Corona Virus; New 9/11 (Global Respond)Prt 2

Salim A. Msangi

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2011
Posts
566
Reaction score
511
Kuna kile kilichoitwa ‘Event 201’, Bill Gates kama kawaida alikuwepo kama mdhamini, mara hii akishirikiana na World Economic Forum, ‘event’ hiyo ilijikita kwenye kuzungumzia uwezekano wa kuibuka baa la maradhi ya kuambukiza litakalo weza kuuwa watu kwa idadi kubwa na kwa muda mfupi. Mpaka jina la virusi hao lilikuwepo, Coronavirus, na hiyo ni Octoba 2019. Hapa ni miezi miwili kabla ya janga lenyewe kutokea.

Mwenendo huu ulitumika sana kabla na baada ya 9/11, kila tukio kubwa tulilo lishuhudia wakati wa vita vya ugaidi, kila ukiunganisha doti, unakutana na hadithi kama hizi za ‘Event 201’.

Kama mtu yoyote yule hakuweza kutambua kujua nini hasa maana ya vita dhidi ya ugaidi, na nani walikuwa walengwa … na hapa niweke wazi, kuna watu wanadhani kuwa waislam ndiyo walikuwa walengwa … hapana bali waislama na uislam walitumika kama ‘means to an end’, walengwa walikuwa ni walimwengu wote, dunia yote, na mifumo yao ya kiuchumi, kijamii, kidini. Kiutamadunia, kiutawala nk.

Sasa ikiwa mpaka muda huo, tunoa elekea kufunga mafaili ya ‘vita ya ugadi’ na kuyatupilia kwenye makabati ya historia na wewe mlengwa hujaelewa ni nini hasa kilitokea, au malengo yake mapana yalikuwa ni yapi … ni vipi basi utalielewa hili la Covid-19?

Walipo kuja kukanusha kuhusu ‘Event 201’, kuhusushwa na utabiri wa Conovirus, walisema kuwa walitengeneza ‘Conovirus’ isiyo halisi ili waone, endapo itatokea ‘Conovirus’ ya ukweli dunia itajibu vipi, itapambana vipi. Hivyo wanakubali kuzungumzia jambo hilo, ila kwenye kiwango cha nadharia na siyo halisi.

Lakini subiri kidogo …

Wakati minara ile miwili ikidondoshwa na ndege za ‘magaidi’, vitengo mbalimbali vya kijeshi na ulinzi vya Marekani vilichelewa kujibu mashambalizi kwa sababu, asubuhi hiyo, kulikuwa na zoezi la mashambulizi kwenye minara hiyo, ambapo mazoezi hayo yalilenga kuangalia endapo minara hiyo itashambuliwa vitengo vya ulinzi vitajibu vipi mashambulizi. Kama ambavyo ‘Event 201’, ilivyo fanya endapo kirusi kikitokea dunia itajibu vipi mapigo. Minara ikadunguliwa na ‘magaidi’, vitengo vya ulinzi vikawa vimepigwa ganzi, sababu hawajui kinacho endelea ni mazoezi au ndiyo kazi imeanza? (Michael Kane: "9/11 War Games? No Coincidence" http://911review.org/brad.com/batcave/WarGames.html.)

Is it coincidence again, kwamba taasisi nyeti ya afya, kama ilivyokuwa NORAD (North American Aerospace Defence Command), taasisi nyeti ya ulinzi wa anga, zote kufanya mazoezi ya ‘nadharia’ juu ya kutokea janga fulani … halafu haichukui muda janga husika kama lilivyo kuwa kwenye nadharia linatokea kwa ukamilifu wake kwenye maisha halisi bila kupungua hata nukta?

9/11 moja ya kazi kubwa iliyo kuja kuifanya ni kuilinda ‘Petrol Dollar’, ambayo ilikuwa inatishiwa na aina ya watu kama akina Saddam na Ghedaffi ambao walijihisi wana mamlaka ya kuamua mafuta yao wauze kwa saraffu gani na pesa yake waifanyie nini. Mashariki ya kati yote imeenda kutulizwa, na walau kwa miaka michache ‘Dollar’ itaendelea kunguruma kwenye safe za ‘Reserve Currency’, na mafuta yakibaki kama injini yake. Dunia ilisogezwa kwa pamoja na kuambia zimwi hili linalo itwa ‘ugaidi’ haliwezi kuuwawa na nchi moja peke yake, lazima dunia ishirikiane. Sheria mbali mbali zikabadilisha, uhuru wa watu ukaporwa, mali zikaporwa, nchi zikatengwa na kuvamiwa kwa jina la ‘Ugaidi.’

