Corona Virus; New 9/11 (P+R=S)Prt 3

Corona Virus; New 9/11 (P+R=S)Prt 3

Salim A. Msangi

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2011
Posts
566
Reaction score
511
Problem + Reaction = Solution. (P+R=S)

Formula hii imetumika sana kwenye majukwaa ya kisiasa, kitaifa na kimataifa, toka enzi za WWI na hata kurudi nyuma mpaka hivi karibuni kwenye 9/11 na yaliyo fuata baada ya hapo. Ukionganisha nukta za maelezo ya wana Globalist kabla ya janga hili, na sasa tukiwa kwenye janga hili, ni kama tupo kwenye aina nyingine ya PRS.

Je janga hili limetengenezwa makusudi, ili kutegemea Reaction ambayo itahitaji Solution ambayo tayari ilisha andaliwa?
Hapana tusihukumu haraka kiasi hicho, hebu kwanza tuangalie tunacho kiona ndicho ama kuna ambacho hatukioni.



Kwanza nisieleweke vibaya, sisemi kuwa hakuna Covid-19, si semi kuwa Covid-19 haisababishi vifo, au kuuwa kabisa, hapana. Sisemi kuwa tusichukue tahadhari juu ya Covid-19, hapana. Sisemi kuwa watu wasifuate maelekezo ya wataalam wa afya dhidi ya kujikinga na Covid-19, Hapana. Bali nasema kuna janga linaitwa Covid-19, na ni hatari kwa namna mbalimbali, na tahadhari lazima zichukuliwe kama zinavyo tolewa na wataalam wa afya.

Aina hii ya janga, litazame kwenye miwani ya 9/11. Minara miwili iliporomoshwa ndiyo, watu walikufa, vikundi fulani fulani visivyo na mipaka viliingia kila kona ya dunia kutekeleza mashambulizi ya kigaidi. Dunia ikagawanya sehemu mbili, ‘Either your with us, or with the Terrorist’ hapakuwa na ‘neutral ground’, lakini mwisho wa yote tulijua huo siyo ukweli wote. Tulijua wanao itwa magaidi na wanao pigana na magaidi lao ni moja, na mwisho wa siku ... wewe ndiye ulikuwa gaidi, sababu sheria, kanuni taratibu zilizo badilishwa kwa ajili ya kukabiliana na magaidi hazi kuwaathiri magaidi zaidi, kama zilivyo kuathiri wewe.

Covid-19, Je tunapishwa kwenye aina nyingine ya 9/11?

911.jpg


Bado tunalitazama hili kupitia miwani ya 9/11, sababu imebeba vionjo na ladha kadha wa kadha za 9/11, na hata wapishi kwa mbaaaaali wanaonekana ni wale wale walio pika 9/11.

Wakati wa 9/11 propaganda zilipaa, ‘maneno yalikuwa ni makali kushinda upanga’, vyombo vya habari kote ulimwenguni maneno na habari zao ziliwafanya watu wa dini fulani kubadilishwa jina na kuitwa magaidi, na dini yao iliitwa dini ya magaidi, maneno yao yalikata kama upanga, data zikapikwa na kupakuliwa, nchi zikavamiwa na viongozi kupinduliwa ... na dunia nzima ikibariki, sababu ‘maneno yalikuwa ni makali kushinda upanga’.

Here we go again ...

Hivyo sasa, mara hii tutaona namna vyombo vya habari vikavyo endelea kulipaisha janga hili, na kutengenza zimwi kutoka hewani litakalo kula uchumi na maisha ya watu. Sijasema Covid-19 haipo, hapana, sijasema kuwa Covid-19 haisababishi kifo, hapana. Lakini namna vyombo vya habari vinavyo liendea jambo hili kuna zua maswali hata kwa wataalam wa afya.

Haijawi katika historia ya dunia kuwa na hamasa ya kuwepo kwa chanjo dunia nzima kwa kila binadama kama ilivyo sasa. Haijawahi kwenye uso wa dunia kuwa na hamasa ya ‘global Lockdown’, kama tunavyo iyona sasa. Kelele za mashirikiano ya kidunia ndiyo kwanza zinaanza ... na siku zinavyo zidi kwenda mbele picha ya haja kwa nini dunia iungane itazidi kuwa wazi.

