Luqman Van Maliki
Member
- Aug 19, 2021
- 6
- 7
Kuanzia mwaka 2019 kila nchi karibu dunia nzima imekumbwa na hali mbaya ya kutembelewa na ugonjwa wa hatari wa CORONA ambao umeendelea kusambaa kwa kasi kubwa huku ukiendelea kunyofoa roho za watu mithili ya uzi mwembamba katika moto.
Tangu kuibuka kwa virusi hivyo ambavyo vilianzia pale katika jimbo la WHUHAN nchini China ambavyo hadi sasa watu zaidi ya million 100 wameambukizwa na huku takribani watu milion tano wamekwisha achana na dunia, hali ya biashara imeendelea kuzorota na kudorora karibu sekta zote japo kwa sasa mambo yameanza kurudi kama awali kwa kiasi kidogo.
Maeneo mengi duniani kwa miezi kadhaa nyuma kila kitu kilibadilishwa utaratibu wake hasa sekta ya biashara na uchumi ambavyo nchi nyingi ndio mhimili wake mkuu wa kipato kwa wananchi wake.
Kuthibitisha CORONA ilivyoathiri na inavyoendelea kuathiri uchumi wa dunia, taasisi ya utafiti ya Brookings ya nchini Marekani Novemba mwaka jana iliwahi kuchapisha taarifa jinsi biashara ya mafuta ilivyokuwa na hali mbaya kupita katika wakati mgumu tangu kuibuka kwa virusi hivyo hatari ulimwenguni.
Kufikia tu mwezi mei mwaka jana jukwaa la maendeleo la umoja wa mataifa UNCTAD lilichapisha taarifa kuwa ugonjwa wa COVID-19 umesababisha anguko la uchumi duniani kote kwa zaidi ya Dola trioni moja, zaidi ya shilingi za kitanzania shilingi Trioni elfu mbili na miatatu (2,300) kwa kuanzia januari mosi mwaka jana hadi kufikia mwezi mei.
Sasa unaweza kupata picha ya kawaida tu kuanzia mwezi mei mwaka jana hadi sasa CORONA imesababisha anguko la kiuchumi kwa ukubwa upi.
Napata maswali mengi yasiyokuwa na majibu ni kwa kiasi gani CORONA itaendelea kukaa duniani ikiendelea kuua na kuhatarisha hali za kiuchumi za mataifa mbalimbali duniani?
Rais wa awamu ya tano wa Tanzania hayati John Pombe Magufuli alijitahidi sana kuhakikisha wananchi wake enzi za uhai wake wanaendelea kufanya kazi hata nyakati ambazo dunia ilikuwa inatishwa zaidi na ugonjwa huo.
Magufuli ni Rais wa namna sana mafunzo yake haya yanakwenda duniani hata leo kwani mataifa yote yameiga kile ambacho hayati magufuli alikifanya alipokuwa madarakani. Nchi zote wakati wakati ule zilifungia raia wake ndani lakini kwa Magufuli hali ilikuwa ni tofauti wananchi wake waliendelea kuchapa kazi na kuondoa hofu ya Corona.
Kwa sasa nchi zote duniani zimewaweka huru raia wake wakiendelea kujitafutia kwa ajili ya maisha yao japo hofu dhidi ya ugonjwa wa Corona bado ipo duniani na watu wanaambukizwa na wengine kufariki.
Mapema mwaka jana shirika la UNCTAD la umoja wa mataifa katika ya moja ya maelezo yao waliyokuwa wakiyafafanua kuhusu janga la Corona lilivyoathiri uchumi wa dunia, walisema kadri jinsi tahadhari kubwa zilivyokuwa zinaendelea kuchukuliwa na mataifa katika kujikinga na janga hilo kati ya nchi na nchi na kufunga mipaka na ujirani wote wa kibiashara ili kujikinga na maambukizi mapya siku zile kungeisababishia dunia anguko zaidi la kiuchumi la dola trilioni tatu ambazo ni sawa na shilingi trioni elfu tano miasaba (5,700) za kitanzania.
Moja ya nukuu zake bora mwana falsafa mahiri wa Uingereza Marehemu Mignon Mclauglin aliwahi kueleza kuhusiana na nadharia ya mwisho wa dunia kuwa "Dunia itakuwa ukingoni pale tu uchumi wa dunia utakapofikia Asilimia 0.5".
Hadi sasa ukiachana na athari kubwa ya biashara ya mafuta kwa ujumla iliyopatikana, biashara za uingizaji na usafirishaji zilishuka kwa kiasi kikubwa, mwaka 2020 na mwanzoni mwa mwaka huu. Wasanii wanaofanya muziki wa jukwaani nao biashara yao ilishuka ingawa baadhi ya nchi walikuwa wanafanya kwa kias kidogo.
Hata hapa nchini vilio vilikuwa vingi kila kona, wakati ule biashara ya usafirishaji ilipodorola duniani wafanyabiashara wengi waliokuwa wanategemea bidhaa kutoka china waliumia.
kampuni nyingi za usafirishaji wa mizigo kati ya nchi na nchi zilikwama sababu ya janga la virusi vya Corona, maeneo mengi biashara zilisimma na uchumi ulisimama na kushuka kwa kasi kubwa.
Uchumi wa michezo nako hali ilikuwa tete na mbaya sana timu hazina pesa mashabiki walizuiwa kuingia uwanjani japo kwa msimu huu wameanza kuruhusiwa ndani ya msimu huu.
Nchi za ulaya kuna muda ilielezwa maduka yalibaki tupu, bidhaa zilikwisha watu walinunua kwa wingina kuhifadhi ndani kusudi wasitoke nje kukwepa COVID-19. Bahati mbaya zaidi bidhaa hasa za chakula ziligeuka adimu hofu ya watu kukosa chakula ni kubwa.
Dunia inaendelea kuteseka dhidi virusi vya Corona ,dunia uchumi ulikuwa unashuka kwa kasi ya asilimia 0.5.Endapo uchumi ukishuka na kifikia hapo ni kutimia tu kwa nadharia ya mwisho wa dunia.
Tuombe maambukizi yasiendelee kwa kasi huku wananchi wakiendelea kuchukua tahdhari dhidi ya ugonjwa wa Corona na kuchanja chanjo kama ambavyo nchi nyingi zinaagiza raia wake kama ilivyo nchini kwetu Tanzania.
Watanzania chini ya Rais Magufuli walisisitizwa sana kuendelea kufanya kazi wasitishwe na mambo yoyote hata janga la Corona ili kutafuta na kuweka akiba ya Maisha yao na Watoto wao.
Mwandishi nguli wa vitabu nchini na watu wengi wanamnadi kama baba wa fasihi nchini marehemu Shaaban Robert aliwahi kuandika kwenye kitabu chake cha wasifu wa Siti binti Saadi kuwa ustawi ulidharau watu walioshindwa kufanya kazi kwa bidiii siku zote na kama kwamba ungeweza kuhesabu orodha ya watu waliofanikiwa bila kufanya kazi na juhudi kubwa usingalimaliza orodha ya vidole vyako vya mkono mmoja.
Funzo ambalo kama watanzania tunalipata kutoka kwa hayati Magufuli ni kufanya kazi kwa bidi na Shaaban Robert pia aliiambia dunia kupitia kalamu yake watu wafanye kazi kwa bidi kwa ajili ya Maisha yao ya sasa na Watoto wao pindi wao watakapoondoka katika dunia hii.

Upvote
1