Tetesi: Corona inapukutisha watu Dar. Kuna wanaolalamika ndugu zao kuzikwa kinguvu na Mamlaka Dar huko Bahari Beach, Buza na Mbweni

Serikali imekupa elimu juu ya kujikinga. Unataka ikulazimishe?

Senti bai yuzingi tecno T301
Kwa hiyo kwa akili zako, serikali haina wajibu wowote.
Ni kazi bure kuendelea kujibu hoja za aina hii.
 
Watu wanaokufa kuna ndugu, rafiki au jamaa yako?Au ndio story za UNAAMBIWA?Unaambiwa na nani?Kwanini kila mtu anakuja na story za UNAAMBIWA?

Senti bai yuzingi tecno T301
Wewe mbigwa, maiti zote za wanaokufa unaletewa kwenu kuzihakiki?
 
Ninamashaka kama hii idadi ya wagonjwa inayotajwa sasa haina uhusiano wowote na tamko la WB la kukopesha nchi zilizoathirika zaidi na corona.
Hata Mimi Nina mashaka na idadi ya waliopona aliyoitaja waziri leo Kama haina uhusiano na tamko la Rais Magufuli kuhusu kuwatangaza wanaopona ya kwamba ni wengi!!!
 
Sasa huu utumbo si yeyote anaweza andika ni 'hear say' ambazo hazina ushahidi wowote!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali pamoja na Makapuni ya Simu na taasisi zingine zinazojihusisha na masuala ya kutuma, kupokea na kufanya miamara ya malipo y fedha. Zingekaa pamoja na kuangalia namna ya kusaidia kupunguza gharama kwenye hiyo miamara ili kupunguza kupokea fedha kutoka mikono ya mtu mmoja kwenda kwa mwingine.

Tujitahidi sote kwa pamoja kupiga vita hivi ili tuweze kuendelea kuona kesho iliyosalama na yenye watanzania walio na afya njema.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Siku ukiugua Corona ndipo utashangaa ni sharti lipi hukulifuata. Wanasema usitukane mamba hali hujavuka mto.

Unadhani wewe unaweza kuwa bingwa kufuata masharti ya kujikinga na Corona kuliko waziri mkuu wa Uingereza au malkia Elizabeth au Prince Charles au yule mheshimiwa mbunge?

Usisahau kuwa ugonjwa huu ungali mgeni sana. Inabidi uanze kujishangaa mwenyewe kama wewe unataka kutuaminisha kuwa ati wewe unaujua vyema zaidi.

Hujasikia tiba zingine za kujifukiza zinaweza kuwa suluhu. Tafiti bado asubuhi sana mkuu ndiyo maana labda hata mkuu yungali maabara pale Chatto akihakiki zake za kufukiza.
 

Mkuu hukusikia hairuhusiwi kutaja majina ya watu?

Mkumbusheni na Ummy inaweza kuwa wagonjwa wa Corona hamna mbona majina, picha au video zao hazipo?
 
Mtu kuwa maskini anakosa vitu vingi sana...huwa sio mkweli, mbishi hata kama hajui, jeuri kwenye jambo linalomwangamiza, uelewa na elimu ya mambo ni mdogo sana...kila kilicho cha mrengo wake atakisifia hata asipokuwa na ABC zake.

Jamani corona inaua na inaua kweli kweli.....data zinazotolewa na mataifa makubwa sio kiini macho ni za kweli.

Kwa sifa zetu Bongo na mfumo wa utawala usitegemee utaambiwa kila kitu, kuna siasa nyingi na mapambano ya propaganda za kivita utafikiri tunapambana na adui tunayemuona, hivyo tunamtisha tumejiandaa na mavifaa chungu mzima.

Corona is just around there close to you, ready to hug and kiss very softly....hakuna kelele hata tumtungue kwa mabomu.

Ifike mahali tusema ukweli maana utaponya wengi na kuokoa wengi.

Uzuri na ubaya wa corona haibugui mazee, so we are all in the cycle...hata mabingwa wa kuchukulia poa, itakuja tu ndio wataelewa maumivu ya wengine kwa ndugu zao.
 
WanaJf mlioko Dar nawapa siri sehemu salama kwa sasa ni Mafia

La sivyo subiri uzikwe huku miguu iko nje na mgambo wa jiji
Habari za Mafia?
Usiwapelekee watanzania corona kwa makusudi tu
 
Lakini pesa yetu haiwezi kusambaza virusi vya corona,au BOT wamefuta barua yao
 
Kama mnajua mnakufa kwanini msijifungie ndani?

kwani kuna mtu kalazimishwa atoke nje ya nyuma yake? Au kiherehere tu
 
Umasikini ni mzigo
 
Linakagua makaburi na kuhoji wanaofufuka bila kibali maalum.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
JF tusiwe mstari wa mbele kueneza Majungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…