Computer science v/s computer engineering

Brother James

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2012
Posts
233
Reaction score
172
Nilikuwa napita pita katika TCU website hususani katika kitabu cha sifa za kudahiliwa katika fani fulani na kuangalia sifa za vyuo mbali mbali za kuingilia katika fani mbali mbali. Nimekutana na sifa za kuingilia fani za za BSc. Computer Science na BSc. Computer Engineering lakini nilichokiona nikaona nisinyamaze kwa sababu nilishindwa kuelewa nikaona niilete hii mada hapa labda wana JF mnaweza kunisaidia kwani yawezekana kuna vitu vya msingi vinavyoangaliwa hadi kufikia kila chuo kuwa na sifa mbali mbali za kuingilia katika fani zinazofanana.

1. Nilipita karibia kila chuo kinachodahili fani tajwa na kuona tofauti kubwa tu kwenye sifa za kuingilia katika hizo fani japo cut-points zao zinafanana zinaanzia 2.0 hadi 3.5. Mfano UDSM wanataka waliofaulu katika PGM, PCM na equivalents za Diploma in Computer Science/IT, UDOM wanataka watu waliofaulu katika EGM, PGM, PCM na equivalent za Dip. in IT/Comp. Science, ST Joseph wanataka waliofaulu (BSc. Comp. Science) katika EGM, PGM, ECA, HGE na Equivalents, St. Joseph (BSc. Comp. Engineering) wanataka waliofaulu ktk PCM na Equivalent tu, Ruaha University wanahitaji waliofaulu katika PCM, EGM, PCB, CBG na equivalents za Comp. science/IT, n.k; Swali langu je nini tafsiri ya hizi tofauti za kuingilia ktk the same programme kwa wanafunzi wanaosoma mtaala wa aina moja??

2. Wengi wa wanachuo wanaodahiliwa katika katika fani hizi kupitia equivalents za Diploma in IT/Comp. Science ni wale waliosoma katika fani za sanaa (Arts Combinations)baada ya kusoma courses za diploma katika vyuo kama UCC, DIT,IFM etc. ndio wanao onekana wapo vizuri zaidi wakidahiliwa ktk fani za computer ukilinganisha na wale direct from schools tena waliosoma PCM ,EGM, PGM, PCB na CBG's, Je Vyuo vyetu havioni kwamba ni wakati muafaka wa kutoa fursa sawa za kudahiliwa kwa wanafunzi waliosoma hata fani za Arts ili mradi tu wawatengee mwaka mmoja wa pre-University katika fani husika?? nimeshuhudia kupitia vyuo vingi tu, hawa (PCM, PGM, PCB, EGM n.k) wetu wakipata shida za kufaulu kwenye hizi fani sambamba kabisa na wale waliosoma arts (Tembelea UCC, St. Joseph, UDOM, IAA, DIT, IFM n.k utawakuta). Hata hivyo pamoja na ugeni wa fani hizi ktk mitaala ya kitanzania (no foundation at all) hususani ktk shule za msingi na masekondari lakini compter courses si ngumu.

3. Ndugu wadau, Je unadhani kuna haja ya kutenganisha sifa za kuingilia katika BSc. Computer Science na BSc. Computer Engineering?? FUNGUKA KAMA UNA MAWAZO MAZURI KWA AJILI YA KUNISAIDIA NA PIA KUVISAIDIA VYUO VYETU NA JAMII NZIMA YA KITANZANIA
####KATIKA KUJENGA POINTS ZAKO UNAWEZA KULINGANISHA FANI NYINGINEZO UNAZOZIFAHAMU ILI KUONA KAMA KUNA HAJA YA KUFANYA MABADILIKO PIA KTK HIZO FANI&SIFA ZA KUINGILIA####

NAOMBA KUWASILISHA
 
upo sahihi kwa kiasi fulani, ni kweli kua kuna watu walisoma arts na wakasoma course za computer na wakimiza mbaya kuliko wale waliyosoma science
 
1: Kila chuo kina sylabus yake pamoja na kuwa jina digrii husika linafanana katika vyuo vuote. IT ni pana sana hivyo kuna uwanja mkubwa wa vyuo kuchagua nini cha kufundisha ingawa kuna baadhi kozi ni basic lazima zifundishwe.
2: Si kweli kwamba IT ni rahisi na hata mtu aliyesoma arts anakimbiza. Ijulikane wazi kuwa basic kubwa ya hizo kozi ni hesabu iwe ulisoma pure mathematics, basic mathematica au o,level mathetics. Ufaulu wa hesabu ndio unaozingatiwa kwani tunaamini kuwa mtu anayejua hesabu ni yule mwenye reasoning kubwa, asiyekariri na computer inahitaji mtu wa namna hiyo hasa ukija kwa upande wa programing, network securitiy na hata databases. Hivuo hesabu ni muhimu.
3: Ni kweli wapo watu waliosoma arts na wanasoma IT lakini ukiangalia background unakuta wamesoma hesabu ndani yake ingawa kwa kiasi kikubwa huwa ni watu wa kukariri na si watu wa kufikiria.
4: Ukija ukiangalia kwenye soko la ajira za IT, passmark haziangaliwi sana. Kikubwa kinachoangaliwa ni uwezo wa kudeliver service na sio uwezo wa kuonyesha A's kwenye vyeti. Ndio maana usishangae mtu ana GPA ya 4.5 anaachwa na mtu wa GPA ya 2.7 kwenye ajira. Practical intelligence inajalisha zaidi kuliko hizo paper intelligence.
 

