Hii imechapishwa KULIKONI la leo...
RIPOTI MAALUM...
Jeetu Patel, Subash, Chavda
ni pembetatu ya majonzi
*Walitumia staili ya DECI kuifukarisha nchi
*Serikali ikatikisika na kuchapa noti mpya
*Shilingi ikashuka, bei za bidhaa zikapanda
*Watanzania sasa wahoji tuhuma, si rangi yao
MWANDISHI WETU
Dar es Salaam
MWAKA 1994, kiasi cha miaka 15 iliyopita, mfanyabiashara V.G Chavda na kundi la washirika wake Jeetu Patel na Subash Patel, ambao pembetatu yao ya majonzi KULIKONI linaifichua leo, waliweza 'kupanda' milioni 2.5 tu na 'kujivunia' mamilioni kutoka Serikali ya Tanzania, katika kisa cha ufisadi wa aina yake unaoweza kufananishwa na sakata la DECI lakini mkasa wenye majonzi na machozi kwa Watanzania.
[FONT=Times New Roman, serif]Watanzania wote wanakumbuka jinsi miaka ya 1990 uchumi wa Taifa ulivyoanguka-shilingi ikashuka thamani na bei za bidhaa zikawa juu lakini sasa imefichuka sababu mojawapo ya hali hiyo ni matendo ya wanamtandao wa pembetatu hii ya wafanyabiashara na sasa wafadhili wa wanasiasa wetu-Jeetu Patel, Subash Patel na V.G Chavda.[/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Sakata hilo na mkasa wenye majonzi kwa Tanzania linaweza kuelezwa vyema kuanzia miaka ya 1970 pale Chavda, raia wa India na mhitimu wa shahada ya pili kutoka Chuo Kikuu cha Massachusets, Marekani alipoingia nchini, kwa lengo adhimu-kujaribu bahati yake katika nchi hii ya amani.[/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Chavda ambaye baadaye aliachana na kazi yake ya utaalamu wa uhandisi na kuanza shughuli zake binafsi huku akiombewa kibali kwa nguvu za Ikulu kwa kuelezwa kuwa atakuwa akifanya kazi nzito nzito za Serikali na mashirika ya umma, baadaye alijisifu kuwa pamoja na kuingia nchini akiwa kama ombaomba, elimu yake na kusafiri sana kwake 'duniani' kulimpa uwezo wa kuyaona mambo ambayo wengi hawakuweza kuyaona.[/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Moja ya vipawa alivyojaliwa vya kuona mambo kikajifunua kupitia mpango wa Serikali wa Kuyabadilisha Madeni (Debt Conversion Program), DCP, ambapo Chavda akiwa mwasisi wa nadharia hiyo ya kiuchumi iliyopingwa na wachumi wengi wa Benki ya Dunia na IMF, aliishawishi Serikali ya Tanzania kuyauza madeni yake kwa wawekezaji wa ndani na nje ili wawekeze katika sekta ambazo zingezalisha na kuuza nje ili kuliongezea Taifa mapato ya fedha za kigeni.[/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Lakini ni ushauri huo kutoka kwa msomi huyo wa Massachusets, kama ilivyokuja kutokea katika sakata la EPA mwaka 2005 (ambapo nako ushauri wa mchumi mmoja mahiri ulizua balaa lote), nako mwaka 1993 Serikali ya Tanzania ilipojikuta ikiuzamisha zaidi uchumi wa nchi hii uliokuwa tayari katikati ya matatizo mambo yalianza kama hivyo.[/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Haikujulikana kama Chavda, Jeetu Patel na Subash Patel walifahamiana kabla ya kukutana Dar es Salaam au la, lakini kilicho dhahiri mpaka sasa na ambacho Kamati Ndogo ya Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi iliyochunguza sakata hilo mwaka 1994, ikiwa chini ya aliyekuwa mbunge wa Rorya, Edward Ayombe Ayila, watatu hao waliielekeza Serikali ya Tanzania katika mchezo wa DECI-kupanda na kuvuna, bila yenyewe kujijua.[/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Alianza Chavda kwa 'kupanda' mbegu zake katika kile Kamati hiyo ilichobaini kuwa ni kiasi kidogo cha milioni 2.5/- tu akinunua moja ya madeni hayo na kuasisi mzunguko mkubwa wa aina ya DECI ambapo baadaye jumla ya kampuni 82 (nyingi mpaka sasa wamiliki wake hawajafahamika) nazo 'zikapanda' kiasi cha bilioni 3 tu na kujivunia Serikalini zaidi ya bilioni 50/- ambazo Serikali ililazimika kuzilipa kwa kuchapisha noti mpya hali iliyougharimu uchumi wa Taifa![/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Akieleza kuwa fedha hizo angezitumia kuwekeza kwenye miradi ya kilimo kwenye mashamba ya mkonge kupitia kampuni zake za alizozisajili haraka haraka za Tanfarms Ltd, Makinyumbi Estates Ltd, Centrepoint Investments Ltd na Arusha Farms, Chavda kwanza alianza 'kupanda' kwa kuyanunua mashamba hayo kutoka Serikalini kwa jumla ya milioni 15/- tu (ambazo zililipwa kwa awamu saba) vikiwemo vyote vilivyokuwa ndani ya mashamba hayo zikiwemo mashine mbalimbali na majengo![/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Kisha baada ya kuyanunua kwa bei hiyo chee, Serikali ikamlipa Chavda fidia ya milioni 100/- kwa kupitisha tu baadhi ya nguzo za umeme na barabara katika kijisehemu tu cha mashamba hayo.