joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,617
Kenya ni nchi ya ajabu sana, hawajui nini wanataka. Uganda na Rwanda zimeanza kulegeza vikwazo baada ya kujiridhisha kwamba hakuna tena maambukizi ndani ya jamii "local transmission", Kenya imeua kuiga kulegeza masharti kipindi ambacho maambukizi ndani ya jamii ndio yanaongezeka kwa kasi kubwa zaidi. Hiyo ndio maana halisi ya " Failed state".
======
Watu wameanza kurudi katika sehemu zao za kazi huku idadi ya watu walioambukizwa virusi vya corona ikiendelea kuongezeka kwani jumanne watu 45 zaidi walipatikana na ugonjwa huo na kufikisha jumla ya visa 535 nchini .
Watalaam sasa wanasema serikali haingefaa kutumia vipimo vya sampuli 25,869 kama kigezo cha kuruhusu kufunguliwa kwa mikahawa kabla ya kufanikisha vipimo vya watu wengi hasa katika maeneo yanayoshukiwa na visa zaidi vya maambukizi.
Jumanne waziri wa afya Mutahi Kagwe alidokezea kwambahuenda serikali ikalazimika kufunga tena mikahawa kwa miezi sita kwa kutotii kanuni zilziotangazwa na wizara yake kabla ya kufunguliwa. Watalaam wamesema idadi ya maambukizi itapanda hata zaidi huku serikali ikizidisha mpango wake wa kuwapima watu zaidi katika maeneo yalio hatarini.Tayari kuna sehemu za Jiji la Nairobi ambazo zimeanza kuibuka kama vitovu vya maambukizi baada ya watu wengi kupatikana na ugonjwa huo.Mtaa wa Eastleigh unaongoza kwa visa 64 ukifuatwa na kawangware kwa 24.katika eneo la Mombasa Old Town visa 39 vimeripotiwa.
Mtaalalm wa matibabu Erick Njogu ambaye amekuwa akifuatilia kwa kina maambukizi ya virusi ya Corona katika mataifa mengi duniani anasema kenya ilikimbilia kurejelea shughuli za kawaida ikifuata mfano wan chi kama Italia na China ambazo zilikuwa zimetangulia kusajili maambukizi na kufika kilele katika idadi ya waliokuwa na ugonjwa huo .Amesema takwimu za sasa za vipimo vya Kenya vikilinganishwa na idadi ya watu nchini zaidi ya milioni 45 haiwezi kutegemewa kufanya maamuzi ya kufungua sekta mbali mbali za uchumi bila kuhatarisha maisha ya wengi .
‘Kosa kubwa ambalo serikali ilifanya ,ni kutoa dhana potovu kwa wakenya kwamba maisha yanaweza kuendelea kwa njia ya kawaida kabla ya kuboresha mikakati ya kuwapima watu wengi’ Njogu amesema.
Aliongeza kusema ;‘Itakuwa vigumu sasa kuwarudisha watu katika nyumba zao kwa sababu wengi wamechoka kusalia ndani na shughuli zao za kipato pia zipo hatarini,Ingekuwa bora kufanya uamuzi huo baada ya kupata hakikisho lakupima idadi ya juu ya watu ili kukadiria hatari na jinsi inavyoweza kudhibitiwa’
Chanzo: Opera News
======
Watu wameanza kurudi katika sehemu zao za kazi huku idadi ya watu walioambukizwa virusi vya corona ikiendelea kuongezeka kwani jumanne watu 45 zaidi walipatikana na ugonjwa huo na kufikisha jumla ya visa 535 nchini .
Hatua ya serikali kutangaza kufunguliwa kwa mikahawa huenda ndio inayowafanya watu kuanza kurejelea shughuli zao za kawaida na kuhatarisha maambukizi zaidi kwani maeneo mengi ya katikati mwa jiji la Nairobi yameanza kufurika watu huku masharti ya kuzuia maambukizi katika baadhi ya hoteli na magari ya usafiri wa umma yakipuuzwa na wananchi .Watalaam sasa wanasema serikali haingefaa kutumia vipimo vya sampuli 25,869 kama kigezo cha kuruhusu kufunguliwa kwa mikahawa kabla ya kufanikisha vipimo vya watu wengi hasa katika maeneo yanayoshukiwa na visa zaidi vya maambukizi.