Elections 2010 CONFIRMED: Kigwangala atangazwa rasmi mshindi Nzega

bahati kupewa mzigo mbona wengine hawajapewa 😡
 

huyu mkuu hata hajijui kama anaamini kuwa bahati ndo ilomfikisha hapo alipo au spirit yake binafsi. (walompigia kura hajawahusisha kabisa kwenye mafanikio yake)

na inaonyesha bado hajaamini, manake posti nzima hamna sentensi ilomaliza na nukta, kama hashangai yeye basi anauliza suala.
 
hongera lakini "naomba ufafanuzi unaposema hii ni " bahati"..
 
Mkuu Kigwangalla,

Hongera sana kwa kushinda huko Nzega. Muhimu kwasasa sio kuangalia nani alisema nini huko nyuma bali kuwaonyesha wote waliokupinga kwamba una uwezo kwa kuchapa kazi kwa vitendo na kuwasaidia wananchi wa Nzega.

Kuanzia sasa mafanikio yako yatatokana na matendo yako wala sio hisia au propaganda za watu wachache. Ukifanya vitendo vya ufisadi itajulikana, lakini pia ukifanya matendo ya kuijenga nchi yetu itajulikana pia.

Usipoteze muda mwingi sana kulaumiana na wana JF maana wengi wetu tunaamini tunachokisoma magazetini bila hata kuwajua wahusika wenyewe. Tumia changamoto za hapa JF kama mtaji wa kukusukuma mbele kutimiza majukumu yako.

Hiyo kazi ya uwakilishi ni mzigo mkubwa mno na kama hujajipanga vizuri unaweza kukulemea mpaka ukadondoka. Lakini pia ni fursa kubwa maana inakupa nafasi ya kuonyesha kwa matendo juu ya uwezo wako wa kuchapa kazi pamoja na maadili yako.

Hongera sana mkuu.

 

Mi sio mshabiki wa CCM wala sijapiga kura zaidi ya miaka 10 tanzania Nipo hapa America na sitegemei kurudi bongo. Ila kama ningekua napiga kura nisingepigia CCM, sio kwamba siipendi CCm ila napenda pawe na upinzani wenye nguvu kama hapa America. Ningependa wapinzani washinde viti vingi ili pawe na uwiano wa madaraka. Huyu bwana Kingwangale nimemsikia sana hasa kwenye face book tangu anagombea. Ila nafikiria kuna watu wana wivu au chuki binafsi nae. mbona watu hawataki ashinde, hao wabunge wote walioshinda wa CCM kina Makongoro, Lowasa mbona watu hawawasakami. muacheni huyu kijana bahati yake imemuangukia. Hakushinda kura za maoni wala hakuwa wa pili na akapitishwa. Hizo ni bahati tuu za uongozi kama ilivyomtokea Obama. mambo ya kumsakama kama vile ananuka muacheni afanye kazi, You never know what future holds may be he will be one of our future leader. Siasa za visasi na kufuatiliana achana nazo. Ameshashinda ubunge muacheni afanye kazi, 2015 ipo kama mtamuona hafai wache watu wa Nzega wamtoe. Mbona kina Sugu wameshinda na hakuna mtu anawafuata. Wengi wenu hamtaki kujaribu kugombea uongozi ila mtu anapojaribu na kufanikiwa mnamuwekea visa. Uchaguzi umekwisha bahati imemuangukia muacheni afanye kazi. God bless you Kingwangale
 
Teh teh teh teee umenikumbusha mbali kweli! nakumbuka ishu hiyo ilikwa patashika nguo kuchanika!!
 
BORA AMETEULIWA KUWAONGOZA WAJINGA WA NZEGA ILA SIO MIMI. ANGECHAGULIWA KWENYE JIMBO LANGU MI NINGEHAMA.MNAFIKI MKUBWA HUYU ETI ANA DHAMIRA SAFI,KAMA ANADHAMIRA SAFI KIVIPI ANAKAA NA WALA RUSHWA?
DHAMIRA GAni safi atakayoitumia kupambana na wala rushwa waliomuweka hapo?
akwende zake huko
 
hongera ndugu. Inaelekea unafurahia kwamba umepata bahati kuwa mbunge. Lakini, je unafurahia bahati ya nini? Unaonyesha kama unafurahia bahati ya kupata ulaji na si kutetea maslahi ya watu wa jimbo lako na Tanzania kwa jumla. Umesema we ni mhangaikaji, unahangaikia tumbo lako au watu wa Tabora. Inatia shaka sana!

Inavyoonyesha huijui Tabora, jimbo lako na wala huwajui watu wa Tabora na wa jimbo lako kwani umesema mwenyewe kuwa ilibidi ufanye kampeni za nguvu mpaka watu wakakufahamu!

Unasema jimbo ilikuwa linaonekana kama lingeenda kwa CHADEMA, je kwa mwenendo wa uchakachuaji wa CCM unauhakika kwa na wewe matokeo yako sio ya uchakachuaji?

Lakini tuachane na uchakachuaji? Je utaweza kupambana na mafisadi kama akina Mwakyembe au ukinunuliwa na akina Rostam ndo utakuwa kwishnei? Nauliza hivyo kwani umesema we ni muhangaikaji, na hivyo ukipata rizki huwezi kuiacha ili kupunguza mahangaiko na makali ya maisha.