Kama vita dhidi ya Ugaidi ilikuwa ni fimbo dhidi ya ulimwengu, Covid-19 tutegemee kuwa mbaya zaidi, sababu safari hii, siyo nchi ila mwili wako. Safari hii hawatumi vibaraka wao (vikundi vya kigaidi), bali wanatuma ‘Microbe’, kwa maneno yake Bill mwenyewe. Ikiwa mwili wako sasa utaonekana ni ki kwazo kwa shule kufunguliwa, watu kusafiri, uchumi kukua, sababu inahifadhi magaidi wanao itwa Covid-19, unafikiri tutakufanyaje kwa jina la Covid-19?

Am just think na kuota ndoto za machana.

Kwanza tuangalie watu tuliyo wapa mamlaka ya kidunia, wana tushauri tufanye nini dhidi ya Covid-19.

Lakini kabla ya kuwauliza tufanye nini kuhusiana na Covid-19, tusikilize walivyo kuwa wakitushauri endapo tutakumbana na aina hii ya majanga.

Papa Benedict alisema;

“Walimwengu walio ungana wataweza kuyashinda matatizo mengi yanayo isumbua duni hivi sasa kutoka kwenye kitisho cha ugaidi mpaka kwenye umasikini ulio kithiri ambao wanaishi mamilioni ya watu, kutoka kwenye ongezeko la uzalishaji wa silaha mpaka kwenye uharibifu wa mazingira unao tishia kuiharibu sayari yetu. Usiogope, weka imani yako kwake! Yeye aliye nuru na nguvu na mwenye uwezo wa kujenga New World Order …( Pope Benedict Calls for a New World Order. http://www.infowars.com/articles/nwo/benedict_calls_for_nwo.htm)

Strobe Talbott makamu katibu mkuu wa nchi katika utawala wa Clinton kutoka 1994 mpaka 2001, mwanachama wa Council on Foreign Relation (CFR), na Trilateral Commission (TC). Mwaka 1992 aliandika makala kwenye Time Magazine yenye jina la ‘Kuzaliwa kwa Taifa la Dunia’, kwenye makala hiyo aliandika kuwa miaka 100 inayo kuja kuwa, Utaifa kama tunavyo ufahamu utatoweka; nchi zote duniani zitaitambua serikali moja tu. Msemo ambao ulitengenezwa katikati ya karne ya 20 -‘citizen of the world’- utakuwa na maana kamilifu mwishoni mwa karne ya 21.( Strobe Talbott, America Abroad. Time Magazine: July 20, 1992: http://www.time.com/time/magazine/article/0,9171,976015,00.html )

Zaidi ya hapo akaendelea kusema,

“Utandawazi umepelekea kuwepo na kusambaa kwa ugaidi, tatizo la dawa za kulevyea, Ukimwi na uharibifu wa mazingira. Lakini kwa vile matatizo hayo ni makubwa kiasi hakuna nchi kama nchi inayoweza kusimama yenyewe na kuyakabili inabidi uhitajio wa mfumo wa kimataifa kukabiliana na matatizo hayo unaoneka wazi”( Strobe Talbott, America Abroad. Time Magazine: July 20, 1992: http://www.time.com/time/magazine/article/0,9171,976015,00.html )

Gideon Rachman, aliandika hivi,

“Matatizo mengi na makubwa yanayo zikabili serikali za kitaifa ni matatizo ambayo asili yake ni yale ya kimataifa; kuna ongezeko la joto duniani, kuna anguko la uchumi wa kidunia, na pia kuna vita vya dunia dhidi ya ugaidi. Tulicho kiona kwenye Umoja wa Ulaya kitakwenda dunia nzima na serikali ya dunia itawezekana. Anguko la kiuchumi la dunia na ongezeko la joto duniani yanaisukuma serikali ya kitaifa kutafuta suluhisho lake kimataifa.”( Gideon Rachman, And now for a world government. The Financial Times: December 8, 2008: Subscribe to read | Financial Times )

Novemba mwaka 2008, United State National Inteligence Council (NIC), Kituo kwa ajili ya mipango ya kistratejia ya muda mrefu na mfupi kwa taifa la Marekani kilitoa ripoti ambayo kupatikana kwake kulihusisha vitengo vingine kadhaa vya mipango ya kistratejia kama makampuni yanayo toa huduma za ushauri na upangaji wa sera, vitengo vya elimu, mamia ya wataalamu pamoja na taasisi kama vile Atlantic Council of the United States, Wilson Centre, RAND Corporation, Brookings Institution, American Enterprise Institute, Texas A&M University, Council on Foreign Relations na Chatham House kutoka London.

