Comrade Ali Sultan Issa: A Revolutionary Icon

Enzi hizo polisi tukiingia mtaani watu wanatimka kuingia majumbani, tulikuwa tunaogopwa.
Hebu atuambie ukweli maana kulikuwa na fununu kwamba jamaa fulani wakiingia mtaani huwa wanatafuta vibinti vya kupeleka kwa waheshimiwa sana wa enzi zile. Ndiyo maana (hasa wasichana wa kiarabu na kihindi) wakitimua mbio za uhakika.

Na yule jamaa jina lake Fumu (marehemu) atupe hizo stori zake pia.......
 
Saturday, February 16, 2013

Comrade Mohammed Ali Foum


Picha : Balozi Mohammed Ali Foum

Mwanzoni mwa Mwezi huu Tanzania ilipata pigo zito mno lislopata mithilika, aliyekuwa Balozi wetu wa Kudumu katika Umoja wa Mataifa Mzee Mohammed Ali Foum aliiaga Dunia Jijini Cairo Nchini Misri.

Balozi Foum (Juni 4, 1936 - Februari Mosi, 2013) ni Mzalendo wa kupigiwa mfano wa Tanzania ambaye aliitumikia Nchi hii, Afrika na Dunia kwa Ujumla kwa Moyo wake wote na Utumishi wa Kutukuka.

Aliteuliwa na Rais Nyerere kuwa Balozi wetu wa kudumu katika Umoja wa Mataifa Mwaka 1984 na akajitambulisha Rasmi kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Javier Perez de Cuellar Tarehe Septemba 14, 1984 kama anavyoonekana Pichani katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York Nchini Marekani.

Ufuatao ni Wasifu Mfupi wa Mema mengi yaliyotendwa na Balozi Mohammed Ali Foum hapa Duniani ambao nimeuhariri kidogo kutoka kwenye Wasifu wa awali ulioandikwa na Mwandishi Nguli na Gwiji, Bwana Amhed Rajab. Wasifu husika ulikuwa ni sehemu ya Tanzia ya Kifo chake ambao ulichapishwa katika Gazeti la 'Raia Mwema' tolea namba 281 la Mwezi huu.

MOHAMMED ALI FOUM: MZALENDO WA KINZANZIBARI NA MSIRI WA NYERERE.

KOMREDI WA KWELI.

Mohammed Ali Foum aliyefariki dunia jijini Cairo Ijumaa usiku, atakumbukwa kama mwanamapinduzi na shujaa aliyepigania "Uhuru wa Zanzibar" na kuchangia mengi katikaM juhudi za kulikomboa Bara la Afrika.

Wengi waliokuwa wakimfahamu juu juu, hawakuutambua mchango wake uliokuwa adhimu katika harakati za ukombozi wa Afrika. Hayo si ya ajabu kwa kuwa Foum hakuwa mtu wa kujionyesha na akipendelea kuuficha umahiri wake hasa katika nyanja ya diplomasia.

Nikimfahamu tangu kufungua kwangu macho kwani sote tulizaliwa Vuga, Mji Mkongwe, Unguja. Alikuwa ni mmoja miongoni mwa kaka zetu wa Vuga waliowashajiisha wadogo zao mtaani wawe na moyo wa kuwa pamoja.

Mwenzake mmoja katika hili, alikuwa Salim Hakim, ambaye sasa ni mmoja wa mabalozi wanaosifika wa Omani. Baadaye wote wawili walikuwa mabalozi katika Umoja wa Matifa, Foum akiiwakilisha Tanzania na Hakim akiiwakilisha Omani.

Katika miaka ya hivi karihuni wakawa tena pamoja wakiishughulikia Somalia. Foum alikuwa Mwakilishi wa Muungano wa Afrika, na Hakim alikuwa Mwakilishi wa Umoja wa Kiarabu (Arab League). Lakini huko utotoni waliwatia ari watoto wa Vuga waunde timu ya soka ya Young Brothers. Nakumbuka hao wawili na wenzao wa rika lao, walikuwa na tabia ya kuitana kwa kupiga mbinja au mluzi, kama wasemavyo Bara.

