Congratulations To Simba Sports Club..

Hongereni sana watani zetu hatimae imekuwa, tangu 2012; Mmepigana kiume mmefurukuta, hakika atafutae hachoki, akichoka ujue kapata, mmekumbushia 2012!!! najua mtabweteka na sifa hizi, Yanga ya mwaka huu sio ile, Tff sio ile, Uongozi wa Nchi sio ule; Hakika ni wakati wa Kipofu kuona mwezi hata kabla haujachomoza..Ni furaha iliyoje!! This is Simba!!!! Mnyama wa mwitoni...hakika mmejifunza kuwa ukiona unaekimbia nae anachechemea wewe ongeza mwendo, usimngoje apone, itakuwa sawa na kumwamusha aliyelala..usije ukalala wewe...safari yenu ilikuwa ngumu pamoja na kutofungwa kwenu lakini kuna wakati Yanga ikawa inawatishia uhakika wenu...mlikaza buti mkamfukuza kocha OMOG, na Mayanja, Hio ikawa uamuzi mzuri sana...Ashukuriwe Mshika timu MO, maana kama ilivyokuwa kwa MANJI amesimama kidedea kuhakikisha PESA haikosekani ikatibua Uhakika wenu; ILA hawa matajili na serikali hii...haya, hayawi hayawi yatakuwa..shikeni hilo pia!! Asante serikali ya Mkoa kwa kuwezesha upande wa Yanga kulegalega..yote mipango ya Mungu!!! Hakika Mungu ni wa wote maana wakati Timu TAJIRI IKIFANIKIWA KUJITWALIA UBINGWA WA VPL, kimataifa ilichemka sababu ya ugeni wa kupanda ndege kwa muda mrefu (poleni sana) ILIHALI TIMU DHAIFU NA MASKINI ikiendelea kujikongoja mdogo mdogo japo kibahati bahati ( Mungu si wa wote? usishangae ikafanya maajabu) na pia PESA ni jawabu la mambo magumu kuwa marahisi...Ila nawakumbusha Maskini akipata..........kuweni makini...maana ajidhanie amesimama aangalie asianguke! Pia kumbukeni Yanga ya mwaka huu sio ile ya miaka iliyopita hadi ikajimilikisha Kombe! wala sio Yanga ya msimu ujao..maana maumivu ya kukosa ubingwa au hata kuwa katika tafrani za kiuchumi haiwezi kuwafanya walale kama ambavyo Bingwa wa mwaka huu ambavyo hakulala miaka yote hii ambapo mdogo wangu alianza form 1 na sasa anaingia Form 6 ndo anasikia kila kona shangwe Simba kabeba ndoo kilaini na kejeli nyingiii juu ya mpinzani dhaifu uwanjani na nje ya uwanja!!!...najua zipo juhudi zitafanyika..hivyo fungeni kibwebwe haswaaa!!

HONGERENI WATANI ZETU SIMBA; VPL YENU HIYO, MSITIZAME NYUMA HAKUNA ANAYEKUJA MSIJE JIKWAA BURE! HONGERA MANARA KWA HAMASA, MAANA HUKUJUA KUSHAKE ILA KWA KUONA MWEZI UKASHAKE MAANA TANGU AJIRA YAKO IMEEANZA HUJAWAHI PATA HII KITU; SEMA WATU HAWAJUI..HONGERA SANA, KIDOGO TU UONDOKE CLUBUNI BILA KUPATA HII KITU..FURAHA UNAYOJISIKIA MANARA NA WAPENZI WOTE WA SIMBA...YANGA TUMEISIKIA MPAKA TUKAKARIRI...MANARA HONGERA RUKSA KWENDA DUBAI SASA!
 
Simbaaaaaaaa[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji122] [emoji122] [emoji122]
 
Sound Good..
 
SUGU katoka na Wengi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…