Ripoti hiyo ilikuwa na haya ya kusema kuhusiana na suala la ujio wa serikali ya dunia;

“Mpaka kufika mwaka 2025 serikali za umoja wa kitaifa hazitakuwa peke yake na hasa hazitakuwa na umuhimu kwenye jukwaa la dunia la mfumo wa kimataifa, matatizo ambayo yanatusukuma (tuende kwenye serikali moja) ni mabadiliko ya hali ya hewa (ongezeko la joto duniani) sharia mpya za masoko ya kidunia na uchumi, uhamiaji, mitandao ya uhalifu n.k. matatizo haya hayawezi kutatulika kwa kiwango cha kitaifa. Haja ya kuwa na serikali ya dunia itakuwa kwa kasi zaidi kushinda vile ambavyo mazingira yanavyoweza kutuletea.”( NIC, Global Trends 2025: A Transformed World. The National Intelligence Council’s 2025 Project: November, 2008: Acknowledgements: http://www.dni.gov/nic/NIC_2025_project.html )

Rais wa 40 wa taifa la Marekani, Ronald Reagan mara kwa mara amekuwa akizungumzia ni namna gani dunia nzima itaweza kuungana endapo patakuwepo na kitisho cha ulimwengu.

Kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mwaka 1987, Septemba 21 alisema;

“Katika hali yetu kubwa ya chuki na utengano tuliyo nayo hivi sasa, mara kwa mara tunasahau ni kiasi gani binaadam tumeungana. Huenda tunahitaji kitu kutoka nje, kitisho cha ulimwengu kitakacho tufanya sisi kuweza kutambua umoja huu tulio nao. Nimekuwa nikifikiria ni namna gani tofauti zetu zitatoweka pale ambapo tutakuwa tunapambana na kitisho cha kiulimwengu kutoka nje ya sayari yetu”. ( Ronald Reagan - The Alien Thread - Speech to the United Nations General Assembly, 42nd General Assembly on September 21, 1987)

Mwaka 1988 Mei 5, White House, kwenye chumba kilicho jaa waandishi wa habari, Reagan alisema,

“Nimekuwa nikijiuliza mwenyewe kwamba itakuwaje kama sisi sote hapa duniani tukagundua ya kuwa kuna kitisho dhidi yetu kutoka nje ya dunia yetu … nguvu ya kutoka kwenye sayari nyingine. Je si mara moja tu tutaweza kutambua kuwa hatuna tofauti yoyote baina yetu, kwamba wote tu binadamu, wananchi wa dunia na je, hatutaungana kupambana na kitisho hicho?”

Henry Kissinger Kwenye mkutano wa Bilderberger, Evians, Ufaransa mwaka 1992 alisema,

“Leo hii Marekani itakasirishwa endapo Umoja wa Mataifa utaingia Los Angeles kutuliza amani. Lakini kesho watafurahia kitu hicho! Hii ni kweli hasa endapo wataambiwa kuna kitisho kutoka nje ya sayari yetu kinacho tishia uhai wetu. Itakuwa hivyo kwa watu wote wa dunia ambapo wataomba msaada wa kupambana na kitisho hicho. Kitu kimoja ambacho kila mtu anakiogopa ni kile ambacho hakifahamiki. Walimwengu watakapo letewa kitisho hicho, haki zao za msingi wataziachia na kuzikabidhi kwa serikali ya dunia ambayo itawahakikishia usalama wao.” ( Former Secretary of State Henry Kissinger, address to the Bilderberger organization meeting in Evian, France (May 21st 1992). The Council on Foreign Relations (CFR) excerpted from the book The Bilderberg Group by Daniel Estulin)

