Stamico yaingia mkataba wa Sh1.2 bilioni na Tanesco kuzalisha umeme wa joto ardhi
MONDAY MARCH 01 2021
Meneja Mkuu wa Kampuni ya TGDC, Mhandisi Kato Kabaka
Summary
- Serikali yataka stamico kuharakisha mradi ili mradi wa umeme uanze utekelezaji.
Mbeya. Kampuni tanzu ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) ya uendeshaji nishati ya joto Ardhini (TGDC) imeingia mkataba wa Sh1.2 bilioni na Shirika la la Madini la Taifa (Stamico) kwa ajili ya kufanya utafiti wa umeme wa joto ardhi.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya TGDC, Mhandisi Kato Kabaka amesema leo Machi Mosi Jijini Mbeya wakati wa kusaini mkataba wa kuanza utekelezaji wa mradi huo ambao utakamilika kwa kipindi cha miezi mitatu na kuanza kufanyiwa Utafiti na uzalishaji wa nishati ya umeme.
Amesema kuwa visima hivyo vitatu vitakavyochorongwa katika Kijiji cha Mbaka wilayani Rungwe mkoani Mbeya vitafikia idadi ya visima vitano vitakavyokuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 200 za nishati ya umeme ambapo kati ya hizo 60 zitazalishwa kwenye mradi wa mbaka na viwili mkoani Songwe ifikapo 2025.
"Lengo la kuanza utekelezaji wa mradi huo na kutoa kandarasi kwa Stamico ni baada ya kubaini eneo hilo linazalisha joto nyuzi gredi 140 ambazo zitakuwa na uwezo mkubwa wa kuzalisha nishati ya umeme na hivyo Kusaidiana jamii kunufaika na nishati hiyo itakayotumia maji moto pamoja na uwekezaji wa viwanda vidogo ," amesema.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Stamico, Mhandisi, Venance Mwase amesema kuwa mkataba huo ambao wameingia na kusaini leo watahakisha unakamilika kabla ya miezi mitatu kutokana na umuhimu wake kwa jamii.
"Tunashukuru serikali kwa kuona Stamico inauwezo mkubwa wa kuchoronga visima hivyo na kwamba ili uweze kukamilika na kuanza kufanya kazi ndani ya miezi miwili. na mitatu kutokana na kuwa na vifaa vya kisasa ," amesema.
Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya ,Mariam Mtunguja ametaka uharakishwaji wa mradi huo kwa wakati ili kuwa chachu katika kuelekea uchumi wa viwanda kwa kuzingatia serikali imewekeza fedha nyingi za mradi huo.
Kampuni tanzu ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) ya uendeshaji nishati ya joto Ardhini (TGDC) imeingia mkataba wa Sh1.2 bilioni na Shirika la la Madini la Taifa (Stamico) kwa ajili ya...