Tangu utotoni, Foum alikuwa si mtu wa kukaa nyuma, Daima akipenda kushirikiana na wenzake mtaani na pia skuli. Ingawa hakuwa pocho Foum aliamua kukatiza masomo yake ya sekondari na kuanza kufanya kazi katika Ofisi ya Leba ambako pia akifanya kazi Ahmed Diria Hassan. Baadaye Diria naye atakuja kuwa mmoja wa mabalozi madhubuti wa Tanzania.

Foum alianza kuzivaa siasa alipojiunga na chama cha Hizbu, yaani Zanzibar Nationalist Party (ZNP). Chama hicho kilimpeleka Havana Cuba kwenda kufungua ile iliyokuwa ikiitwa Ofisi ya Zanzibar. Huko alikuwa pamoja na Kanali Ali Mahfoudh na Komredi Salim Ahmed Salim ambao alijiunga nao kwa muda mfupi. Nyumba yao mjini Havana, ambayo pia ilikuwa ni ofisi yao, ilikuwa katika eneo la Vedado ambako wakiishi Wacuba wa tabaka la kati. Sehemu moja ya nyumba hiyo ilikuwa ofisi ya chama cha ANC cha Afrika ya Kusini.

SOGELEA UKOMBOZI.

Foum na wenzake waliwasili Havana si muda mrefu baada ya Fidel Castro na Che Guevara kuuteka mji huo katika Mapinduzi yaliyomwondoa Fulgencio Batista madarakani. Tayari wakati huo Foum alikuwa amekwishaanza kuzikumbatia siasa za mrengo wa kushoto. Huko Cuba pia alikuwa akihudhuria mafunzo ya kijeshi yaliyokuwa yameandaliwa mahsusi kwa vijana Wakikomred kutoka Zanzibar, waliokuwa wakifunzwa namna ya kupindua Serikali.

Baadaye vijana hao pamoja na kina Foum, Ali Mahfoudh na Salim Ahmed walijiunga na chama cha Umma Party cha Abdulrahman Babu na kushiriki katika Mapinduzi ya 1964. Waandishi wa habari kutoka nje waliofika Zanzibar baada ya Mapinduzi na kuandika kwamba walikuwako Wacuba huko, walikuwa kwa hakika wakiwazungumza kina Foum na makomred wenzake waliorejea kutoka Cuba na waliokuwa wakizungumza Kispanyola.

Mwaka 1963 walipokuwa bado Havana, Foum na Ali Mahfoudh waliandika kijitabu kilichoitwa: ‘Forge Ahead To Emancipation’ (Songelea Ukombozi) kilichozungumzia vuguvugu la Zanzibar la kuupinga ubeberu.

Historia ya Umma Party, inaonyesha kwamba Ali Sultan Issa, Foum, Mahfoudh na Salim Rashid ndio waliokuwa wakimshadidia zaidi Babu wakiache mkono chama cha ZNP.

UGWIJI KATIKA DIPLOMASIA, UFASAHA WA MANENO KATIKA KURAI NA UAMINIFU KATIKA KUTUNZA SIRI.

Katika miezi ya mwanzo ya Mapinduzi, Foum alikuwa pamoja na Mahfoudh kwenye kambi ya kijeshi na baada ya kuundwa Muungano, akateuliwa awe mshauri (counselor) katika Ubalozi wa Tanzania, New York. Hapo ndipo Foum alipoanza kazi zake za kidiplomasia na kuanza kung’ara katika shughuli hizo. Rais Julius Nyerere alimteua awe Balozi wa Tanzania India, Italia na pia katika Umoja wa Mataifa. Foum aliwahi pia kuwa waziri mdogo wa mambo ya nje.

Nyerere akimuamini sana, na Foum alikuwa ni msiri wake mkubwa, na hasa kuhusu shughuli za kimataifa. Mara nyingi Mwalimu Nyerere alikuwa akimtuma kuonana na viongozi wa nchi nyingine alipokuwa ana mambo nyeti yaliomfanya awasiliane na viongozi hao. Yeye mwenyewe Foum, alikuwa na uhusiano na wanaharakati mbalimbali wa kimataifa.

MAFUNGAMANO NA MALCOLM X PAMOJA NA WAPIGANIA HAKI, USAWA NA UTU WENGINE.