Kwa uchache sanaa, nukuu hizo za watu wakubwa duniani, kwa nyakati tofauti, mbele ya vyombo vya habari, majukwaa ya kisiasa na taasisi, wamekuwa wakitarajia kuwepo kwa muungano wa kidunia ambao utazaliwa kwenye majivu ya kitisho cha kiulimwengu. Eidha ni kitisho cha Ugaidi, Mzingira kama ongezeko la joto duniani, uhalifu, uchumi n.k

Kuanzia WWI, WWII, anguko kubwa la kiuchumi soluhisho lake lilipelekea kuundwa kwa vyombo vyenye mamlaka ya kidunia ili kudhibiti majanga hayo yasijirudie. Tumeona dunia nzima ilivyo unganishwa na kushirkishwa kwenye vita dhidi ya Ugaidi ... unapo unganisha doti hizo ni vipi nikushangae kama utaiyona Covid-19 ni 9/11 nyingine?

Kama tulikuwa tunasubiria kitisho cha kidunia, ili kuweza kuifunga dunia barabara sambamba na malengo yetu, je kuna kinacho tupa sababu ya kufanya hivyo kama Covid-19? Je hii ni lifti tunaidandia kuelekea kwenye malengo yetu kusimamisha serikali ya dunia, au ni gari tulilo litengeneza kufanya hivyo? Je ajenda inapiga hatua nyingine ya muhimu au tupo kwenye majaribio ya kuona njia ipi itafaa kutekeleza malengo yetu?

Ngoja viongozi wa kidunia waje watujibu hapa maswali yetu.

‘A Global Challenge Needs a Global Response’ Hicho ni kicho cha habari kwenye makala iliyoandikwa na Bernhard Zand, Machi 19, 2020.

Zand anasema, ‘Hakuna yoyote atakaye weza kuiokoa dunia kwenye janga lilipo peke yake. ... Covid-19 kila uchao inaweka wazi madhara yake. Kwenye janga kama hili, aina fulani ya serikali ya kidunia inatakiwa, ... Janga hili linahitaji mawasiliano na mashirikiano yanayo vuka mipaka ya kitaifa na hata ya ki mabara... Hakuna yoyote anayeweza kutatua tatizo hili peke yake. Siyo China ... Siyo Marekani ... Wala siyo Yuropa ... Social distance ni tiba ya janga hilo kwenye kiwango cha mtu mmoja mmoja, lakini kwenye kiwango cha kimataifa tunahitaji muungano wa kidunia.”

Aliyekuwa waziri mkuu wa Uingereza, Gordon Brown wakati wa mtikisiko wa kiuchumi wa mwaka 2009, alisisitiza haja ya kuwa na , New World Order Goverment, kama njia ya kutengua tatizo hilo na kuweka mikakati ya kutojirudia. Hiyo ni mwaka 2009, leo anasemaje kwenye Covid-19?

Gazeti la The Guardian, Machi 26, limerusha ripoti ambayo inasema, Gordon Brown, anaitaka kuundwa kwa serikali ya kidunia kupambana na Coronavirus. Kwa mujibu wa makala hayo, Gordon Brown anawataka viongozi wa dunia kutengeneza ‘Serikali ya Dharura ya Dunia’ kupambana na janga hili la Covid-19. Nchi moja peke yake haiwezi kupambana na janga hili.’

Henry Kissenger, Globalist mwenyewe, tumsikilize anatuambiaje kwenye hili.

Kissenger.jpg

Apr 3, 2020, kwenye gazeti la Wall St Journal aliandika makala iliyo kwenda kwa jina la, ‘The Coronavirus Pandemic will forever Alter the World Order.’ Kwenye Makala hiyo ndefu baadhi ya mambo aliyozungumzia ni kama ifuatavyo, ‘... Wakati janga hili la Covid-19 likifikia mwisho, nchi nyingi, taasisi zitahesabika kuwa zime feli. ... Ukweli ni kuwa dunia haitakuwa kama awali baada ya Covid-19. Viongozi wa kidunia wanapambana na janga hili kwenye kiwango cha kitaifa ... lakini madhara ya janga hili haya tambui mipaka. Hali za kiafya na madhara yake kwa waathirika yanaweza kuwa ya muda mfupi, lakini mabadiliko ya kiuchumi na kisiasa yatadumu vizazi na vizazi. Hakuna nchi, hata Marekani kwamba itaweza kutatua tatizo hilo pekee yake bila mashirikiano ya kimataifa...’ Makala ni ndefu lakini msisitizo ukiwa ni janga hili lazima liilete mashirikiano ya kidunia pamoja, ni kama tume pata sababu ya kutokea, hii ni fursa ya kubadilisha sura ya dunia kiuchumi na kisiasa milele. Na ikiwa viongozi wa kidunia wakiendelea kujitenga kwenye kuliendea janga hili, basi dunia itawaka moto.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, anassema; ‘Mahusiano baina ya mataifa makubwa hayajapata kuwa dhaifu na hafifu. Covid-19 ina tuonesha kwa kasi kubwa, kwamba lazima tuungane pamoja … au tutashindwa kwenye vita hivi.’

