Awali ya yote ninamshukuru Mungu aliyetuweka hai mpaka sasa mimi na wewe tupo pamoja katika ukurasa wetu wa jamii.
Mwanajamii, karibu tuangalie kwa pamoja kwa jinsi gani tunaweza kuchukua hatua dhidi ya haya maambukizi ya virusi vya corona.
Kwanza,
Bila kupoteza mda nianze kwa kuangalia hatua ambazo tukizizingatia kwa pamoja kama wanajamii na katika ngazi ya familia zetu zitasaidia kwa kiasi kikubwa kujilinda dhidi ya haya maambukizi ya virusi vya Corona.
Swali 1:
Je, ni hatua zipi za kuchukua kujilinda dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona?
Jibu;
una hatua mbalimbali za kuchukua kujilinda dhidi ya maambukizi ya virusi ya Corona, miongoni mwa njia hizo ni:
A. Kuvaa barakoa kwa ufasaha;
~Tokea kipindi ulipolipuka ugonjwa wa Corona kumekuwa na kampeni juu ya uvaaji wa barakoa. Lakini hapa tuangalie ni namna gani hii barakoa ivaliwe kwa usahihi ili kuepukanana na maambukizi:
Tuanze hivi:
1. Nawa mikono yako kwa maji safi tiririka na sabuni kabla ya kuvaa barakoa.
2. Ishike barakoa yako, hakikisha pindo (linda) za barakoa zimeelekea chini na chuma laini kama mpira (rubber) imeelekea juu
3. Vaa barakoa kuanzia juu ya pua kushuka mdomoni mpaka chini ya kidevu. Chuma laini kikae juu ya pua
4. Hakikisha barakoa imefunika pua, mdomo na sehemu ya kidevu. Pia, uwe na uwezo wa kupumua vizuri.
5. Ifunge barakoa yako kama ni ya kamba, na kama ni ya mipira ya kuvalisha masikioni vaa. Hakikisha imekaa imara.
6. Epuka kushika sehemu ya nje ya barakoa pindi ukiwa umeivaa.
7. Ukitaka kukohoa au kupiga chafya usivue barakoa.
8. Wakati wa kuvua barakoa yako, shika sehemu ya ndani ya barakoa, au kamba za barakoa. Epuka kushika sehemu ya nje wakati wa kuivua. Taratibu ivue barakoa yako.
9. Weka barakoa yako sehemu sahihi.
10. Kisha, nawa mikono yako kwa maji safi tiririka na sabuni
B: kunawa mikono kwa maji safi tiririka na sabuni:
~Nawa mikono yako kila baada ya mda kadhaa, baada ya kushika vifaa mbalimbali vinavyoweza kuwa vimebeba virusi, mara baada ya kushikana mikono n.k
C: kuepukana na misongamano isiyo ya lazima.
~Kama unauwezo wa kupata mahitaji yako pasipo kuingia katika msongamano wa watu, ni vyema kutoingia sehemu za msongamano
Nini cha kufanya unapojihisi kuwa na dalili za maambukizi?
1. Endelea kuchukua tahadhari za kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona kama kuvaa barakoa, kunawa mikono, n.k
2. Kama unafamilia wajulishe
3. Fika kituo chochote cha afya kilichopo karibu nawewe kwa huduma zaidi.
Mwisho, ni vyema kuchukua tahadhari ili kuepukana na maambukizi haya ya virusi vya Corona. Na kwa maelekezo zaidi tuendelee kufuata taratibu za afya kama zinazotolewa na wizara ya afya kupitia vyombo vya habari, watumishi wa kada ya afya, n.k
Asanteni wanajamii kwa umoja wenu.. Najivunia kuwa pamoja nanyi

Upvote
2