Ng'wanamalundi
JF-Expert Member
- Feb 4, 2008
- 1,203
- 1,422
Habarini za jioni wanajamvi.
Mimi siishi Dar Muda mfupi uliopita niliona ujumbe kwenye WhatsApp ya ndugu mmoja ikionyesha magari yakipita Kariakoo yakifukizia dawa ya kuua corona, sawasawa na yale yaliyokuwa yakionekana kwenye miji ya Uchina.
Hii ni hatua kubwa na nzuri sana iliyochukuliwa na Serikali kukabili janga hili. Baada ya kuona 'clip' hiyo nilikimbilia hapa JF nikifikiria nitapata habari zaidi hapa kwa kuwa nyuzi huanzishwa hapa hata juu ya tetesi tu ya kitu tarajiwa na watu hufurika kuchangia nyuzi hizo. Nimestuka kwamba hakuna chochote humu JF juu ya habari hii!
Je, hii ni kwa sababu suala lenyewe si muhimu? Au ni kwa sababu ni hatua nzuri iliyochukuliwa na Serikali na wachangiaji wengi wa humu JF wamejikita kwenye mada za kulaumu Serikali tu? Kwa kuwa hili ni jambo zuri lisilolaumika, labda ndiyo maana wachangiaji hao wameona wakae kimya tu?
Kwenye 'clip' hiyo niliwasikia wakazi wa hapo Kariakoo na viongozi wa Machinga wakisifia hatua hiyo na mmoja wa wachangiaji akagusia kwamba hatua hiyo iliagizwa na Mkuu wa Mkoa.
Labda ndiyo hilo limeleta nongwa kwa kuwa hakuna mtu anayekuwa tayari kumpongeza Makonda au Serikali ya JPM kwa ujumla. Watu wamejikita katika kumlaumu Makonda tu na Serikali ya JPM.
Naomba mjuaji anielimishe kuhusu hili.