Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 1,278
- 797
Balozi wa Comoro nchini Tanzania, Mhe. Dkt. Ahamada El Badaoui ametembelea Ubalozi wa Tanzania mjini Moroni, Comoro na kufanya mazungumzo na Balozi wake, Mhe. Saidi Yakubu.
Katika mazungumzo hayo, Mhe. Balozi Badaoui ambaye pia ni Amidi wa Mabalozi nchini Tanzania alitumia fursa hiyo kuwasilisha salamu za pongezi za Comoro kwa Tanzania kufuatia ushindi wa Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile katika nafasi ya Ukurugenzi Mkuu wa Kanda ya Afrika wa Shirika la Afya Duniani (WHO),” ushindi wa Dkt. Ndugulile umepokelewa vyema hapa Comoro nasi tunamuahidi ushirikiano pale itakapohitajika na ni uthibitisho wa namna uongozi wa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan unavyokubalika katika medani ya diplomasia” alisema Balozi Dkt. Badaoui.
Kwa upande wake, Mhe. Balozi Yakubu alimshukuru Balozi Badaoui kwa ushirikiano na uungaji mkono wa Comoro katika kinyang’anyiro hicho na kumuahidi kufikisha salamu hizo nyumbani Tanzania.
Mazungumzo hayo pia yalijikita katika masuala kadhaa ya ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.