Corona hakuna nchini, lakini majirani zetu wanayo

Hili swali ni zuri sana ingawa huwezi kupewa majibu toshelezi zaidi ya kuambiwa Mungu anatulinda.

Hata hivyo hali si hali ya joto ni kubwa sana kwa mkoa wa Dar lakini watu wana mafua yasiyoisha pamoja na kukohoa sana na kuumwa, mawodini watu wapo hoi.
 
Siku ikimgonga mtu mzito mzito kidogo ndio tutaelewa kua corona ipo au laah.
 
Hata wale BAWACHA 19 ni COVID-19 tupo nao humu humu kwenye mipaka yetu na ni hatari kwa mustakabali wa taifa.
 
Mtu mmoja nimeona aikitoa hotuba na akikana uwepo wa covid huku 'akipenyezewa' kimiminika ambacho ukikitizama vyema utagundua sio maji ya kawaida.
 
Mkuu, juzi hapa Malawi imetoa amri ya kufunga shule, mwezi mmoja au mwili iliyo pita Malawi ilipoteza mawaziri wawili kwa mpigo, walipishana kwa siku tu!

Wiki iliyopita niliona BBC documetary ikizungumzia kwamba Kenya imegundurika ina a new strain ya corona ambayo haipo popote Duniani hisipo kuwa Kenya tu na kibaya zaidi wanasema ugonjwa huo umegundurika huko TAVETA yaani mpakani mwa Kenya na Tanzania, nikawa najiuliza maswali mengi hivi hawa Wakenya wanazungumzia ugunduzi wa new strain ya corona mpakani mwa Tanzania na Kenya wana lengo gani? Kwa nini taasisi ya utafiti ya chanjo kutoka Uingereza (Oxford University) ikishirikiana na taasisi ya utafiti ya Kenya (KEMRON) wanakuja na horror stories kutoka mpakani mwa nchi zetu mbili.

Binafsi nashauri ingekuwa vizuri kama Serikali yetu inge hoji kwa kina taasisi hizo mbili zinazo jihusisha na tafiti pamoja na majaribio ya chanjo ya Oxford ili ijulikane statements zao zilikuwa zina maanisha nini au zina ajenda ya siri.

Tukija hapa kwetu so far so good i.e hali ya hivi sasa aona ni shwari kabisa, cha muhimu ni kila mmoja wetu achukue tahadhali - wataalamu wetu wa Wizara ya afya labda wanachukuwa approach ya kisayansi inayo julikana kama "herd immunity theory" kama wenzetu wa Sweden - mbinu hiyo imefanya maambukizi ya corona yapunguwe sana sana huko Sweden unlike Continental Europe na USA wanao lazimisha lockdown - my opinion.
 

Mijaa ya CCM haiwezi kukuelewa.

Heri ukampigia mbuzi gitaa mkuu lakini siyo hii mijima ya kinondoni.
 
Ushauri mzuri na wa kiungwana
 
Hii sirikali yetu inajifanyaga Mungu anakaa Tanzania, inaupendeleo maalum duniani!
 
Za kuambiwa changanya na za kwako...

Siku zote nchi sio wananchi, kama nchi haina covid-19, wananchi je?
 
Brother nitakupinga hapo sweden. Herd immunity haijawasaidia chochote. Walikuwa na maambukizi 535000 na vifo 10,323.
Katika miezi yote hiyo december kuelekea mwaka mpya maambukizi yali spike juu kuliko kiwaida.

Herd immunity ni theory ambayo kuwa successful si 100%. Practical ni kubahatisha tu na ni risk. Maana congo walishajarib wakati wa outbreak ya ebola.

Ika backfire vibaya mno.

Brazil nao walianza na hii kitu mwanzoni. Ika backfire kwao pia. Sasa hiv wamerudi nyuma. Waki practices tracing. But its too late.
 
Covid ipo. Japokuwa serekal haiwezi ku declare public.
Ni bora watu wakachukua hatua za kujikinga wenyewe. Si mpaka waambiwe.
 
Mkuu nchi ipo salama, hofu kwako tu Corona tunaiona kwa wenzetu
Ila kwetu ni hadithi fikirishi
Nawashilisha
 
Mungu anaonesha "UWEPO WAKE"
ukimuomba kwa dhati atakujibu.
Hii nayo inatakiwa iwekwe kwenye maajabu yale ya dunia.
Tuzidi kumuomba MUNGU.
 
Unataka uambiwe ili uchukue hatua zipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…