Corona: Tusinyoosheane vidole. Kama unaweza kusaidia, please do. Usisubiri uombwe - jitokeze saidia, vinginevyo nyamaza!

Snitich kazini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yes, na ukisaidia unyamaze.....hatutaki popularity kupitia janga hili...
 
Rais Magufuli hajakataa kushauriwa, alichokataa ni kushinikizwa!, kulazimishwa!.
Mkuu mbona unatuona kama sisi watanzania ni wajinga sana? hivi ulichoandika na ulichosema vinaendana kweli? wewe kama mwandishi najua utakua na hotuba zake nenda katafute usikilize upya na sio unakuja kutugeuzia maneno hapa!!
 
Watu wakulaumiwa na kunyooshewa vidole wapo.
Sina msaada wowote lakini pia sitaki kupangiwa cha kusema.
 
Mkuu PASKALI najua ulidhamiria kufikisha ujumbe muhimu lakini utawaambia nini hawa binadamu kwa sasa wakuelewe...!!
Hawa hawa binadamu walihimiza na kushauri hatua stahiki zichukuliwe mapema kabisa lakini walijibiwa ovyo ovyo na wenye mamlaka...
Binafsi nilishauri serikali ifanye makubwa zaidi... Ituachie sisi kuchukua tahadhari ikiwa ni pamoja na kunawa mikono kwa maji tiririka...
PASKALI; We played our parts thinking that the government will also take more effective measures but it surely didn't!
Usituzuie kuwalaumu na kuwanyooshea vidole...!!
Na hata sasa hali ilipofika pabaya bado hawajajipanga kuboresha huduma mahospitalini kukabiliana na ongezeko la wagonjwa...!!!
Please... Tushauri kuongeza juhudi za kuwalaumu badala ya kuwanyamazia...
May be they will comeback to their correct senses to see this pandemic in the way that it deserves to be seen!!
Kule Italia ilifikia hatua wananchi walianza kuzitupa pesa zao kwenye mitaro na mabarabarani wakiamini si uchumi wala pesa ni muhimu kwa sasa!!!😩😩😩
 
Mkuu mbona unatuona kama sisi watanzania ni wajinga sana? hivi ulichoandika na ulichosema vinaendana kweli? wewe kama mwandishi najua utakua na hotuba zake nenda katafute usikilize upya na sio unakuja kutugeuzia maneno hapa!!
Mkuu Upepo Pesa, rais Magufuli ni Msukuma wa kuzaliwa, kukulia na kosea kijijini, hivyo lugha ya Kiswahii fasaha ni issue, rais lazima ashauriwe na kila siku anashauriwa na kuna mambo kibao anafuata ushauri na matokeo tunayaona.
Ushauri kwa rais ni ushauri wa aina mbili
1. Ushauri wa Wajibu- huu ni ule ushauri ambao rais anashauriwa na washauri mbalimbali ambao hao ni wajibu wao kumshauri rais na ushauri wao ni wa siri, rais anakuwa free kutekeleza au kuupuuza pia ni siri.
2. Ushauri wa bure na wa wazi, ni ushauri unaotolewa na Mtanzania yoyote kuhusu jambo lolote, ushauri huu unakuwa wa wazi, uko open, na rais yuko free kuutumia au kuupuuza.

Kunapotokea tatizo au janga kubwa la kitaifa kama hili janga la Corona, wewe kama una ushauri wa jinsi ya kusaidia, utoe tuu kwa uwazi, openly, ili ukipuuzwa kikija kutokea cha kutokea, utakuwa na haki ya kulaumu kwa hoja kuwa ulishauri kabla lakini ukapuuzwa.
Naamini Rais Magufuli ana washauri wazuri na anashauriwa vizuri tuu! , Ila... - JamiiForums
P
 
Hiki ndio kinachotokea kwa sasa.

Mara ngapi tulishauri ndege zizuiwe wakapuuza? baada ya kuona hali mbaya ndio wakazuia infact haikua na maana sababu mashirika mengi yalikua yamezuia safari zao..

Haya leo tena tunashari dsm ifungwe nani anasikia?

Kwa mtindo huu ndio maana tunanyoosheana vidole... na kwasababu ushasema "nitakua na haki" basi acha kunizuia maana ni haki yangu kufanya hivyo.
 
Mkuu Jay One, asante kwa hii
Corona: Tusinyoosheane vidole. Kama unaweza kusaidia, please do. Usisubiri uombwe - jitokeze saidia, vinginevyo nyamaza! - JamiiForums
P
 
Wandugu, hapa nafanya tuu follow up ya Corona nikipitia kujikumbusha niliwahi kuandika nini au kusema nini kuhusu Corona na hiki kinacho endelea sasa. Corona is real tusifanye masihara, tujilinde kwa kufuata ushauri wa kitaalamu.

