Salim A. Msangi
JF-Expert Member
- Apr 26, 2011
- 566
- 511
Kwa miongo kadhaa sasa kumekuwa na juhudi za makusudi za kutoa chanjo zinazo lenga kupambana na aina Fulani ya maradhi na mahusisi kwa makundi tofauti ya watu, rika, maeneo na hata nchi. Pamoja na kwamba chanjo hizi zimekuwa zikipokea upinzani mkubwa, tena wakitafiti, wenye hadidi rejea za kutosha lakini bado zimeendelea kutolea kwa njia na taratibu mbalimbali tena bila gharama yoyote kwa mpokeaji wa chanjo hiyo.
Hata hivyo watu kama mimi tumekuwa tukiandika kwa muda mrefu kwamba kunayo mpango mahususi unao andaliwa ambao utawalazimisha walimwengu wote wapewe chanjo. Katika link nilizo kwisha zitoa huko nyuma kwenye mfululizo wa bandiko hili la Corana zinaonesha mpango huo, na kama ilivyo mipango mingine ya waheshimiwa hawa, hakuna kinacho hitajika Zaidi ya sababu tu.
Baada ya janga hili kuibuka, imekuwa wazi sasa, lisemwalo lipo. Wale walio kuwa wakishangaa na kusema itawezekanaje kwa dunia nzima kupigwa chanjo, nadhani sasa wanaanza kuelewa.
Mara kadhaa imesemwa dunia haiwezi kurudi kama kawaida mpaka welimwengu wote wapokee chanjo. Wenye akili huru wanajua hili si janga la kimazingira, wanao tuambia hii ni adhabu ya Mola kwa makosa yetu sasa tunaadhibiwa wanapotosha ukweli, namna mambo yanavo funguka moja baada ya jingine ni wazi hili ni jambo lilikuwa linasubiriwa, huu ni mango ulio andaliwa na walio andaa mpango huu, wanayo malengo mahususi na moja wapo bila kumumunya maneno ni CHANJO.
Kwanini chanjo?
Majibu ni mengi kutegemea nani anauliza, nan ani ndiye anaye toa majibu.
Kwanza suala la “ku-make business out of it’, litupe kwenye dustbin, kuna makampuni kadhaa, kuna watu kadhaa, kuna taasisi na hata nchi kadhaa zitakazo tengeneza fedha nzuri kwenye hili. Lakini hili siyo lengo kuu, hii kwao ni motisha kwa wale watakao simama na sisi, hii ni zile athari za mbali sana na zitawagusa watu fulani mahususi, sababu mahitaji, matakwa na maono ya watu hao yameshavuka kwenye vitu vinavyo itwa pesa, hela, nk, hiyo kwao ni michezo ya watoto,
Hivyo chanjo inakwenda kuwapatia kile ambacho pesa haiwezi kuwapatia.
Chanjo inakwenda kuwapa kitu kimoja muhimu, cha msingi, mahususi na bila kitu hicho, mpango huu wa Zaidi ya milenia kadhaa siyo kitu, ushindi wao unaanzia pale ambapo chanjo itabisha hodi kwenye kila nyumba na kila mlango wa kila chumba kwenye dunia hii na kupokelewa kwa mikono miwili.
Kwa Zaidi ya milenia kadhaa, vizazi na vizazi vya watu hawa mahususi, wenye malengo na maono hasi dhidi ya ulimwengu wamekuwa wakifanyia kazi hichi ambacho leo chanjo inakaribia kuanza kukikamilisha. Utaona sasa kwenye hili Bill Gates na taasisi yake ni kama mjumbe, kama walivyo pita wajumbe wengine kwenye mpango huu.
Chanjo inakwenda kuwapa, ‘’Hati miliki ya Maisha ya Kila mtu kwenye uso huu wa dunia’’
Suala la kupunguza idadi ya watu duniani kupitia chanjo nalo ni ‘secondary’, lakini lililo la msingi na kuu juu ya yote ni, ‘’Kuyatawalia Maisha ya Kila Mtu, Kila nukta Popote Pale alipo’’
Kama unafikiri bado naota ndoto za alinacha subiri.
Lakini haya yanatoka kwenye midomo yao wenyewe, siwaekei maneno mdomoni, neno kwa neno, kwa miongo kadhaa, taratibu hatua moja baada ya nyingine mpaka hapa tulipo fikishwa.
Bill Gate kwa maneno yake mwenye anasema tunapo takiwa kufika ni kuwatia chanjo watu wote ulimwenguni ndiyo dunia irudi kawaida.
Na wanayo uhakika wa kufanya hivyo, sababu wakati dunia inafikiri Corona imeisha na vitu vianza kurudi kawaida, WHO wanaanza kusema maneno aliyo yasema Gates, kuwa ‘’Secound Wave’’, inakuja, baadhi ya nchi zimeanza maandalizi ya kupambana na Secound Wave ikiwemo Uingereza. Kwamba kwa bunduki au kwa makubaliano hili ni dirisha la fursa kwao, ambalo kabla halijafafungwa lazima malengo yafikiwe na nambari moja kwenye listi ni chanjo kwa dunia nzima.
