Corona: Machine rahisi za kupima zilivyoleta mapinduzi ya ugonjwa Italy

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Moja kwa moja kwenye mada itifaki yote imezingatiwa.

Ninaandika uzi huu nikiwa ninafahamu kuwa Corona imetangazwa kuwa imedhibitiwa Tanzania, pasipokuwapo na takwimu zozote rasmi za kimaabara hadharani.

Ninaandika uzi huu nikiwa ninafahamu mafanikio haya makubwa ambayo Tanzania imeyapata yametokana na uongozi shupavu wa mzee baba na waziri Ummy ambao hata hivyo wote wawili si wataalamu wa tiba yoyote ya binadamu.

Ninafahamu pia kuwa mafanikio Tanzania iliyoyapata yametokana na mzee baba kulichukulia suala la Corona kuwa ni vita kamili na kumwamrisha waziri Ummy kijeshi kusonga mbele tu bila kujali lolote.

Kijeshi takwimu zote huwa ni mali za serikali, ndiyo maana bila ya shaka tokea mawazo ya mheshimiwa Mwigulu yapatikane taarifa na takwimu zote zilikoma. Tukatakiwa kuwekeza zaidi kwenye maombezi, nyungu na mitishamba.

Italy ni moja ya mataifa yaliyokuwa yameathirika vibaya mno na ugonjwa huu. Jitihada zao za kupambana nao zimekuwa wazi kwa dunia yote kuona.

Pamoja kuwa tumeshashinda vita na kuwa kesho tutakuwa mitaani kwenye vigeregere, chereko chereko na mayowe ya ushindi, hasara gani kufahamu kwingine vita hivi wenzetu wengine wameishinda vipi.

Hapa chini pana yaliyojiri Italy kivipimo.

Katika hali yoyote ile vipimo lilikuwa ni jambo muhimu, vinginevyo tunaweza kukuta badala ya ushindi tukawa njiani kujihalalishia vifo ambavyo vingeweza kuepukika.

Your browser is not able to display this video.

Your browser is not able to display this video.
 
Mchina alizingiza chaka nchi nyingi,Kenya nao wana vilalamikia vipimo.
 
Kwaiyo sasa hivi mikusanyiko ruksa tu

Mmhh! Tokea Bunda leo kumezikwa mwenyekiti wa CCM wilaya. Vikiripotiwa pia vifo vya viongozi wengine 2 CCM ndani wa wiki hii hii.

Huu ushindi vipi? Ngoma hii yaweza kuwa bado mbichi.
 
Mmhh! Tokea Bunda leo kumezikwa mwenyekiti wa CCM wilaya. Vikiripotiwa pia vifo vya viongozi wengine 2 CCM ndani wa wiki hii hii.

Huu ushindi vipi? Ngoma hii yaweza kuwa bado mbichi.
Acha tuone show hii mwisho wake ni upi mkuu ila aya ni maswala ya brainwashing tu hakuna cha ziada
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…