Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Siku ya leo Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ametangaza hatua kuu muhimu za kijamii na kiuchumi za kuwanusuru raia wa Kenya kutokana na madhara yatakayotokana na hatua za kudhibiti athari za kuenea kwa maambukizi ya Corona nchini Kenya.
Pamoja na ukosoaji mwingi uliokuwepo na uliopo kutoka kwa wakenya wengi kuhusu kuchelewa au kuzembea kwa serikali ya Kenyatta kuchukua hatua katika kukabiliana na athari za maambukizi ya Corona, lakini hili la leo lililofanywa na Rais Uhuru Kenyatta litabakia kuwa kumbukumbu nzuri ya kudumu katika ukanda wa Afrika mashariki, Maziwa makuu, kusini mwa jangwa la Afrika, Afrika au Dunia kiujumla.
Kwa uchache hizi ndio hatua ambazo Uhuru Kenyatta amezitangaza leo....
-Mshahara wa chini ya shilingi Laki tano za kitanzania hautakatwa kodi kabisa.
-PAYE Kupunguzwa kwa 5% (kutoka 30% mpaka 25%)
-Corporation tax kupunguzwa kwa 5%
-Turnover tax kupunguzwa kwa 2%
-Jamii isiyojiweza imetengewa zaidi ya bilioni 200 za kitanzania.
-Kusitishwa kwa muda riba katika mikopo ya biashara zitakazo dumaa au kufirisika katika kipindi hichi cha mlipuko wa Corona.
-VAT Kupunguzwa kwa 2% (Kutoka 16% mpaka 14%)
-Kuidhinisha mara moja zaidi ya shilingi bilioni 20 za kitanzania kutoka mfuko wa Afya kwenda kupambana na Corona.
-Kupunguza mishahara ya maafisa wa juu wa serikali kwa karibu 80%.
-Watumishi wenye umri mkubwa au wenye afya dhaifu kupewa likizo huku wakiendelea kula mshahara kama kawaida wakiwa majumbani mwao.