Yule jamaa aliyemchimba biti Trump kuwa kutakuwa na Surprise Attack, Rafiki wa Gates, naye kasema dunia haiwezi kurusi normal, mpaka kila mtu apokee chanjo.
Kissenger, mmoja wa mitume wa muda mrefu kwenye ajenda hizi, aka the man of one phone call … Nikson alipoanza kujifanya kuwa na yeye ni mchezaji badala ya mchezeshwaji … Kissenger alipiga simu moja tu, na biashara ya Nikson ilikuwa ni historia, mtu aliyo andika tafiti moja maarufu, ‘’Global 2000’’, anakuambia dunia nzima lazima ipigwe chanjo na kisha akaongezea kitu kimoja, ni wakati sasa dunia kuanza kutekeleza miundo mbinu ya kuelekea kwenye … Cashless Society.
Baada unafikiri naota ndoto za machan?
Huzi sikii sasa taasisi za fedha hata hapa nchi zinavyo himiza watu kuelekea kwenye mfumo wa fedha wa kimtandao zaidi? Automatiki mambo yanaanza kujiwekea tiki na baada ya miaka 2, tutakuwa tunaishi kwenye dunia nyingine kabisa, dunia itarudi ‘’Normal””lakini itakuwa ni, “’New Normal”
Waziri Mkuu wa Australia anasema, dunia haitarudi kuwa “normal’’, mpaka hapo patakapo kuwa na chanjo.
Johson & Johson washirika muhimu kwenye ‘’Event 201”, wanasema wanajiandaa kusambaza Chanjo dunia nzima.
Denmark inapitisha sharia, sijui kama imepita ama la, sharia mahususi ya dharura ya kupambana na Coronavirus, ambayo inamtaka kila mwananchi apokee chanjo.
Italy imekwenda mbali Zaidi, lakini ndiko ambako dunia nzima inatakiwa iende, kuwa ili urudi kazini lazima uwe na ‘’alama’’ inayo onesha kuwa unayo kinga dhidi ya Corona Virus. Punde nitalizungumza hili kwa kina.
Bill Gate anayo mradi unao itwa 2020 Global ID, Bill Gate akasema ili dunia irudi kama kawaida lazima watu wapewe vitambulisho vya kielectronic ambavyo vitaonesha kuwa wapo salama, kuw awamepokea chanjo.
Ndiyo maana nasema chanjo kutumika kupunguza idadi ya watu hilo ni, ‘’secondary’’, Bill Gate anasema tukufanya kazi nzuri kwenye chanjo tutapunguza asilimia kadhaa ya idadi ya watu, lakini mimi nasema hili la idadi ya watu ni secondary, la msingi nambari moja ni hii Global ID.
Huwezi kuwatawala watu ambao huwatambui, huwezi kuwatawala watu ambao huwamiliki, hata kama utapunguza idadi ya watu duniani kama huwatambui ni kazi bure. Hivyo la msingi na nambari moja ni kuhakikisha kuwa kila mwanachi, na sasa itaitwa, ‘’Global Citezen’’, lazima awe na kitambulisho, tena cha kielektroniksi, wala hatambei nacho mfukoni kama ilivyo simu au hizi passport za kielektroniksi, hapana kitakuwa chini ya ngozi yake, kifupi ndani ya mwili wake.
Knight Templar, moja ya sasi za sirikwenye muungano huu wa kishetani, karne kadhaa nyuma, walikuwa wanayo ramani ambayo Ulaya ilionekana nan chi moja, haina mipaka. Watu waliwacheka na kuwashangaa. Lakini matokeo yake karibuni tukaona Umoja wa Ulaya umeundwa, mpaka sasa Pamoja na kasoro nyingi lakini mwanachi wa nchi yoyote kwenye Umoja wa Ulaya Maisha yao ni kama mipaka baina ya nchi nan chi haipo, hasa unapo tizama sera zao za uhamiaji, biashara, uchumi, sharia n.k
Lakini wakati Knight Templar wakionesha ramani hizo, kuliwa na maneno yakisemwa dunia ya baadae itakuwa hivyo, hicho kilikuwa kicheko zaidi kushinda ile dhana ya Umoja wa Ulaya, leo tuko hapa, tunafanya maandalizi ya Global ID, na msemo unao anza kushika kasi kwenye vyombo vya Habari ni Global Citizen, bado unayo pumzi za kuwacheka Kinght Templar, au unapaswa kujicheka mwenyewe?
Moja ya Global ID inayo pendekezwa na inayo tajwa sana kwa sasa, ni Tattoo, ‘’Quantum-dot tattoos, tunajua kwenye mafundisho ya baadhi ya dini, kama ya Kiislam Tattoo ni haram una haifai. Lakini ukiachilia nia ovu iliyo nyuma ya kitambulisho hicho cha kiduani, nakuambia subiri uone viongozi wetu wa kidini watakvyo kuja na fatwaa za kuhalalisha Tattoo hizo, kama ambayo wengi walivyo kimbilia kusema, Corona Virus inaonesha jinsi gani Mola alivyo na nguvu … unayo uhakika wewe kuwa hii kitu ni kazi ya Mola Mtukufu dhidi ya waja wake?
