Come dine with me

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Nina business proposal ni TV program itarushwa kila wiki. Watu wanne kila wiki watakaribishana chakula, host atatengeneza a three course meal, marks zitatoka kwa kila mtu. Atakae score The highest atapata laki tano.

Wageni wanakuwa huru kuona mazingira ya nyumba ya host kuanzia chumbani. Wale wanaoanika vyupi chumbani tutashauri wazitoe mapema.

Ninatafuta TV Station tutakayo ingia Mkataba.
 
Uliwahi kutoa wazo tuwe tunakaribishana. Nahisi watu walisusa.

Naomba kazi ya kuandika script kwakua hakuna mtu atataka kuangalia watu wakipika na kula pekee. Itakua haina tofauti na kipindi cha mapishi.

Hivyo kutakua na kitu cha kujadili muda wa kupika na kula. Mostly itakua ni komedi au mada ya kufungua watu macho juu ya vitu fulani.

Pia kama itawezekana au kama haujapata naomba uniruhusu niorganize hadi crew ya kutengeneza kipindi. Hivyo nitakuletea mtu wa Kamera, edita wa video, mshika maiki, muandaa mandhari na wengine kwa kadri utakavyohitaji.

Natanguliza shukurani.
 
iko creative sana. Ila nasikia Tv imebaki TBC tu LOL!!. ila seriously iko poa sana hiyo, ila huoni wa mwisho kualika wenzake atashinda sababu atakuwa kisha waona na atapanga kuwapiga bao. Au recipe wanakupa kabisa mwanzoni na hakuna kubadilisha?
 
Yap kunatakiwa kuwa na kamada au zile ishu za game night.
 
Itakuwa tofauti na kipindi cha mapishi kwani unafanya matayarisho yote lakini unapika wageni wakiwa wameshafika ili was ile chakula kilichopoa. Wageni watakaribishwa na vinywaji.
 
Nobody wants to show off their crib to complete strangers let alone on national TV. Haiendani kabisa na utamaduni wa Mtanzania wa kawaida.
 
Kama uko serious na hii kitu, nicheki tuseme vema kidogo mpendwa. Maana siku hizi humu chai kibao sana
 
Wazo zuri sana umbuje. Ila nakushauri utafute tiivii za Kenya maana hizi zetu local hatuwezi kuziona ukiacha wachache sana wenye visembuse vya Ting
 
Itakuwa tofauti na kipindi cha mapishi kwani unafanya matayarisho yote lakini unapika wageni wakiwa wameshafika ili was ile chakula kilichopoa. Wageni watakaribishwa na vinywaji.
Unaonaje pendekezo langu?

Watu wanatulia kuwaangalia Kardashians wakila kwa sababu wanajua kuna mada zitajadiliwa mezani, mfano Baba kuamua kua mwanamke na Rob kuachana na Chyna.

Kama una plot twist idea yako ni bonge la dude.

Hongera
 
Hata sijaelewa sijui akili ndogo au haya mambo mageni kwangu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…