johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 97,869
- 171,716
Inasemekana hadi sasa sekta ya Utalii ndio imepata pigo kubwa sana kufuatia kuzuka kwa ugonjwa wa Corona.
Wataalamu wanasema nchi zinazotegemea sana utalii katika uchumi wake zitayumba sana hata baada ya ugonjwa huu kudhibitiwa. Inashauriwa Wachumi na wanasiasa waanze kubuni sasa mikakati ya kuimarisha chumi zao kwani kutakuwa na udhibiti mkubwa wa wazungu kuja Afrika na hata aina ya misaada itakayotolewa.
Kwa sasa nchi makini duniani zimewapeleka likizo wanasiasa na nafasi yao kuchukuliwa na Wachumi kwani kuna uwezekano mkubwa mfumo wa Siasa ukabadilika kabisa duniani. Zama za mbumbumbu kutafuta ajira kupitia Siasa ndio zinafikia mwisho wake na barani Afrika wanasiasa wengi wataziacha ofisi zao kwa kuhofia nguvu ya Umma.
Maendeleo hayana vyama!