Miaka michache iliyopita nilimpelekea baruapepe Amiri Baraka, Mshairi, Mwandishi na Mwanaharakati wa Kimarekani mwenye asili ya Kiafrika na nikamuuliza lini alikutana mwanzo na Babu. Baraka (ambaye zamani akijulikana kwa jina la LeRoi Jones) alinijibu: “Nilikutana naye Astoria Hotel, New York, mwaka 1964 wakati uleule nilipokutana mwanzo na Malcolm X”.

Wakati huo, Foum tayari alikuwa New York na alikuwa Mtanzania wa mwanzo kujuana na Malcom X na halafu akamjulisha kwa Babu aliyekuwa akidhuhuria kikao cha Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Gamba la albamu moja ya hotuba za Malcolm X lina picha ya Foum na Babu wakiwa pamoja naye Malcolm X. Ninajua kwamba Babu aliwahi kuiona albamu hiyo na gamba lake, lakini Foum hakuwahi kuiona.

Miaka miwili iliyopita tukiwa pamoja Nairobi alinishikiia nimtafutie gamba la albamu hilo. Moja ya masikitiko yangu ni kwamba sikujaaliwa kumtimizia haja yake. Usuhuba wa Foum na Malcolm X ulikuwa mkubwa kiasi cha kuwafanya wawe wanatembeleana majumbani mwao. Mwengine aliyekuwa akimtembelea Foum nyumbani kwake New York alikuwa mwanamapinduzi wa Cuba Che Guevara. Kwa ujasiri wake na licha ya kujuwa kwamba akiandamwa na majasusi wa CIA wa Marekani Foum alikuwa akifuatana bila ya kificho na Malcolm X pamoja na Che.

FOUM, KIASHIRIA CHA UTU, HESHIMA NA SERA ILIYOTUKUKA YA MAMBO YA NJE YA TANZANIA.

Kwa hilo na pia kwa harakati zake za kupinga ukoloni na ubeberu Foum alikuwa heshi kuwakera Wamarekani. Aliwakera sana kwa msimamo wake imara wakati mijadala ya vikao vya Kamati ya 24 ya kuufyeka ukoloni duniani. Foum aliteuliwa kuiwakilisha Tanzania katika kamati hiyo.

Mfano wa jinsi Wamarekani walivyokuwa wakimuona kuwa ni mkorofi ni telegramu moja kutoka ujumbe wa Marekani katika Umoja wa Mataifa iliyopelekwa kwenye wizara ya mambo ya nje ya Marekani. Telegramu hiyo iliandikwa Novemba 26, 1968, wakati Marekani ilipokuwa ikizingatia kujitoa kutoka kwenye Kamati ya 24.

Ilisema hivi: “Maazimio kama hayo yanatungwa hasa na Waafrika wenye siasa kali — kama Foum (Tanzania) wakisaidiwa na Masovieti na Waarabu wenye siasa kali kama Syria na Iraq”. Diplomasia kama ilikuwa katika damu yake na inaonyesha alimrithisha mdogo Abdillahi ambaye mwaka jana tu alistaafu akiwa balozi mdogo wa Sweden mjini Addis Ababa.

WATU WEMA HAWACHOKI KUWATUMIKIA WENZAO.

Yeye mwenyewe Foum aliendelea na shughuli za kidiplomasia hata baada ya kustaafu serikalini. Novemba 22, 2002, Amara Essy, Mwenyekiti wa muda wa wakati huo wa Muungano wa Afrika (AU), alimteua awe mjumbe wake maalum nchini Somalia. Foum alijipatia sifa kwa uchapaji kazi wake na kwa jitihada zake wakati wa Mkutano wa Somalia wa Kuleta Suluhu ya Kitaifa uliofanywa nchini Kenya toka Oktoba 2002 hadi Oktoba 2004.

Alikuwa mbioni pia wakati wa jitihada nyingine zilizochukuliwa baadaye na jumuiya ya kimataifa kujaribu kustawisha amani na kuleta suluhu nchini Somalia. Aliuacha wadhifa wa kuwa Mwakilishi Maalum wa Muungano wa Afrika kwa Somalia mnamo 2007 na mahala pake pakashikwa na Nicolas Bwakira kutoka Burundi.

Baadaye kama miaka miwili hivi iliyopita alichukuliwa kwa muda na Augustine Mahiga, mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika Somalia, awe mshauri wake. Aliiacha kazi hiyo mwaka jana akishughulika na biashara. Ujuzi wake wa siasa za Somalia na majungu ya wanasiasa Wakisomali ulikuwa wa kupigiwa mfano. Binafsi nilifaidika nao nilipokuja kuishi Nairobi na kusimamia mradi mmoja wa shirika la UNDP la Umoja wa Mataifa kuhusu kielelezo cha katiba mpya ya Somalia.

