Copied somewhere.

Robot la Matope

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2015
Posts
8,174
Reaction score
16,794
Mwenye kutaka rafiki asiye kuwa na Dosari, basi ataishi mpweke daima.

Mwenye kutaka Mke au Mume ambaye hana mapungufu, ataishi bila ya kuoa au kuolewa (Bachelor) mpaka siku ya kufa kwake.

Mwenye kutaka ndugu asiye kuwa na matatizo, ataishi akimtafuta milele.

Mwenye kutaka mtu wa karibu aliyekamilika, daima ataishi akiukataa udugu.

Tuvumilie matatizo ya wenzetu pamoja na changamoto zao, ili turejeshe hali ya maelewano kati yetu.

Unapotaka kuishi kwa furaha maishani, basi usitafsiri kila kitu unachokiona au kukisikia.

Wala usichunguze sana kila kitu kilichopo mbele yako.

Wala usichambue kila kitu unachokiona au kukisoma.

Hakika ya wale walioichambua Almasi sana, mwisho wa siku waliikuta ni Mkaa.

Usiwahukumu watu kutokana na mandhari (muonekano wa nje), vyo vyote vile walivyo.

Fahamu ya kuwa pamoja na yote hayo, bado ni wanadamu kama wewe (uhalisia wao).

Tuvumiliane hakuna mkamilifu isipokuwa Mwenyezi Mungu pekee !!!
 
tunayasoma tunayaelewa yanatuingia na tunayaacha hapa hapa halafu tunaendelea na maisha yetu yale yale
 
Maneno Ibrahim ajibu ayo kwenye page yake ya instagram
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Thread yangu ya kufunga mwaka 2018....




#LastThreadToCommentIn2018
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…