JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Virusi vya Corona katika hatua ya mwanzo husababisha homa ya mapafu na kushindwa kupumua vizuri ambayo inaweza kusababisha madhara ya kudumu kwenye mapafu.
Lakini Covid-19 sio tu ugonjwa wa mapafu, inaweza kusababisha shida nyingine zenye kubadilisha mfumo mzima wa afya ya mtu.
Huongeza hatari ya kuganda kwa damu, kutokana na kuganda kwa damu hupelekea kukwama kwa mzunguko wa damu kwenye maeneo yaliyoathiriwa
Aidha husababisha hatari kubwa zaidi ikiwa damu itaganda kwenye maeneo muhimu ya mzunguko wake kama vile ubongo na mapafu
Hupelekea shambulizi la moyo na kiharusi
Huathiri misuli ya moyo na kupelekea mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida.
Upvote
0