Corona bado ni tishio, tusiache kunawa mikono

Corona bado ni tishio, tusiache kunawa mikono

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Joined
Aug 7, 2018
Posts
685
Reaction score
1,124
Hadi hivi sasa maambukizi ya Virusi vya Corona yaneendelea kuitesa dunia na Tanzania inaonekana kujitahidi kudhibiti ongezeko la idadi ya wagonjwa.

Wakati haya yakiendelea, bado kuna haja ya kukumbushana kunawa mikono mara kwa mara na kuepuka kushika macho, pua na mdomo kwa mikono isiyo safi.

Njia kuu ya kudhibiti maambukizi ya Virusi vya #Corona ni kunawa mikono kila mara ili kuondoa virusi hivyo endapo umegusa mahala penye maambukizi au kama umeambukizwa kuepuka kuwaambukiza wengine


Hakuna idadi ya kikomo ya kunawa mikono kwa siku. Nawa kila unapoingia sehemu, kila baada ya kukohoa au kupiga chafya, kila baada ya kushika sehemu hatarishi kama vitasa, swichi za taa na milango ya gari

Endapo hakuna maji na sabuni karibu, vitakasa mikono vyenye kilevi kwa asilimia 60 au zaidi vinaweza kutumika. Kumbuka kuua vijidudu kwenye vifaa vitumikavyo kila mara kama simu, waleti, rimoti na meza
 
Upvote 0
Kwa hiyo Italy, Spain, USA, China e.t.c hawakuwa wananawa mikono?!
 
pia kujitahidi kutibu magonjwa nyemelezi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom