#COVID19 Corona: 99% ya vifo Marekani hawakuwa Wamechanjwa

#COVID19 Corona: 99% ya vifo Marekani hawakuwa Wamechanjwa

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Mengi yameelezwa kuhusu chanjo za Corona.

Kwa mujibu wa balozi wa Marekani, katika vifo vyote vitokanavyo na Corona sasa hivi huko kwao, 99% ni watu ambao hawakuwa wamechanjwa.

Angalizo:

1. Ni muhimu ikafahamika kuwa chanjo hizi si dawa ya kutibu au kuzuia mtu kutopata ugonjwa.

2. Chanjo hizi huuandaa mwili kupambana ikiwa ugonjwa utakuja.

3. Madhara ya ugonjwa ukimpata aliyechanjwa yanakuwa ni madogo zaidi.

Habari ndiyo hiyo.
 
Wamechanjwa Sasa, je korona imeondoka?
Kuna variant mpya kutoka Peru na amesha spread nchi 30, huyo hadhuriki na hako ka chanjo, hata Kama umechanjwa chanjo zote anakuparura tu.
 
Na pia 97% ya wanaolazwa mahospitalini ni wale ambao hawajapata chanjo,
 
Wamechanjwa Sasa, je korona imeondoka?
Kuna variant mpya kutoka Peru na amesha spread nchi 30, huyo hadhuriki na hako ka chanjo, hata Kama umechanjwa chanjo zote anakuparura tu.

Hapo ndipo utakuwa bila shaka unauona umuhimu wa kuwapata watu wengi kadri iwezekanavyo kuchanjwa ili ugonjwa kuweza kutokomezwa.

Pana threshold ya watu duniani na katika kila nchi ambao wakishachanjwa ugonjwa utadhibitika na hatimaye kuto kutoweka kabisa.

Hii ni kama ilivyotokea kwa ndui au tunakoelekea kwenye polio.

Ndiyo maana mataifa lazima yasaidiwe kuchanja watu wao. Kwa kubembelezwa au hata kwa lazima ikibidi.

Ujinga na upumbavu wa watu wowote hauwezi kuachwa kuiweka dunia hatarini.

Au wewe huoni hivyo?
 
UKikosa hoja, unanyamaza. Huwezi kulazimisha watu kwa kitu ambacho hakina maslahi kwa yeyote. Kama ingelikuw ahivyo basi dunia ingelikuwa ni animal firm.

Shirkisha solutions, siyo ubabe.

Dawa nyingine ya kutibu corona hii hapa.

Shauri serikali iwasiliane na ubalzo wa Israel iagize hizi dawa kama hatunazo hapa.

Malumbano ya kulinda misimamo bila facts hayajengi.
 
Pata maji unywe utulie utafakari.

1. Kuna kiwango cha watu katika jamii wakichanjwa wote maambukizi yatapungua kwa maana kila wanaoambukizwa madhara yatakuwa yanakuwa kidogo.

2. Kama maambukizi yatakuwa yanapungua uwezekano wa variant zingine utakuwa unakwenda kumalizika.

3. #1 na #2 hapo juu ni pure science kama anavyosema balozi wa Marekani. Haya ni mambo yanayojulikana.

4. Kwa salama ya dunia kama ilivyo kwa silaha za maangamizi dunia iliyostaarabika haiwezi kukubali kuwekwa hatarini kwa sababu ya ujinga au upumbavu tokea kokote.

5. Utabembelezwa, utaletewa dawa bure bado hutaki, bado threshold inavyotakiwa nchini haifikiwi? Tuombeane uzima. Kwani chanjo za polio ni hiari?
 
Back
Top Bottom