Kila Jumamosi asubuhi kuanzia saa 1:30 hadi saa 3:00 asubuhi , Star TV, huwa ninakuwa live kwenye kipindi cha TV cha Jicho Letu Ndani ya Habari ambacho huwa kinatangwa live na Star TV kila siku za Jumamosi asubuhi, kwa Jumamosi ya kesho, mgeni wetu ni Waziri wa Habari, Dr. Harrison Mwakyembe tukijadili kuhusu athari za Corona kwenye sekta ya Habari, nini kifanyike.

Ukipata nafasi karibu utufuatilie.

P
 
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU YATOKANAYO NA RIPOTI YA KAMATI MAALUMU YA MHESHIMIWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA KUFANYA TATHMINI YA UGONJWA WA COVID-19 NCHINI
DAR ES SALAAM 17 MEI, 2021

Ndugu wanahabari, mtakumbuka kwamba kupitia hotuba ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliyoitoa tarehe 6 Aprili, 2021 wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam kuhusu kuunda Kamati ya kitaalamu ya kufanya tathimini ya ugonjwa wa COVID-19 na baadaye msisitizo alioutoa tarehe 22 Aprili, 2021 wakati akilihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma, naomba kuwajulisha kuwa Kamati hiyo imewasilisha rasmi ripoti yake kwa Mheshimiwa Rais leo tarehe 17 Mei, 2021.

Ndugu Wanahabari, Kamati ilifanyia kazi hadidu za rejea 12 zilizohusu maeneo mbalimbali ya tathmini ya mwenendo wa ugonjwa pamoja na afua za udhibiti wa COVID-19 ikiwemo chanjo hapa nchini, kikanda na kimataifa.
Ndugu Wanahabari, Tangu kuingia kwa ugonjwa wa COVID-19 nchini mwezi Machi 2020, Tanzania imekumbwa na mawimbi mawili makubwa na hivi sasa kutokana na mwenendo wa ugonjwa huo katika mataifa mengine duniani na kuna tishio la kutokea kwa wimbi la tatu hapa nchini.