Swali ni Je!

Safari hii kuna nchi zitavamiwa sababu ya Covid-19?

Kuna serikali zitapinduliwa kwa sababu ya Covid-19?

Kuna nchi zitaekewa vikwazwo vya kiuchumi kwa sababu ya Covid-19?

BUSH.jpg


Time will tell

Lakini je kama dunia nzima kupitia WHO na taasisi zingine za kiafya kidunia, kiuchumi, kiusalama zikaona nchi yako inashirikiana na magaidi wanao itwa Covid-19, nchi yako haitaki kufanya vile mabwana wakubwa wanataka dhidi ya gaidi mpya anayeitwa Covid-19, hivyo unahatarisha uhai wa wananchi wako, unaendelea kuvifanya vita dhidi ya adui huyu kuwa vigumu kwa kutoruhusu Lockdown, au chanjo kwa wanachi wako, ua hutaki wataalam wa kimataifa waje kukukagua kama unamiliki silaha mpya za maangamizi zinazo itwa Corona ... bila kusahu nchi yako ipo kwenye strategic position labda una madini ya kutosha, mafuta au vingine vizuri tunavyo vitamani ... vp hapo, si ndiyo mwanzo wa Iraq au Libya nyingine?

In the name of Covid-19 dunia inakwenda kubadilika, na ajenda inapigishwa hatua nyingine kubwa na ya muhimu.



Tunapo onganisha doti, kwenye aina hii ya matukio, na kulinganisha na kile ambacho vyombo vya habari ulimwengu mzima vinavyo tuambia, tukaongezea na kile tunacho ambiwa na taasisi mbalimbali za kitaifa na kimataifa juu ya aina hii ya matukio au majanga, tukawasilikila za baddhi ya viongozi wa kitaifa na kimataifa wanacho sema … ni kama kila kitu hamna kilicho kaa mahali pake, maswali yaasiyo jibika, mtiiririko wa matukio kabla ya janga kutokea, na matukio baada ya jnga, maoni ya mabwana wakubwa juu ya suluhisho ya janga hili yote haya yanaacha uwazi mkubwa ambao unashadidia wachambuzi huru kutazama aina hii ya mwenendo wa matukio haya kwa jicho tofauti na wanalo tizama watu wa kawaida.

Ni kama kuna yanayo fanyika mbele ya pazia kwa kila mtu kuona, na kuna ambayo yanafanywa nyuma ya pazia yanayo onekana na wachache mahususi, lakini yakiwa na athari kwa walimwengu wote.

Kwa wasomaji wangu wa muda mrefu watakuwa wameelewa nazungumzia nini … kwa wale wapya … soon tutaelewana.

Kumekuwa na mpango wa muda mrefu … muda mrefu hasa, mpango wa zaidi ya milenia moja wenye lengo la kuwafunga walimwengu wote chini ya aina moja ya utawala, utawala wa kidunia. Tunapo zungumizia aina hii ya utawala na kitisho chake kwa walimwengu ndipo suala la ‘ukitaka kumuuwa mbwa; mpe jina baya’ … linapokuja…’ conspiracy theorist.

Lakini kwa sababu mpango huu upo, na wahusika kwa nyakati tofauti, tangu zama hizo wamekuwa wakikiri juu ya kuwepo kwa mpango huo, n ahata mpaka sasa wanakiri na wanaufanyia kazi, na kwa vile tunayo picha ya namna unavyo tekelezwa hatua kwa hatua, mpaka nukta ya mwisho … aina hii ya majanga yanapokuja kuweka alama ya vema kwenye hatua za kuelekea kwenye serikali ya kidunia … unawezaje kusema tofauti?

9/11 tulisema ni moja ya majanga yaliyo kuja kuipigisha ajenda hatua nyingine kuelekea kwenye lengo kamili. Haikujalisha nani kalipua minara ile, ingawa iko wazi kama tofauti ya mchana na usiku kuwa si Osama Bin Laden aliyefanya kazi ile. Lakini mwisho wa siku, imewezesha kile kinacho itwa ‘Geostrategic Regions’ kuwa chini ya vibaraka wanao andaa serikali ya dunia. Tunajua ncho zote ambazo zimevamiwa baada ya 9/11 zipo taabaani kiuchumi na miundo mbinu, na kuingizwa kwenye mtego wa madeni kupitia WB na IMF, ambapo rasilimali zao, ‘Black Gold’, itatumika kulipa kama siyo dhamna ya mikopo hiyo na viongozi wao lazima wawe na baraka kutoka kwa vibaraka wa serikali ya kidunia.

