foleni za barabarani na jahazi lake. Pumzika kwa amani Kibonde. MUNGU awalinde watoto wake.
Kabisa yaani ile jioni foleni unakuwa huioni jamaa akianza kupiga stori zake. Tuwaombee neema watoto wake waliosalia yatima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…