Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Leo hii serikali ya Congo DRC imetangaza kuvunja mahusiano na Rwanda huku wanajeshi wapatao 13 wa kutoka vikosi vya kulinda amani na wanajeshi wengine wa kigeni kuuawa.
Wizara ya mambo ya nje ya Congo DRC imetangaza leo kuwa inawaondoa watumishi wote walioko katika ofisi ya ubalozi wa Congo DRC mjini Kinshasa. Serikali ya Rwanda bado kujibu hata hii inoashiria mambo kutokuwa mazuri baina ya nchi hizi majirani.
Ofisi hiyo itafungwa ndani ya masaa 48 yajayo na wafanyakazi wote wameamriwa kurudi Kinshasa.
Leo hii pia baraza La Usalama la Umoja wa Mataifa litaketi kuzungumzia hali inoendelea nchini Congo DRC kufuatia ombi la serikali ya Congo DRC.
Hadi sasa vikosi vya waasi wa M23 vikiwa ni sehemu ya vikosi vya waasi vipatavyo 100 vimeshachukua kilomita zipatazo 27 za mji wa Sake. Jana serikali ya Congo ilisema vikosi vya nchi za SADC vya SAMIDRC viliweza kuwarudisha nyuma waasi hao lakini tayari wanajeshi wawili wa Afrika Kusini, mmoja wa Uruguay na wengine wa kigeni wameishauawa.
Akizungumza na AP kwa masharti ya kutotajwa jina afisa mmoja wa UN amesema kuwa pia kuna wanajeshi wengine watatu walouawa kutoka Malawi na Afrika Kusini pekee hadi sasa imepiteza wanajeshi 7.
Majeshi ya kulinda amani ya MONUSCO yapo nchini Congo DRC tangia mwaka 2005 na iadadi yao ilikuwa ni askari 14,000. Tangu mwaka 2021 majeshi ya Congo DRC na yale ya nchi SADC yamekuwa yakikabiliana na vikosi vya M23 kuvizuia kuchukua mji wa Goma.
Mji huo wa kistratejia una madini lukuki waasi hao wa M23 ambao ni wa kabila la Watutsi wamekuwa wakidai kuwa Goma ni jimbo lao. Rwanda pia imekuwa ikituhumiwa kuvisaidia vikosi hivyo kwa silaha, mitambo ya makombora na vingine.
Madini yaliyoko katika maeneo ya mji huo ni pamoja na Dhahabu, Almasi, cassiterite, coltan, tourmaline, pyrochlore, na Wolfram.
Rwanda imekana kuvisaidia vikosi hivyo lakini imekiri kuwepo kwa vikosi vya majeshi ya Rwanda upande wa mashariki ambako ndiko kunopakana na mji wa Goma na pia kuwepo kwa mitambo ya makombora huku ikidai kuwa mitambo hiyo ipo kuimarisha ulinzi na pia kuangalia vikosi vya Congo DRC ili kuvizuia kuingia Rwanda.
Pia habari za kijasusi ambazo bado hazijathibitishwa zadai kuwa vikosi vya majeshi ya Rwanda vimeingia mpakani na Congo DRC kusaidia vikosi vya waasi kuchukua mazima mji wa Goma ambao ni makao makuu ya jimbo la Kivu ya kaskazini.
Kwa kifupi ni kuwa tayari vita kamili ikaingia hatua ingine nchini Rwanda khasa kufuatia kitendo kilofanywa na majeshi ya Rwanda hadi kufikia asubuhi ya leo.
Baadhi ya vyanzo vya habari hii:
Actualite
AP