Korona haiteui, tajiri na maskini
Dunia haichagui, iuwe iache nani
Waafrika hijui, wachina wamarekani
Korona ina hasara, na zake faida pia
Ingawa inagutusha, kwa kuuwa wengi watu
Katika haya maisha, inazo faida kwetu
Mwanzo imetufundisha, kunawa mikono yetu
Korona ina hasara, na zake faida pia
Mitaroni na vilabu , walevi wametitia
Wamepunguza sharabu, hatuwaoni kwa ndia
Wote wamejiratibu,kwa nyumba kajifungia
Korona ina hasara, na zake faida pia.
Ubovu umesimama , vita sijavisikia
Kumekuwa na heshima,silaha zimetulia
Tumeanza kuisoma,Korani na Bibilia
Korona ina hasara, na faida zake pia.
Ile mipango ya kando, kitambo ulosikia
Biashara za magendo, usiku ukiingia
Vyote vimewekwa kando, na watu kujirudia
Korona ina hasara, na faida zake pia
Sent using
Jamii Forums mobile app