Comoro na Tanzania kushirikiana katika kilimo na uvuvi

Comoro na Tanzania kushirikiana katika kilimo na uvuvi

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
Balozi wa Tanzania nchini Comoro Mhe. Saidi Yakubu, amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Kilimo na Uvuvi wa Comoro, Mhe. Dkt. Stanley Ali Bandar. Mazungumzo yao yalijikita katika namna Tanzania na Comoro zinavyoweza kuboresha ushirikiano katika sekta hizo mbili za Uvuvi na Kilimo.

Balozi Yakubu alimueleza Mhe. Bandar kuhusu namna Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ilivyopiga hatua katika sekta hizo ambapo hivi sasa kuna mpango maalum wa ushirikishwaji vijana kwenye kilimo na upatikanaji wa vifaa vya kilimo. Aidha, alimkaribisha kutembelea Tanzania na kujionea hatua zilizopigwa.

Balozi Yakubu alitumia fursa hiyo kumwalika rasmi Waziri Bandar katika Kongamano maalum la ziara ya uwekezaji wa Sekta za Kilimo, Mifugo na Usafirishaji litakalofanywa na wafanyabiashara wa Tanzania Nchini Comoro tarehe 20-22 Agosti, 2024.

Kwa upande wake Waziri Bandar alimhakikishia Balozi Yakubu utayari wa Serikali ya Comoro kuendelea kushirikiana na Tanzania na kuwa anatambua bidhaa nyingi za chakula Comoro hutoka Tanzania na hivyo wataendeleza ushirikiano na kukubali mwaliko wa kukutana na wafanyabiashara toka Tanzania.

Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi za Wizara ya Kilimo na Uvuvi ya Comoro, tarehe 09 Agosti, 2024.
IMG-20240809-WA0094.jpg
IMG-20240809-WA0093.jpg
 

Attachments

  • IMG-20240809-WA0092.jpg
    IMG-20240809-WA0092.jpg
    128.7 KB · Views: 4
  • IMG-20240809-WA0095.jpg
    IMG-20240809-WA0095.jpg
    87.1 KB · Views: 4
  • IMG-20240809-WA0091.jpg
    IMG-20240809-WA0091.jpg
    89.6 KB · Views: 4
Ila Comoro na Tanganyika wana lao jambo sio bure au tunahusika na serikali ya Anjoun?
 
Back
Top Bottom