Ndugu yangu nakutakia maisha mema ndani ya bunge, ukawatetee watu wa Tabora na Watanzania kwa ujumla ingawa umechagua wrong chama lakini ukiwa msafi na mtetezi wa wanyonge na si wa maslahi yako binafsi basi utafanikiwa na kuheshimika sana mwana JF mwenzetu.

Tutafuatilia matendo yako sana kwani wana JF ni wana harakati, hivyo utuwakilishe vyema, usiende kinyume na matarajio yetu. Tutakufadhaika sana, usituangushe wana JF. We're watching you very closely. Kazi njema, ukapambane na ufisadi.😛eep:
 
Mbunge Kigwangalla anaamini kushinda kwa bahati? Hivi tutamaliza umaskini kwa fikra za kufanya mambo kwa kubahatisha? Anaona mzigo wa kuwatumikia watu masikini bahati?
lazima ujue background ya uchaguzi wa Kigwangalalanga kuelewa ana maana gani bahati.

Kigwangallalaa alishindwa preliminaries za CCM, alikuwa wa tatu. Wa kwanza alikuwa disqualified kwa sababu ni illegal alien, wa pili Selelii, a Richmonduli celebrity aliyekuwa adui ndani ya Chama. Ndio CCM kuwaengua wote wawili kumuokota figurehead wa tatu awe candidate. Na yeye mwenyewe ali survive criminal scandal la kufoji majina ya vyeti.

Ndo maana anasema ana bahati, mpe pongezi ya kuwa mkweli, hakustahili. Kwanza cheki anavyoanza remarks zake "Oyaaa..." hata gravitas ya Ubunge hana.
 
Hamisi mdogo wangu

nakupongeza sana kwa ushindi na umekua DR. pili kuwa mbunge mwaka huu pekee....

Ila bado nasikitika sana mlivyomchakachua bashe kifedhuli na kwakweli najisikia vibaya sana kuingia sehemu at the expense of another fellow in teh way you did... they say, what goes around comes around

Ila wanasema wanasiasa hawajaumbwa na haya na ndio maana hata bosi wako JK pamoja na kuiba kote wala hajisikii vibaya

"hongera" hamisi
 
Hongera sana kwa ushindi
kwa nini matokeo yalicheleweshwa???
 
hahahaaaa.... hamisi kamchakachua bashe na selelii, atashindwaje kuchakachua mengine?
 
OYAAAAAA, Bro... to some "gold standards" may mean something else

Ndio nchi yetu
 
Mh. Keep focused on the positive sides. Challenges are always there and will help to mold you better!
 
Hamisi yuko sahihi kabisa kusema kuwa hiyo ni "bahati" yake, na "spirit" yake ndiyo imemfikisha hapo. Isingekuwa rahisi kwake kuja hapa na kusema hiyo ni 'zawadi' ya Mama, kwa 'yale yote' anayofanya.

Nadhani anaelewa ni upande upi wa mkate wake una siagi, yasije yakamkuta ya......baba na mwana tunaimba na kucheza.

Ila Hamisi kumbuka tu kuwa ajidhaniaye amesimama.............nawasilisha.
 

Kwa majibu haya nimeishaingia wasiwasi maana majigambo 2 much! Naona Mkuu hapa umefika. Swali ni kama utawachukuwa unaowawakilisha kwenye hiyo neema.


Amandla.......
 

Daang son,

So that's what it's all about now ? Sasa tutategemea huyu stooge aliyekuwa planted top down, ambaye hata hakuambulia nafasi ya pili katika primaries za chama chake mwenyewe a represent interests za wananchi ?
 
Mr Kigwangala,
Kwanza nakupongeza kwa ushindi ulioupata (kama kwenye kura zilizokuwezesha kushinda hakuna kura za wizi, I'll never, ever, congratulate a thief)
Pili, kuhusu hizo shutuma kwamba umebebwa na watu kufika hapo ulipo, naamini hilo liko mikononi mwako kuuthibitishi umma unaokuzunguka kuwa hayo ni matokeo ya juhudi zako na siyo matokeo ya kubebwa na mtu yeyote. Ni juu yako kujipambanua kuwa wewe ni mpambanaji na siyo mbebwaji. Fanya kazi, watu wataona kazi yako na watajua kwa uhakika wewe ni nani. Watumikie wananchi walikuchagua; fanya kazi kwa bidii na ufanisi. Usibweteke kwa mafanikio uliyoyapata.
 
Hongera Dk. Naona kuna wa CCM theoretically wana ideas nzuri wameingia mjengoni. Mwenzako Kanuanry anasema atakopa fedhali kupata malori ya kusafirsha matunda kutoka jimbni kwake ambayo yatakuwa chini ya ushirika


  • Sijui wewe Vision yako hasa au ndoto yako ni kuona au kupugia debe mabadiliko gani jimboni kwako?
  • Assume JK anakuuliza analylsis yako kwa nini Parenetage ya kura za CCM zimepungua? Anakuuliza pia ni udhaifu gani kwenye utawala wake uli observe for past five years. utamjibu nini?
Nakutakia U Dk uheshimiwa wenye tija kwa taifa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…