Alinishauri na kunielekeza wapi pa kupiga hodi ili kazi zangu kuhusu Somalia zifanikiwe. Wakati mwingine akinishauri hata bila kuomba ushauri wake. Huo ni mfano wa sifa nyingine aliyokuwa nayo — ya ukarimu na kutokuwa na uchoyo.

WEMA HAWADUMU ULIMWENGUNI, MOLA AMLAZE PEMA MCHAMUNGU MOHAMMED ALI FOUM.

Hizo zote ni sifa za mcha Mungu, na Foum alikuwa mtu wa aina hiyo kama marehemu baba yake, Inspekta Ali Foum.

Safari moja nikiwa Jeddah, Saudi Arabia, mfanyakazi mmoja katika Ubalozi mdogo wa Tanzania aliniambia kwa masikitiko: “Sijui Foum mzima kwa sababu haipiti mwezi hutokea hapa kuja kufanya umra Makkah. Mwezi huu sijamuona”.

Ama mimi sitomuona tena siku za Ijumaa katika Msikiti wa Hurlingham hapa Nairobi.

"Hakika sisi ni Miliki ya Mungu, na Hakika kwake tutarejea", Mola amlaze Pema Mja Mwema huyu.

zanzinews.com
 
Comrade Salim Ahmed Salim akiwa katika majukumu yake ya kimataifa


July 1990
Addis Ababa

Comrade wa umma party wa Zanzibar aliyekuja kuwa katibu mkuu AU Dr. Salim Ahmed Salim wa Umoja wa Afrika akipokea viongozi mbalimbali walipowasili kwa mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika rais Sam Nujoma

African heads of States arriving in Addis Ababa for OAU meeting July 1990

Italy - Talks on Zaire crisis

(7 Nov 1996) T/I: 10:55:22 The secretary-general of the Organisation of African Unity (OAU), Salim Ahmed Salim, on Thursday (7/11) said any international response to the Zairean crisis should be co-ordinated by the UN Security Council. Speaking after a meeting in Rome with Italian foreign minister Lamberto Dini, Salim said it was important that any proposals have lasting impact. SHOWS: ROME, ITALY, 7 NOVEMBER, 1996 SOT Secretary General of the Organisation of African Unity (OAU) Salim Ahmed Salim SAYING I would hope that the french and spanish proposals will be taken in the context of what happened in the security council. we prefer a security council action because this can facilitate greater participation of the international community. I am told that the security council will make a decision soon because it is not one of those situations where one can afford the luxury of time. the longer this goes on the more people will suffer. EXT Italian foreign ministry; Dini walking to microphones; Italian Foreign Minister Lamberto Dini, saying we in Italy will play our part in a coordinated fashion with the other European countries
 
Hizbu bado mpo tu na ndoto yenu.Ni vigumu kwenu kuitimiza na sababu mnaijua.Anyway rest in peace comrade.
 
Mh karume hakua mjinga kukataa maoni ya makomredi,na inajulikana kwanini alikataa ideas za makomredi shirikishi.
 
Mh karume hakua mjinga kukataa maoni ya makomredi,na inajulikana kwanini alikataa ideas za makomredi shirikishi.

Ma-Comrade inaonekana walikuwa na akili nyingi sana.

11 Feb 1980) Tanzanian Minister of Foreign Affairs, Salim Ahmed Salim, holds a press conference on the delevlopments in Zimbabwe Rhodesia
 
Ma-Comrade inaonekana walikuwa na akili nyingi sana.

11 Feb 1980) Tanzanian Minister of Foreign Affairs, Salim Ahmed Salim, holds a press conference on the delevlopments in Zimbabwe Rhodesia
Akili wapi mkuu??????Walikua na ajenda yao nyuma ya pazia.Ndio maana karume akawakataa.
 
