Copa America 2019 - Brazil

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
23,620
Reaction score
52,790
Michuano ya Bara la America ya Kusini maarufu kama "Copa America" inaanza Juni 14 mpaka Julai 7 mwaka huu nchini Brazil.

Michuano hiyo itashirikisha jumla ya timu 12 ambazo zitakuwa katika makundi matatu. Kati ya timu 12, timu 10 ni mwenyeji wa bara hilo huku timu zikialikwa kushiriki ambazo ni Japan na Qatar kutoka barani Asia.

Hii ni michuano inayoshuhudia mpira wa hali ya juu ukitandazwa huku mastaa mbalimbali wakiziwakilisha timu zao vyema. Hii ndio michuano ambayo kuna kuwa na wingi wa mawakala toka barani ulaya kuja kuangalia vipaji vipya toka bara linalosifiwa kwa kuzalisha vipaji vingi vya soka katika historia ya mchezo huu.

Bingwa wa kihistoria wa michuano hii ni Uruguay ambapo ana mataji 15, Argentina mataji 14 na Brazil mataji 8.

Karibu tujuzane yanayotokea katika michuano ya mwaka huu.

Mashindano.haya yanarushwa na Startimes.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…