Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Ripoti mpya ya mwaka kuhusu Takwimu na Makadirio ya Biashara iliyotolewa jana Jumatano na Shirika la Biashara Duniani WTO, inasema biashara duniani inakadiriwa kupungua kati ya asilimia 13 hadi asilimia 32 mwaka huu, kutokana na athari za mlipuko wa COVID-19 unaokithiri kote duniani.
Ripoti inasema kupungua huko kunaweza kuchochea kuporomoka kwa biashara kulikosababishwa na msukosuko wa fedha wa kimataifa wa mwaka 2008, na kwamba kanda za Amerika Kaskazini na Asia zitaathiriwa zaidi kutokana na janga hili, wakati kanda zote za dunia zinakadiriwa kushuhudia kupungua kwa zaidi ya asilimia 10 kwenye biashara.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, biashara duniani inatarajiwa kufufuka kwa asilimia 21 hadi 24 mwaka 2021, endapo mlipuko wa virusi vya Corona utadhibitiwa.