Kwenye hii ’Quantum-dot tattoos’’ Gates kama mwaga mpunga akishirikiana na MiT kutengeneza hii teknolojia ambayo itaweka kumbukumbu ya chanjo, wakati imetolewa na taarifa hizo zinaweza kusomwa kuwa kutumia skana kwenye simu janja. Hii si microchip, lakini kazi inayo fanya ni saw ana microchip, hivyo tuko palepale.
Hii Tattoo itaambatana na chanjo, ikiwa itapitishwa kwamba itumike hii, sababu wanazo aina nyingi ya zana zinazo weza kufanya kazi hii ya kufuatilia watu. Sababu kile kinacho sema ni kuwa baada ya mtu kupewa chanjo lazima kwanza atambulike kuwa huyu ni mtu salama, ni safi anayo kinga, au kwa lugha ya karibu miongo miwili sasa, huyu mtu si gaidi.
Kisha baada ya kumtambua kuwa si gaidi—samahani baada ya kumtambua kuwa yeye hafugi virusi vya maangamizi vinavyo itwa Corona sababu anayo chanjo, sasa tunapaswa kufuatilia kila hatua yake ya Maisha isije akawa anakutana na watu wenye virusi hivyo kisha kurudi kuambukiza tena wengine.
Sasa hapo kwenye kufuatilia, ndipo tunapo pataka, na kwa ajili ya hili tulisha tengeneza ina nyingi sana ya vifaa na teknolojia ya kufanya hivyo, na tumesha fanya majaribio ya kutosha, na sasa lazima tuchague moja mahususi kwa ajili ya wote, “One Ring to Rule Them All”, huenda hiyo ringi ikawa ni hii chanjo inayo ambatana na ina Fulani ya alama kama tattoo, ambayo hiyo sasa ndiyo ID yenyewe.
Kwanini nasema hii ID, ndiyo nambari One na chanjo ni kisingizio?
Sababu kwenye hiyo Global ID, iwe Tattoo ID, au nyingine yoyote watakayo tumia, hapatakuwa na rikodi za chanjo pekee yake, bali rikodi za maisha yako yote. Unaishi wapi, unafanya shughuli gani, kipato chako ni kiasi gani, unatumia wapi fedha zako, lini ulienda hospitali mara ya mwisho, umewahi kwenda jela, kusimamishwa mahakamani …. Marafiki zako ni akina nani, ni mambo gani unafanya ukiwa unayo muda wa ziada … aina gani ya maradhi unayo … ukitaka kununua … ukitaka kuuza … leseni yako ya gari … hati ya kusafiiri … Kila kitu maisha yako yote … A to Z kitafungamanishwa na GLOBAL ID.
Na nina kuambia, wale ambao wananchi wanawaamini, kuwatumainia wakiwemo wanasiasa na viongozi wa dini ndiyo watakuwa mstari wa mbele kwenda kupokea chanjo hiyo na kuwahimiza wafuasi na waumini wao kufanya the same.
Hivyo kuna vitu viwili hapa, kuna chanjo, ambayo inayo malengo yake, na moja wapo huenda ni kupunguza idadi ya watu duniani, halafu kunayo global ID, nav yote viwili hivi vinakwenda kwa Pamoja.
Taratibu dunia itafunguka, lakini itakuwa ni, ‘’New Normal’’, mipaka itakuwepo lakini itakuwa tofauti na sasa. Hutasafiri bila aina hii mpya ya kitambulisho, ambayo kisingizio chake kikubwa ni je umepata chanjo, tutajuaje kama umepata chanjo, tutaskani hiyo DigitaL ID, hati yako ya kusafiria yenyewe itakuwepo ndani ya hiyo ID, manunuzi utakayo fanya sasa taarifa zake zitakuwepo humo, kuna maeneo ambayo watu watapigwa marufuku wasiende, kunanachi ambazo watu wataambiwa wasiende sababu ya kitisho cha Corona. Tunakumbuka wakati wa 9/11 majirani zetu Kenya walivyo kuwa wakitajwa vibaya sababu ya ugaidi na kuathiri uchumi wao, tutegemee hadithi kama hizo lakini safari hii ni Corona Virus.
Ukisikiliza mazungumzo kwenye “Event 201”, kuna mahala wanashauri kutumika kwa , “Soft Power” ili kuzishurutisha nchi zinazo kuwa kikwazo kwenye vita hivi. Nadhani hapo tutakuwa tunataja vikwazo vya kiuchumi, tunataja kuwanyima watu kutoka nchi hiyo kuingia nchi zingine au kuwataja ni watu hatarishi kwenda nchi nyingine nk. Haya yote yatafanyika kwa jina la CHANJO.
... To be continued Inshallah ....
ZILIZO TANGULIA
: Corona Virus; New 9/11 (Kumekucha)Prt 1
: Corona Virus; New 9/11 (Global Respond)Prt 2
: Corona Virus; New 9/11 (P+R=S)Prt 3
:Corona Virus; New 9/11 (Gates Man of the Show)Prt 4