Alkisak
New Member
- Sep 7, 2020
- 0
- 0
CORONA SI KIGEZO CHA KUMFANYA MAGUFULI KUWA BORA KULIKO LISSU
Ni kweli sisi kama Watu wa kiimani za dini tumefurahishwa sana approach alizotumia Rais Magufuli hasa katika namna alivyoweza kulishughulikia janga la kidunia la Corona kwa Kumtanguliza Mungu na kukataa kabisa Lockdown yoyote wala Baba yake lockdown na kuzuia kabisa Nyumba za ibada zisifungwe kwasababu ya Corona, bali alihamasisha watu kuendelea kumuomba Mungu kwa kutangaza siku 3 za kumuomba Mungu atuepushe na janga hili.
Kwa approach hii aliyotumia kusema kweli nimpongeze sana Magufuli maana aliona kwa janga hili kwa uwezo wa wanadamu hilo lisingewezekana ila kwa Mungu linawezekana, ndio sababu ya kutumia Approach ya kiimani si ya kisiasa. Na kusema kweli imefanikiwa kwa sehemu kubwa na kuwa msaada hata kwa wale walioibeza kwa mara ya kwanza na kuipuuza, leo hata wao wanafurahia uhuru wa kukusanyika pamoja hasa katika kampeni zetu.
Lakini pamoja na yote bado hilo halimfanyi Rais Magufuli aonekane bora na mcha Mungu kuliko Tundu lissu eti kwa sababu ameonekana kumtanguliza Mungu wakati wa janga la corona na approacha yake ikafanikiwa. Lazima tufahamu ni kweli approach zao kati ya Magufuli na Lissu (Wapinzani) zilitofautiana lakini wote walikuwa na nia moja kutaka kutafuta suluhu ya kuepusha watu wasife kama ugonjwa ulivyo na hatari ya kusambaa na kuua kwa haraka.
Ni lazima tufahamu Wapinzani (Lissu) ni wanasiasa na approach zao sio ajabu kuona ni za kisiasa. Ni Ukweli usiopingika approach za ulimwengu mzima hata mataifa makubwa na mashirika ya afya duniani (WHO) ndio yaliyoshauri nchi mbalimbali duniani kuweka watu lockdown ili kuepusha maafa kwa watu kutokana na janga la Corona.Je ni dhambi gani kwa mwanasiasa kama Lissu kushauri serikali yetu kufuata approch ya WHO ya kuweka watu Lockdown na kupingana na Approach ya Magufuli?
Ishu ya Lockdown sio ishu ya Tundu Lissu au wapinzani bali ni ya WHO, wao walikuwa wanaishinikiza serikali kufuata ushauri wa kidunia.Je wao wamekuwa maajenti wa shetani kwa kuishauri serikali yetu kufuata ushauri wa kisiasa uliotolewa na shirika la Afya duniani (WHO) kinyume na approach ya Magufuli ya Kutumia maombi ambao ni approach ya kiimani?
Mbona ni kawaida kabisa pale nchi inapoingia katika hali ya hatari kama ya Magonjwa ya milipuko au Vita, ni kawaida Rais kuzuia makusanyiko yoyote hata makusanyiko ya kidini yaani ibada huwa zinafungwa pale hali ya vita ya hatari inapotokea, si kwasababu ya roho ya mpinga kristo ila inashauriwa kuweka watu lockdown mpaka pale nchi inaporudi katika hali ya usalama mzuri wa watu.Hivyo hata kwenye hili swala la Corona, kama wapinzani walishauri serikali kuweka watu lockdown kwasababu janga la corona lilikuwa linaonyesha hali ya hatari ya watu kuweza kufa hivyo solution ya haraka ambayo inatumika duniani ni kuzuia makusanyiko wala sio kwasababu wanatumiwa na Roho ya mpinga kristo.
Jambo la pili, lazima ufahamu Magufuli na Lissu wote watu wa dini wala hajaokoka hivyo si ajabu kutoa ushauri wa kisiasa badala wa kiimani katika janga Kubwa kama hili la Corona.Wala Magufuli sio wa kiroho sana au ana hofu ya Mungu sana kumzidi Lissu eti kwasababu ameonekana kumtanguliza Mungu kwa maombi katika swala la corona. Magufuli naamini ni Rais ambaye hata approach hiyo aliyoitumia ameitumia kwa kushauriwa sana na watumishi wa Mungu na viongozi wa dini ambao wana macho ya rohoni waliotambua kuwa huu ugonjwa hauondolewa kwa solution za kisiasa bali kwa maombi. Hivyo Hata angekuwa Rais Lissu bado angeweza kupokea ushauri huo huo na angemtanguliza tu Mungu kama alivyofanya magufuli.
