#COVID19 Corona ni Mtihani, Jee Ummy Mwalimu Amepasi Mtihani?. Mnaonaje Ampokee Majaaliwa as PM, na Majaliwa Ampokee Magufuli?.

P kumbuka na kurejea:
β€œSmall minds discuss people. Average minds discuss events. Great minds discuss ideas.”
AMEN
 
Kujifukiza ni kwa ajili ya kufungua njia ya hewa kutokana na mafua. COVID-19 hawaji kwa njia ya mafua tu bali wanakuwepo kwenye blood stream hivyo wanazivamia cells na kufanya mabonge ya damu kwenye mishipa ambayo inaleta embolism za aina zote.Sasa kujifukiza kunaweza vipi kufanya damu iwe nyepesi? Wewe umeangalia upande mmoja tu wa kuwa na shida kwenye njia ya hewa ambayo hata hivyo kujifukiza siyo dawa iliyothibitishwa inatibu kwa asilimia 100, ndiyo maana wazee wetu wengine walipona wengine walikufa, na wote walijifukiza kama mnavyofanya leo (Wengine wanakufa, wengine wanapona kutegemeana na jinsi ugonjwa ulivyoshambulia mapafu, koo au kwenye damu/cells)
Bado kujifukiza siyo tiba kwa asilimia kubwa....Kwa mafua ya kawaida ni sawa ila kwa COVID-19 inaweza kusaidia kwa kiasi fulani ukichanganya na dawa zingine.
 
Paskali, kadri siku zinavyozidi kwenda ndivyo na uwezo wako wa kuwasilisha mada zenye mashiko unazidi kudumaa, yaani huoni aibu kuandikia Umma kwamba unamuangalia Ummy kwa umbo lake na kwamba unataka kutushawishi kumuona anafaa kuwa kiongozi mkuu wa mawaziri ?, watanzani bado tuko kwenye matope, yaani wewe ndio mjanja miongoni mwa wasukuma walio wengi ?, yaani wewe ndie uliewatangulia wasukuma wenzako kutangulia walau kuingia mjini mapema ?, kupata hako kaelimu kidogo ??, shame on you
 

P,
Ana sifa moja ambayo wengi kwenye serikali ya Magu hawana. Ni Mzuri kwenye mawasiliano na ni rahisi kumwelewa.
 
Yaani wewe hadi leo hujapata jibu? Hujiulizi kwanini watu walikuwa wanazikwa usiku? Hujiulizi kwanini takwimu zilikuwa zinafichwa?
 
Pascal Mayalla najua umemuelewa sana huyo dada, hupo peke yako mkuu hata mimi, dada kakamilia kwa kweli.

Ila anatakiwa kujiunga na upinzani kama Bulaya hapo ndipo tutamkubali Zaidi. Na chama cha ACT ndio wanaendana kabisa, Karibu Upinzani Ummy.
 
Ummy kafanikiwa kuficha ukubwa wa ugonjwa
 
Kilichomsaidia ni kukubali kila agizo na kutumikia usiri na amri za kuficha ukweli kama alivyoagizwa. Waliojifanya wajuaji kama vile naibu wake wameishia nje. Kwahiyo ni hatari sana kufikiri Ummy anauwezo, labda uwezo wa kuficha ukweli kwa gharama ya maisha ya wanachi.
 

Kati ya comments nyingi za kijinga za Mayalla, hii imezizidi zote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…