Mtanganyika
JF-Expert Member
- Jul 18, 2007
- 1,601
- 955
Waungwana hivi kwa nini hakuna mjasilimali alieanzisha commodity market in Tanzania? Hii itasababisha kustabilize price ya nafaka nyingi nchini, vilevile itawapa wakulima access na wateja direct.
Ethiopia wameanzisha, Kenya wamefanya hivyo. Kwa nini Tanzania tunalega lega?
Tuelezeni kwanza hiyo commodity market inafanya kazi vipi?
JF ni shule, wengine tunategemea kufunzwa humu humu...
Ni kama tu ilivyo Stock exchange market, na hii ya comodity market inakuwa na vitu hivyo hivyo
1. Wauzaji
2. Wanunuzi
3. Bei
Ila kwa Bongo kama mnavyo jua bei za mazao hupangwa na bod sijui za pamba, korosho na kazalika so kuwa na strong comodity market huku kwetu ni ndoto sana,
Na kuna comodity za aina mbili,
1, Hard commodity- hii ni kama madini, natural gesi, makaa ya mawe na kazalika
2. Soft Commodity- hii ndo ina vitu kama mazao means mahindi. pamba, mchele na kazalika