Jarida kubwa la kimtandao, TRT World, limekuja na makala ndefu inayo bebwa na kichwa cha habari, “We Must invent a new world order now to stop Covid-19’.

Makala hiyo imechambua kwa kina haja ya kuwa na Serikali ya dunia katika kipindi hichi cha Covid-19 kuliko kipindi chochote katika historia.

... To be continued Inshallah ....
ILIYO TANGULIA : Corona Virus; New 9/11 (Kumekucha)Prt 1
 
Mbona katika quotes zote sijaona tatizo? ktk dhoruba si vibaya kuungana kupambana na dhoruba hyo as long as inaleta athari kwetu sote.
 
Asante kwa makala nzuri,Aisee,nini kimefichwa kwenye hiyo new world order? Je sisi km sisi tutanufaika au kuna hasara zaidi ya faida?
 
Tiririka na posti zote mpaka mwisho utakuwa na majibu.
 
Mbona katika quotes zote sijaona tatizo? ktk dhoruba si vibaya kuungana kupambana na dhoruba hyo as long as inaleta athari kwetu sote.
Ukitaka naweza kukuwekea link ya mada ambazo utaelewa kwa urahisi na kuona kitu.
 
View attachment 1465354

Apr 3, 2020, kwenye gazeti la Wall St Journal aliandika makala iliyo kwenda kwa jina la, ‘The Coronavirus Pandemic will forever Alter the World Order.’ Kwenye Makala hiyo ndefu baadhi ya mambo aliyozungumzia ni kama ifuatavyo, ‘... Wakati janga hili la Covid-19 likifikia mwisho, nchi nyingi, taasisi zitahesabika kuwa zime feli. ... Ukweli ni kuwa dunia haitakuwa kama awali baada ya Covid-19. Viongozi wa kidunia wanapambana na janga hili kwenye kiwango cha kitaifa ... lakini madhara ya janga hili haya tambui mipaka. Hali za kiafya na madhara yake kwa waathirika yanaweza kuwa ya muda mfupi, lakini mabadiliko ya kiuchumi na kisiasa yatadumu vizazi na vizazi. Hakuna nchi, hata Marekani kwamba itaweza kutatua tatizo hilo pekee yake bila mashirikiano ya kimataifa...’ Makala ni ndefu lakini msisitizo ukiwa ni janga hili lazima liilete mashirikiano ya kidunia pamoja, ni kama tume pata sababu ya kutokea, hii ni fursa ya kubadilisha sura ya dunia kiuchumi na kisiasa milele. Na ikiwa viongozi wa kidunia wakiendelea kujitenga kwenye kuliendea janga hili, basi dunia itawaka moto.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, anassema; ‘Mahusiano baina ya mataifa makubwa hayajapata kuwa dhaifu na hafifu. Covid-19 ina tuonesha kwa kasi kubwa, kwamba lazima tuungane pamoja … au tutashindwa kwenye vita hivi.’

Jarida kubwa la kimtandao, TRT World, limekuja na makala ndefu inayo bebwa na kichwa cha habari, “We Must invent a new world order now to stop Covid-19’.

Makala hiyo imechambua kwa kina haja ya kuwa na Serikali ya dunia katika kipindi hichi cha Covid-19 kuliko kipindi chochote katika historia.

... To be continued Inshallah ....
ILIYO TANGULIA : Corona Virus; New 9/11 (Kumekucha)Prt 1
Safi sana mkuu,
 
Ahsante Salim Msangi. Nimefuatilia sana suala hili kutoka kwa wabobezi wanaoguswa na mikakati hii duniani. Maswali ni mengi. Nikushukuru kwa kuliandikia jambo hili kwa Kiswahili. Ubarikiwe sana.
 
Back
Top Bottom