Agrey998
JF-Expert Member
- Jul 8, 2019
- 417
- 550
Imekua kawaida kwa Bunge kupitisha miswada mbalimbali inayohusu maslahi ya walio wengi haswa wa kipato cha chini lakini miswaada hio imekua michungu mithilii ya siki katika Maisha ya wananchi wa Hali ya chini na umekua Kama utamaduni baada ya miswaada hio kupitishwa Raid anakuja kutengua miswaada hio Kwa kuifuta au kupunguza makali.
mwaka 2019 tuliona swala juu ya kikokotoo cha Pensheni za wastaafu, Jambo lililalamikiwa na wengi maana liligusa wastaafu wengi ambao Pensheni zao ndo zilikua mkombozi wao uzeeni lakini baada ya muda Rais akaja akaondoa kikokotoo.
Mwaka 2021 Bunge letu lilipitisha Sheria ya tozo za simu , wahanga wakuu katika swala hili lilikua wafanyabiashara wadogo wa huduma za kifedha na watu wa kipato cha chini ambao hutegemea miamala ya fedha kuendesha Maisha Yao , kilio kilikua kikubwa mpaka ikaundwa tume juu ya swala hili , wanasema tozo zimepunguzwa lakini bado makali ya Sheria hii yanatafuna biashara za wengi hasa masikini na hata CEO aliepita wa Vodacom alitamka wazi athari za Sheria hii kwenye MPesa.
Tozo za mafuta kupunguzwa
Bunge lilipitisha kupandisha tozo ya mafuta na kusababisha bei kupanda maradufu ilikua inashangaza kwamba Zambia wanategemea Bandari zetu kuleta mafuta katika nchi Yao lakini bei ya mafuta kwao ilikua ndogo kuliko apa , ilikua inashangaza Mtu kutoka Tunduma kwenda Zambia kununua mafuta Nadhan hata Zambia walikua wanatushangaa.
Kwa matajiri wala hutasikia wakilalamikia Sheria hizi maana wao wanapata economies of scale katika biashara zao Kwa kuwa wanafanya kwa wingi kwaio hata wakija wakicalculate Amount of Tax/levy per unit gharama unakuja ndogo tofauti na maskini anaezalisha unit chache na hata akipiga amount of levy per unit unakuja kubwa na kufanya gharama iwe kubwa zaidi na kumfanya auze Kwa gharama kubwa na alifanya Ivo ndo mwanzo wa wateja kukimbia na kwenda Kwa Tajiri anaezalisha Kwa gharama ndogo na kupelekea kuua biashara ya mtu masikini
Je, nini kifanyike
Nadhan Bunge letu lingejitahidi kuunda Sheria ambazo zinawezesha zaidi wafanyabiashara wadogo na watu wa Hali ya chini ili kupunguza income inequality Kwa Taifa maana Sheria zetu kwa kiasi kikubwa zina athari ndogo Sana Kwa matajiri.
Kufanya upembuzi yakinifu juu ya Sheria wanazoweka na madhara yake na manufaa yake. Hapa Nadhan kuna kamati za Bunge ambazo zina wataalamu ambao wangeweza kufanya utafiti mdogo juu ya Sheria hizo na kutoa majibu sahihi maana kazi zinazoenda kufanya na tume zinazoundwa baada ya tatzo kutokea zingefanywa na kamati za Bunge na kutoa majibu sahihi ambayo yangepunguza hata taharuki Kwa wananchi na pia hata wananchi wangekua na Imani juu ya watu waliowateua kuwawakilisha .
Nawasilisha Hoja . Kuwa mzalendo, ipende Nchi yako