duuuuh!! kweli hizi ndoa/mahusiano ya siku hizi ni vichekesho!!, unasema unaogopa kumwambia na unamkumbuka ex-bf wako?........,, Inakuwaje mtu ambaye unayempenda kweli ushindwe kumueleza ili ajaribu kufanya vile ambavyo utaridhika ili hata mapenzi yenu baadae yawe matamu?. Kama kumwambia ss hv unaogopa kumdis-appoint, unahisi baada ya kukuoa au mbele ya safari yenu ukimwambia ndo utamfurahisha?. Wewe ni mwanamke mwenye bahati sana kuwa na jamaa ambaye tatizo lake ni rahisi kuelekezana na kushauriana kulimaliza, tatizo wewe mwenyewe pia hujishughulishi kumsaidia mwenzako ambaye inawezekana hajui kuwa huridhiki kutokana na wewe kutomuelekeza nini akufanyie. Kitu kingine nachoona hapa kama vile unawa-alert watu kuwa unataka kuolewa ila baada ya kuolewa unataka kidume kingine pia cha pembeni sababu inaonyesha huwa huridhiki na mwanaume mmoja. Ushauri wangu ni kwamba kaa chini uongee na jamaa wako katika hali ya utulivu ili akuelewe au uwe unamuelekeza unapenda ufanyiwe kitu gani muwapo kwenye mambo yenu, vinginevyo mnapoteza muda tu ni heri kila mmoja achukue 50 zake.