Uko sahihi kabisa mkuu bila kua na background ya hesabu hapo nyuma huku ni majanga kuna binary calculations na nyingne kibao.kila somo nalogusa nakutana na hesabu na pia ukikariri ukichengwa kidogo umekosea swali zima ukikosea herufi moja program yote chini mimi kuna watu nasoma nao yani unaweza waonea huruma
 
chuo gani kikali kwa hayo mambo.na ipi facult kali kwa mtu anyependa mautundu ya computer basing on software
 
chuo gani kikali kwa hayo mambo.na ipi facult kali kwa mtu anyependa mautundu ya computer basing on software

bachelor of science in software engneering Udom..... ila uwe tayari kuumiza kichwa
 
Nimefarijika kwa maelezo yako mazuri, pia nimetambua kuwa msingi wa hizi fani zote mbili ni kuwa mzuri katika calculations. Pamoja na maelezo yako mazuri naomba niulize hivi; Kama somo la Hisabati ndio funga kazi mbona kuna vyuo vinaangalia masomo makuu mawili tu, yaani Physics na Math, Je combinations zingine kama EGM huoni kama physics haipo hapo?? ni kwanini basi watake uwepo wa physics kwa kiasi kikubwa angali physics haina calculations nyingi kama maths yenyewe??
Nimejaribu pia kupitia courses za IT/Computer science katika vyuo mbali mbali nikagundua most of them zaidi ya 75% courses wanazo fundisha zinafana, iweje leo sifa za kuingilia zifanane??
Watu wa PCB, HGE,CBG, CBA, aidha wamesoma hisabati na kufanya vizuri tu kule O-level na pia wameendelea kusoma Basic Applied Mathematics wakiwa A-Level, Je kwanini wasiwe miongoni mwa waombaji wa fani za computer kama kweli hisabati ndio sifa ya mtu kuchaguliwa?? Mfano mzuri pale UDSM wanataka watu wa Computer Science wawe na ufaulu katika masomo mawili tu fixed (Mathematics&Physics), tafsiri yake ni kwamba hatutaki muombaji wa aina yoyote zzaidi ya mtu aliyesoma PM. Je haya masomo yanayoambatana na PM hayana maana kabisa ktk fani za computer hadi wanayatenga na kuona si ya kupewa nafasi??

 

Mkuu nikuambie tu kuwa mie nimesoma Computer Science na nikapata upper second class. O'level nilifanya vinzuri sana but advance sikufanya vinzuri na nilisoma PCB. Nilisoma certificate in Computer Science na nikafaulu vyema kwa kupata "Distinction" na nikapata nafasi ya kuingia degree na kumaliza kwa kupata upper second class. Katika darasa nililosoma, kulikuwa na watu waliosoma advance HGE, EGM na hata CBG. Ukiangalia vyeti vyao ni kuwa walisoma basic applied mathematics (BAM) na O'level walipass vinzuri mathematics. Na nikuhakikishie kuwa hao jamaa walipata mkopo na hata mimi nilikuwa na mkopo wa asilimia 80%. Sasa nikija kwenye hoja yako, mimi kwangu sioni umuhimu sana wa Physics kwa mtu anayesoma Computer science kwani kama ni ishu ya electronics hiyo kozi ipo na inafundishwa kwenye mwaka wa kwanza wa masomo. Kwetu ilikuwa inaitwa Digital system. Hata hivyo bado ndani ya hiyo kozi kilichokuwa kinaendelea ni hesabu za binary number, hexadecimal numbers na nyingine. So phyisics inachukua nafasi kidogo. Ukija upande wa programming, networks, systems security, computer architecture, operating systems, bado sikuona kama kuna application kubwa ya phyisics. Sehemu kubwa ni hesabu ndio unatakiwa uwe vinzuri kwa sababu unatumia sana "Logic or reasoning". Sina uhakika kwa Computer Engineering kwani sijajua syllabus yake ikoje lakini kama jina linavyojionyesha yawezekana Physics ni muhimu.
Kwa upande wa UDSM, wale huwa wana policies zao ambazo wanapenda kuwa tofauti na vyuo vingine hata kama hakuna ulazima huo. Mfano mnzuri mimi chuo nilichosoma (Ruaha University College – RUCO) kilikuwa kinatumia syllabus ya UDSM, na Dr. Syllvanus Kitinya (kwa waliosoma Computer Science UDSM kuanzia 2005 kushuka chini wanamfahamu) ndiye alikuwa Dean wa kitivo cha IT. Watu wenye sifa kama za kwangu UDSM walikosa nafasi but RUCO tulipata nafasi na mkopo tukapata, na kwenye masomo tukafanya vinzuri practically na theory.
 
Nimepata kitu kizuri toka kwako maboso, pls tuwasiliane kwa kupeana maujuzi zaidi, nitupie contacts hapa: tanzania.james@yahoo.co.uk, don't ignore friend
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…