Ndugu Wanahabari, Baada ya uchambuzi wa kina Kamati imependekeza yafuatayo:
1. Serikali ihuishe mipango ya dharura (Contigency and Response Plans) katika ngazi zote kwa ajili ya kukabiliana na majanga likiwemo janga la ugonjwa wa COVID-19.
2. Serikali itoe taarifa juu ya uwepo wa ugonjwa wa COVID-19 na ichukue hatua madhubuti kuimarisha hatua zote za afua za kinga (interventions) katika ngazi zote ili kuepusha wimbi la tatu la ugonjwa huo.
3. Wataalamu wa afya watimize wajibu wao kitaalamu, kwa kuzingatia weledi, miiko na maadili katika kuelimisha, kukinga na kutibu ugonjwa wa COVID-19 nchini.
4. Tanzania ishiriki ipasavyo katika maamuzi na itekeleze maazimio ya kikanda na kimataifa iliyoridhia katika jumuiya za EAC, SADC, AU na WHO.
5. Kuhusu chanjo dhidi ya ugonjwa wa COVID-19:
a. Kamati inashauri Serikali kwa kutumia vyombo vyake iendelee na hatua kuelekea kuruhusu matumizi huru ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa COVID-19 kwa kutumia chanjo zilizoorodheshwa na Shirika la Afya Duniani ili kuwapa fursa ya kinga wananchi wake kwa kuwa kupitia uchambuzi wa Kamati, chanjo hizo zina ufanisi na usalama unaokubalika kisayansi;
b. Pamoja na mapendekezo haya, Kamati Huru ya Kitaifa ya Ushauri wa Chanjo (NITAG) na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) ziendelee kushirikishwa katika kutoa ushauri na kudhibiti chanjo hizo;
c. Kipaumbele cha utoaji wa chanjo dhidi ya COVID-19 nchini kwa kuanzia kiwe katika makundi yafuatayo kwa umuhimu:
i. Wahudumu katika vituo vya kutolea huduma za afya na watumishi walio katika mstari wa mbele wa utoaji wa huduma (frontline workers) mathalani watumishi sekta ya utalii, hoteli, mipakani, viongozi wa dini na mahujaji;
ii. Wazee na watu wazima kuanzia umri wa miaka zaidi ya 50;
iii. Watu wazima wenye maradhi sugu mengine (comorbidities) mathalani kisukari, shinikizo la damu, maradhi ya mfumo wa upumuaji, magonjwa ya figo n.k.;
iv. Watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama; na
v. Wasafiri wanaokwenda nje ya nchi.
d. Kufanya uhamasishaji na maandalizi ya upokeaji, utunzaji, usafirishaji na utoaji wa chanjo na wananchi wawe huru kuamua kuchanja au la.
e. Serikali iratibu upatikanaji wa chanjo kwa watumishi wa taasisi za kimataifa walioko nchini.
6. Serikali ya Tanzania ijiunge na COVAX Facility kwa kuwasilisha andiko la kupatiwa chanjo, kwa kutumia fursa inayotolewa na GAVI.
7. Serikali itumie fursa zilizopo wakati huu wa janga la COVID-19 kuanza mchakato wa uanzishaji wa viwanda vya kutengeneza chanjo.
8. Serikali iimarishe huduma za uchunguzi kwa kuijengea uwezo Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii na maabara nyingine nchini ili kupanua wigo wa upimaji wa ugonjwa wa COVID-19.
9. Serikali ijenge uwezo wa ndani wa utambuzi wa virusi anuai vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19 na magonjwa mengine ya kuambukiza.
10. Serikali itoe takwimu sahihi za ugonjwa wa COVID-19 kwa umma na Shirika la Afya Duniani ili wananchi wapate taarifa sahihi toka Mamlaka za Serikali na kuheshimu makubaliano na kanuni ambazo nchi iliridhia.
11. Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ikamilishe mwongozo mpya wa matibabu ya ugonjwa wa COVID-19.
12. Serikali iendelee kuhakikisha kuwa matumizi ya tiba asili na tiba mbadala katika mfumo rasmi wa tiba za kisasa yanazingatia misingi ya kisayansi.
13. Serikali iendelee kutoa fursa na kuwawezesha wanasayansi kufanya tafiti kwa kufuata miiko, maadili na taratibu zilizowekwa ili kuimarisha kinga, tiba, uchunguzi wa ugonjwa wa COVID-19 na athari zake katika jamii nchini.
14. Serikali iendelee kuzingatia mazingira ya kitanzania katika udhibiti wa ugonjwa wa COVID-19 katika kuamua kuweka au kutokuweka shuruti ya kujifungia (lockdown) na kuwa na ubunifu ili kuruhusu ukuaji wa uchumi na kuimarisha sekta zinazochangia katika uchumi.
15. Wizara yenye dhamana ya fedha na uchumi ifanye tathmini ya kina ya athari za janga la COVID-19 na kuweka mpango madhubuti wa haraka wa sasa, wa muda wa kati na wa muda mrefu unaotekelezeka ili kukuza uchumi wa nchi.
16. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ziendelee kushirikiana ipasavyo katika hatua zote za kukabiliana na janga la COVID-19 pamoja na majanga mengineyo ikiwemo utoaji wa nyaraka za kimataifa kama vile Travel Advisory Note.
17. Idara ya Maafa katika Ofisi ya Waziri Mkuu iendelee kutekeleza ipasavyo jukumu la uratibu na kutoa rasilimali husika wakati wa majanga ya kitaifa na kimataifa kama ugonjwa wa COVID-19 kwa kushirikisha ngazi na sekta zote.
18. Serikali ikamilishe malipo ya madeni ya watoa huduma na watumishi waliokuwa mstari wa mbele katika kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19 ili kuongeza ari na tija ya udhibiti wa ugonjwa huo.
19. Serikali iendelee kushirikisha wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini, wadau wa maendeleo, sekta binafsi na vyombo vya habari katika mapambano dhidi ya janga la ugonjwa wa COVID-19.

Ndugu Wanahabari,

Asanteni kwa kunisikiliza.
Hii ni C&P

Thanks for this!. Alale pema peponi!, sisi tulio duniani, lazima tuendelee kuishi, kama ili kuishi ni pamoja na kupindua misimamo ya kijima ya mtangulizi, then ni bingiribingira mpaka Makka!. Kuna mambo kwenye mapendekezo hayo akina sisi tulishauri, na sasa ndio yameshauriwa na wataalamu, tuachage siasa kwenye proffesionalism, tupige siasa kwenye siasa, tuache wataalam kwenye issues za kitaalamu. Corona inatufundisha Tanzania tuna tatizo kuchanganya siasa na professionalism. Hongera Prof. Janabi kwa elimu uliyotoa, so far you are the best!
P.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…