Corona Virus Mauritania yafunga Airport

Corona Virus Mauritania yafunga Airport

Nyamsusa JB

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2015
Posts
567
Reaction score
1,564
Habarini wanajanvi.

Jana nilirudi kazini Mauritania. Watu wote tuliofika na Ndege za jana tumewekwa kizuizini kwa siku 14 kuangalia kama tuna maambukizi ya Corona virus. Hivyo tutakuwa hapa hotelini kwa siku 14. Haturuhusiwi kutoka vyumbani na wala kukutana na watu.

Pia leo Airport imefungwa kwa muda usiojulikana mpaka hapo itakapotangazwa.

Vipi huko Nyumbani hatua kama hizi zimechukuliwa.

Tuombe Mungu hii Issue inakuwa Mbaya kila Uchao.

Tutafahamishana hali ilivyo kadri ya siku 14 zangu kizuizini. Tuombe Mungu.
 
Hamruhusiwi kutoka vyumbani wala kukutana na watu...!

Vipi kuhusu chakula inakuaje mkuu.

Wamearrange sehemu ya kulia chakula. Wahudumu wanaleta bila sisi kuwepo then wanatutaarifu kwa simu. Tunaenda kula au kuchukua hicho chakula ukimaliza unarudisha vyombo au vifungashio kwenye hicho chumba.
 
Hizo siku 14 nani anawa hudumia hapo hotelini?
Nani anawa gharamia?


Sent using Jamii Forums mobile app
Tumepelekwa Hotel mbalimbali. Mimi na mwenzangu mmoja kutoka Zimbabwe tulichukuliwa Hotel na Kampuni tunayoifanyia kazi. Arrangement ya hapa ndio nitakayoiupdate as we countdown 14 days. Waliopelekwa Hotel zingine sijui arrangement za huko.
 
Back
Top Bottom