Corona kusababisha biashara kushuka kwa asilimia 32 duniani

Corona kusababisha biashara kushuka kwa asilimia 32 duniani

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Ripoti mpya ya mwaka kuhusu Takwimu na Makadirio ya Biashara iliyotolewa jana Jumatano na Shirika la Biashara Duniani WTO, inasema biashara duniani inakadiriwa kupungua kati ya asilimia 13 hadi asilimia 32 mwaka huu, kutokana na athari za mlipuko wa COVID-19 unaokithiri kote duniani.

Ripoti inasema kupungua huko kunaweza kuchochea kuporomoka kwa biashara kulikosababishwa na msukosuko wa fedha wa kimataifa wa mwaka 2008, na kwamba kanda za Amerika Kaskazini na Asia zitaathiriwa zaidi kutokana na janga hili, wakati kanda zote za dunia zinakadiriwa kushuhudia kupungua kwa zaidi ya asilimia 10 kwenye biashara.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, biashara duniani inatarajiwa kufufuka kwa asilimia 21 hadi 24 mwaka 2021, endapo mlipuko wa virusi vya Corona utadhibitiwa.
 
Hali kama hii wenye mitaji huwa matajir na masikini huwa masikini zaid.

Watu watauza assets kwa bei za kutupa.
Watu watauza shares kwa bei za kutupa.
Maajiriwa watapunguzwa.
Makampuni yatatafta alternative za kupunguza cost za uzalishaji.
Banks zitatoa mikopo kwa matajiri.
Serikal zitakuja na stimulus programmes.
Bei za bidhaa zitapanda.
Dhamani ya pesa itashuka.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hali kama hii wenye mitaji huwa matajir na masikini huwa masikini zaid.

Watu watauza assets kwa bei za kutupa.
Watu watauza shares kwa bei za kutupa.
Maajiriwa watapunguzwa.
Makampuni yatatafta alternative za kupunguza cost za uzalishaji.
Banks zitatoa mikopo kwa matajiri.
Serikal zitakuja na stimulus programmes.
Bei za bidhaa zitapanda.
Dhamani ya pesa itashuka.


Sent using Jamii Forums mobile app
Nikweli mkuu. vip kwasis watu wakawaida wahali ya chini tunaweza kuja nanjia mbadala nakufanikiwa kiuchumi kwenye kipindi hichi??

Nahis kama tutafocus tunaweza kugundua jambo manake itakua ningum kufanya biashara(kuuza na kununua) sababu mitaji itakua midogo, bank hazitakua nahela zakutosha, sababu uchumi wa dunia umeshuka inaweza kua ngum kuimport vitu kma tulivyozoea. Labda ndomuda wasisi kuproduce na kuexport,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom