Tetesi: Corona inapukutisha watu Dar. Kuna wanaolalamika ndugu zao kuzikwa kinguvu na Mamlaka Dar huko Bahari Beach, Buza na Mbweni

Siku yakiwakuta na wao ndio akili zitawarudi. Si unajuwa corona haichagui, ni muda ndio utaongea.
 
Wewe ni mzushi na muongo mkubwa lete uthibitisho hapa na sio kuja kuwapa watu hofu.
 
Mpaka sasa hujachukua tahadhari?,ugonjwa hauna tiba wala kinga,ndio maana mmeambiwa mtumie pia njia za kienyeji kupunguza makali,mfano tangawizi,limao,muarobaini,maji yenye vuguvugu na chumvi,paracetamol nakadharika,kama mnategemea hoaspital kupona mtaangamia sana
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa tutatembeaje vitua mbele huku tukijifukiza si tutagongwa na magari jamani?!
 
Mimi bado nina mshangao tu kuwa Rais amesema tujifukize sijui kawaza nini mheshimiwa
Kwa 'sauti' yake ile ilivyokuwa wakati wa hotuba yake ya jana (toka Chato), yaonekana alikuwa katoka kuvukizwa kama siku moja nyuma.
Ila kule kwetu ZAMANI sana ilikuwa, ukisha fukizwa unaonyweshwa mifupa na takataka nyingine ETI vilikuwa mwilini mwako. Hivi ndiko tunakokwenda tena ? Miaka yote hiyo baada ya uhuru?
 
Wewe una ndugu au jamaa zako walioathirika na kufariki?.Kama huna pita hivi na habari yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi bado nina mshangao tu kuwa Rais amesema tujifukize sijui kawaza nini mheshimiwa
Kwa 'sauti' yake ile ilivyokuwa wakati wa hotuba yake ya jana (toka Chato), yaonekana alikuwa katoka kuvukizwa kama siku moja nyuma.
Ila kule kwetu ZAMANI sana ilikuwa, ukisha fukizwa unaonyweshwa mifupa na takataka nyingine ETI vilikuwa mwilini mwako. Hivi ndiko tunakokwenda tena ? Miaka yote hiyo baada ya uhuru?
 
Mkuu, watu kama huyu mtoa post ndio Rais Magufuli amewaagiza TCRA na Polisi wawachukulie hatua. Wakikamatwa labda ndio watatuonesha hayo makaburi na hizo familia zinazolia.
 
Tatizo bavicha kutwa kuchwa mnawawazia mabaya watanzania. Dua zenu Mungu hatazikubali. Watanzania hawatakufa kama mnavyotamani. Bali hilo lichama lenu la kishetani ndilo litajifia lenyewe kwa watu kuwapuuza

Sent using Jamii Forums mobile app
Shetani anataka turudi kwenye tibambadala ili tukafukizwe. Keshaanda wanajeshi wa kusimamia kama ilivyokuwa ya KOROSHO.
 
Tembeleeni usiku wa manane sehemu zilizotajwa kama Buza makaburini mkajionee
Bahari beach eneo la kondo Buza na Mbweni acheni kusifia mapambio ya mwami wa kihutu anaetupeleka kuzimu
Mkuu mimi ni kati ya watu wachache tulio anzisha mada za kuomba serikali ichukue hatua madhubuti kudhibiti huu ugonjwa.
Nimesema hivi ili kuweka kumbukumbu sawa kwamba sipo kundi la watetezi wa serikali.

Wewe na mleta mada mmekuja na madai mazito sana ambayo yanaweza kuleta vurugu kubwa na kuvunja amani.

Kwa uzito huu kwanini hamja warekodi watu walipoteza ndugu na kuambiwa wamezikwa na mamlaka bila taarifa na ridhaa yao?

Habari kama hii tengezeni blog ya bure kuwe na majina na anuani kamili za wahanga wote, picha za baadhi ya matukio hayo ya kuzikwa watu usiku na mamlaka mlizosema ili waandishi waende kuwahoji, wananchi tupate uhakika.

Inawezekana kurekodi video na picha za hayo matukio makaburini bila kuonwa.
Tuihukumu mamala kwa makosa halali na siyo tuhuma huenda zenye malengo flani ovu ya kisiasa au kisasi.
 
Kuna jamaa yangu kaichukua familia yake yote ameipelekea Mafia kisiwani

Kanipigia anasema sehemu pekee salama kwa sasa ni huko

Nami nimemuahidi hata kwa kuogelea nitakwenda na wapendwa wangu
Kwakuwa hakuna movement restrictions, nako mtawasambazia and very soon mtakuwa kama mzizima.
 
Kwakuwa hakuna movement restrictions, nako mtawasambazia and very soon mtakuwa kama mzizima.
Ni kweli ninachokiona ni kwamba huko population ni ndogo sana kwa hio maamuzi ya kukaa mbali na makazi ya watu sio mabaya angalao tutavuta muda mrefu mpaka hapo wavuvi watakapoambukizwa na kushindwa kuvua tutahamia kwenye ugali na mboga mboga
 
Jambo la msingi hapa ni kila mtu kuhakikisha anajilinda yeye pamoja na familia yake.

Siasa katika hili jambo hazitasaidia sana.
 
Acha uzushi ndugu.

Huwezi kuongea bila ushahidi kwa kudadavua tu kauli za viongozi halafu tukuamini.

Vifo kama vimetokea si jambo la kificho lazima tu itajulikana.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uchunguzi anza wewe kwenye kaya yako, majirani, ndugu, marafiki na wafanyakazi/waateja wako au madukani/sokoni unakonunua bidhaa iwapo kuna mwathirika au marehemu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…