Lakini jambo la tatu, Tundu Lissu hakupuuza maombi wala si kwamba hatambui umuhimu wa kumtanguliza Mungu katika maswala mazito ya nchi, maana uhai wake wenyewe ni muujiza tosha wa kujua kazi ya maombi ilivyo na nguvu na si mara moja alikuwa aliomba sana watanzania wamuombee ili apone hivyo ni vigumu kupuuza maombi wakati wa corona wakati anaujua uweza wa maombi ndio uliomfanya awe hai mpaka leo anagombea Urais kupitia Chadema.
Ila alichokipuuza kwenye ile audio na kuita idiot (Punguani) ni kile kitendo cha kuhamsisha watu waombe alafu waache kuchukua tahadhari zote zinazotolewa kwa ushauri wa kidunia, hilo ndilo aliita idiot ila hakumpuuza Mungu wala hakuwaona Mapunguani wale waliomtanguliza Mungu kwa maombi. Bado maombi yana umuhimu sana lakini bado tulipaswa pia kuchukua tahadhari nyinginezo ndio maombi yetu yatakuwa na maana
Jambo la nne, lazima tufahamu tupo kumchagua Rais anayetufaa katika maeneo yote ya kiuchumi, kisiasa, kielimu, kimaendeleo si tu katika eneo la kiimani pekee (la kidini). Swala la Corona, Mungu anaweza kumtumia mtu yeyote hata kama hana hofu ya Mungu, kutimiza kusudi lake, alimtumia Farao,Nebukadeneza hivyo hata kama angekusudiwa kutumiwa Lissu kama angekuwa Rais angetumika tu vizuri.
Hatumchagui magufuli kwasababu kalitatua vizuri swala la corona kwa njia za kiimani, Mbona huyo huyo Magufuli na serikali yake ndiye iliyopiga marufuku maombi yasifanyike ya kumuombea Tundu lissu yaliyopangwa kufanyika nchi mzima kwa kukutanika katika viwanja mbalimbali vya Tanzania ambapo walituma Polisi kuyazuia kabisa? Je tuseme wamempuuza Mungu na walifurahia Tundu lissu asiiombewe ili afe?
Mbona yapo matukio mengi ambayo Magufuli na Serikali yake wamewafanyia viongozi wa dini na kuwadharisha na wengine wamewanyang'anya passport zao mpaka leo hawajarudishiwa kwasababu tu ya kuikosoa serikali.Je tuseme Magufuli hafai kwasababu aliwapuuza watumishi wa Mumgu/Viongozi wa dini? Wapo mashehe wamefungwa gerezani kwa kuiokosoa serikali, wengine wamepewa kesi nyingi tu na serikali hii hii, Je tuseme hafai kwasababu hizo za kuonyesha kutoheshimu viongozi wa dini? Je tuseme hana hofu ya Mungu?
Jambo la msingi tusisimame kwenye uchaguzi huu kwa kuchukuliwa na hoja nyepesi za kuwaona wagombea fulani ndio wacha Mungu sana kuliko wengine kwasababu ya hoja moja ya Corona wakati yapo mabaya mengi ya kutoonyesha hofu ya Mungu aliyoyatenda.Rais Magufuli Alikataa kuhidhinisha pesa kwa ajili ya matibabu ya Lissu, ina maana alikuwa anataka afe? Hakusimama hadharani kukemea hao watu wanaoitwa wasiojulika na wala hakutoa Pole kwa Tundu lissu alipopatwa na Shambulio lile la hatari, kweli huo ni ucha Mungu?.
Tuachane na maswala ya ucha Mungu na maswala ya Corona, hatutafuti malaika wala hatufuti mchungaji wa kutupeleka mbinguni ila tunatafuta Rais mwenye uwezo wa kutukwamua katika mkwamo wa kiuchumi kwa kutuletea maendeleo ya watu na uhuru wa maoni, uhuru wa kuabudu n.k