[/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Baada ya kumiliki mashamba hayo ndipo 'upandaji' na 'uvunaji' ukaanza rasmi, akianza kwa kuchota 916,755,147.60/- mwaka 1990 kutoka Benki ya Ushirika na Maendeleo Vijijini wakati huo (CRDB) ikiwa ni mkopo kwa ajili ya kununulia mitambo tu ya kuwekeza katika mashamba hayo. Mkopo ambao hadi Chavda anatimuliwa nchini mwaka 1994 haukuwa umelipwa hata senti![/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Kutoka mkopo huo, Chavda akaingia katika DCP (fedha ambazo kwa sasa ndio zimewekwa katika akaunti ya EPA) ambako ikichukuliwa yeye ndiye aliyeasisi mkakati huo kupitia kwa mwanasheria wake Nimrodi Mkono, alinunua deni la milioni 2.5/- tu na kuingiziwa jumla ya milioni 661/- ambazo tofauti na masharti ya malipo hayo-kuwekeza kwenye kuboresha kilimo cha mkonge kwa kupanda mazao mapya na kuyahudumia hadi yatakapouzwa nje ya nchi na kulipatia Taifa fedha za kigeni, lakini badala yake Chavda akaingia katika pembetatu ya aina yake na washirika wake, Subash Patel na Jeetu Patel.[/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Badala ya kuwekeza katika mashamba ya mkonge Chavda akawalipa Subash na Jeetu malipo tata kwa madai kuwa walimpa huduma mbalimbali ambazo hata hivyo ushahidi wao haujapatikana mpaka sasa.[/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Kwa mfano Subash ambaye naye baadaye 'akapanda' moja kwa moja kwenye mpango huo na kuvuna jumla ya bilioni 6. 98/- (kupitia kampuni zake za Deco Arts, Hotel Sea Cliff, M.M Motors na M.M Garage) ambazo haijajulikana alizifanyia nini, bado alinufaika kutoka fedha alizolipwa 'kaka' yake (Chavda) kwa kuingiziwa malipo tata ya jumla ya 515,995,375/- kati ya milioni 661/- alizolipwa Chavda.[/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Naye Jeetu Patel kupitia kampuni zake za Azania, Agricultural Enterprises, Liberty Leather Shoe Ltd, Azania Eximco na kadhalika, alithibitisha kupokea 82,295,000/- vyote vikithibitika kuwa ni uongo kwa mujibu wa wachunguzi wa Serikali.[/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Malipo hayo ingawa Chavda alidai kuwa ni ya vifaa na utaalamu ambao Subash na Jeetu walizipa kampuni zake za mkonge, wote watatu walishindwa kuonesha ushahidi mbele ya kamati hiyo ya Bunge walipotakiwa kuthibitisha kwa nyaraka huduma au biashara waliyoifanya na badala yake wakaikacha Kamati hiyo kwa visingizio vya kisheria katika barua zao mbili ambazo mfululizo wa maelezo ya kutotaka kuhojiwa ulikuwa ukifanana kama vile umeandikwa kutoka ofisi moja na mtu mmoja.[/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Subash Patel na Jeetu Patel wamejipatia jumla ya 661,274,660/-. Fedha hizi wamezipata bure bila kutoa huduma yoyote. Wala hawakuzilipia fedha hizo kodi ya mapato. V.G Chavda ameifanya Tanzania kama ni shamba lake la kuchuma. Watanzania ni vibarua wake. Ama kweli wajinga ndio waliwao..., imehitimisha sehemu ya ripoti hiyo ya Apiyo ikimnukuu aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani wakati huo Augustine Lyatonga Mremba ambaye naye alilivalia njuga sakata hilo na kufanya uchunguzi wake uliobaini makubwa.[/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]KULIKONI limebaini kuwa kupitia mpango huo wa Chavda uliozinufaisha kampuni 82 nyingi zikiwa wamiliki wake hawajulikani, Serikali ilitikisika mno hali iliyosababisha athari kubwa katika uchumi wa Taifa ambao ulielezwa hivi kwa maneno ya Kamati yenyewe:[/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Kwa kipindi hicho cha miaka miwili na nusu ambacho programu hiyo iliendeshwa jumla ya kampuni 82 zilipata vibali vya kununua madeni yenye thamani ya jumla ya bilioni 3.038/- nazo zikalipwa na serikali Bilioni 50.877/- sawa na asilimia 18.02% ya bajeti ya matumizi ya kawaida.[/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Hii ina maana kuwa Serikali ililazimika kuchapisha fedha kiasi cha Tshs. Bilioni 48 kufidia pengo! Inakadiriwa kuwa hadi Serikali ilipoamua kusimamisha programu ya DCP, Juni 30, 1993, madeni hayo yalishaliathiri Taifa kwa kuongeza mfumuko wa bei kwa asilimia 15 huku madeni hayo yakiwafaidisha wafanyabiashara wachache. [/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Kwa ufisadi wa aina hii KULIKONI linahoji Watanzania wanapodai utajiri wa Taifa lao uliopokwa kwa mbinu ambazo zinajirudia kila baada ya muda, watalaumiwa kwa ubaguzi wa rangi?[/FONT]