Comrade comandante Fidel Castro wa Cuba mapokezi 'live' ziara yake nchini Tanzania

Cuban leader Fidel Castro Receives Hero's Welcome in Tanzania Dar es Salaam 1977

View: https://m.youtube.com/watch?v=C0ix0gML9ak
Comrade comandante Fidel Castro wa Cuba aliyekuwa na ushawishi mkubwa kwa makada wa vyama vya siasa vya makomredi wa Zanzibar ambapo vijana kabla na baada tu ya mapinduzi matukufu ya 1964 walikwenda Cuba kwa mafunzo. Hapa video ikionesha mapokezi ya Fidel Castro alipotua Tanzania 1977 live / mubashara
 
Akili wapi mkuu??????Walikua na ajenda yao nyuma ya pazia.Ndio maana karume akawakataa.


Tovuti ya balozi Salim Ahmed Salim

27 September 2023

Tanzanian President Samia Suluhu will oversee the launch of the archive of Dr Salim Ahmed Salim, a well known diplomat.

View: https://m.youtube.com/watch?v=GgSSVlkbHgg
Source : SABC News
 
30 September 2023
Dar es Salaam, Tanzania

Tanzanian President inaugurates the Dr. Salim Ahmed Salim's Digital Archives

View: https://m.youtube.com/watch?v=bLTQuNAnsZwPresident Samia Suluhu Hassan has inaugurated the Dr. Salim Ahmed Salim Digital Archives in Dar es Salaam today.Dr. Salim is an eminent international diplomat, previously held the esteemed positions of the fifth Prime Minister of the United Republic of Tanzania and the eighth Secretary-General of the Organisation of African Unity (OAU) from 1989 to 2001. Our correspondent Isaac Lukando joins us live from Dar es Salaam

Source : SABC News
 
OAU Secretary General Press Conference in Nairobi 1990


View: https://m.youtube.com/watch?v=QbZclZlCOCADr. Salim arrives in Nairobi Kenya and has a press conference at the JKIA airport in June 1990. He was en route to Madagascar to attend the 30th anniversary of the country's independence.

Source : Salim Ahmed Salim
 
16 September 1989
Dar es Salaam, Tanzania

Press Conference at the Center of Foreign Relations Tanzania


View: https://m.youtube.com/watch?v=LZ1RcPxD1c8Dr. Salim participates in a press conference hosted by the Center of Foreign Relations in Dar es Salaam, Tanzania. The press conference took place on September 16, 1989 - only three days before assuming the post as Secretary General of the OAU in Addis Ababa.

Source : Salim Ahmed Salim
 
28 September 2023
President Thabo Mbeki shares his experiences with Dr. Salim Ahmed Salim.


View: https://m.youtube.com/watch?v=JQfNwPYKJK0
Source : Salim Ahmed Salim

Annual Thabo Mbeki Africa Day Lecture 2014 : Defining the Leadership Paradigm for a new Africa by Dr. Salim Ahmed Salim


View: https://m.youtube.com/watch?v=Rw2AhvtkRuEDr. Salim is the guest of honor at the 5th Annual Thabo Mbeki Africa Day Lecture held on May 23, 2014. Dr. Salim spoke about 'Defining the Leadership Paradigm for a new Africa
Source : Salim Ahmed Salim
 
Africa Peace Award Presentation to President Nelson Mandela


View: https://m.youtube.com/watch?v=u0_veIPPnTgMarch 18, 1995 President Nelson Mandela received the Africa Peace Award. The event was presented in Durban and Dr. Salim Ahmed Salim, then OAU Secretary General, had the honor of presenting the awardd to President Mandela. The event was jointly sponsored by the African Centre for the Constructive Resolution of Disputes (ACCORD) and the OAU.
Source : Salim Ahmed Salim
 
FIDEL CASTRO ALIPOHUDHURIA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA UN-GA MWAKA 1979


Picha kwa hisani kubwa ya tovuti : salimahmedsalim.com
 
Cairo, Egypt 1964

Mwaka 1964 balozi mteule Salim Ahmed Salim wa Tanzania akikabidhi hati za utambulisho kwa Raisi Gamal Nasser wa Egypt


Picha kwa hisani ya tovuti : salimahmedsalim.com
Balozi Salim Ahmed Salim mwaka 1964 alikuwa na umri wa miaka 22 .
 
Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania umoja wa mataifa balozi Salim Ahmed Salim mwaka 1970 akiwasilisha hati za utambulisho kwa katibu mkuu wa UN


Picha kwa hisani ya tovuti : salimahmedsalim.com
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…