GEO.jpg


Tumemaliza suala la ‘Geopolitical Regions’, vimebaki viporo viwili Iran na Syria … mkakati upo mezani namna ya kumalizia viporo hivyo, sasa tunakwenda hatua nyingine, ajenda inapiga hatua nyingine. Lazima tuiyone ni hatua nyingine sababu ni kitu ambacho kinaleta mabadiliko makubwa ya kidunia na yanayo mgusa mtu mmoja na yanayo kwenda kubadilisha utaratibu wa maisha kwa walimwengu wote.

Unajiuliza janga hili linayo nguvu kiasi gani la kuweza kubadilisha mfumo wa maisha ya kila binadam kwenye uso wa dunia? Hapo ndipo kama binadam upate wasiwasi, kwamba huenda kuna Zaidi ya kile viongozi, wataalam, taasisi na serikali zetu zinavyo tuambia au kutuaminisha.

Kuna mwali kafichwa nyuma ya janga hili, kelele lazima zipigwe ili walimwengu wakubali kumpokea mwali huyu. Kelele za mwanzo na za muda mfupi ni ‘maambukizi na vifo’.

Namba za idadi ya maambukizi na vifo lazima ipazwe, iwe kubwa kiasi kile mtu aone kuwa salama ni ‘lockdown’ na kelele za pili ni uchumi ambazo zitafuatia automatiki.

Linapokuja sula la ‘statiski’ kwa watu hawa mkogano mkubwa na wa makusudi unazaliwa. Tumeshuhudia idadi kubwa ya vifo Italia. Lakini taasisi za afya za Italia zina tupatia hadithi tofauti. Wanasema kuna vifo vya aina mbili kutokan na janga hili. ‘KUFA NA KORONA’ na ‘KUFA KWA KORONA’, Italy wanasema 12% ya vifo vilivyo ripotiwa ndiyo vifo vilivyo sababihwa na Korona, au ‘Kufa kwa Korona’ na waliobakia wote walikuw ana maradhi mengine hivyo si kwamba wamekufa kwa Korona, bali wamekufa na Korona.

Hii si mara ya kwanza aina hii ya takwimu kutumika kulikuza jambo, wakati HIV inapigiwa upatu, mgonjwa akifa na maradhi kumi na HIV ikiwa ni moja wapo, hayo mengine hayoto tajwa bali HIV peke yake. Lengo ni kukuza takwimu za wanao kufa na HIV waonekane ni wengi kuliko uhalisia, HIV moja ya sifa zake ni ‘bigBusiness’, takwimu zikiwa ndogo Business itakufa.

Ikafika mahali WHO ikaongeza magonjwa mengine kama Kifua Kikuu, Magonjwa ya akili na mengine kama 25 hivi, ukifa na moja ya magonjwa hayo, hata kama haukuwa na HIV, utaandikiwa kuwa umekufa kwa HIV, huo ni muongozo kutoka WHO.

Dr. Sherri Tenpenny, mtafiti wa muda mrefu kwenye masuala ya chanjo, na pia mmilikiwa mtandao unao kwenda kwa jina vaxxter.com na muandishi wa kitabu maarufu kinacho kwenda kwa jina la ‘Say No to Vaccine’, anasema kuwa Conovirus siyo kirusi kipya, anasema kunayo aina 36 ya Conovirus inayo julikana na jamii ya wanasayansi wa masuala ya maikrobu. Virusi 7 kati ya hivyo 36 havina madhara kabisa kwa binaadam na virusi 4 kati ya hivyo 7 ni maarufu kwenye ya mafua ya kawaida ambayo mara kwa mara tunakumbana nayo.

Swali linakuja.

Zinapo tolewa takwimu za wagonjwa wa Corona kokote pale ulimwenguni, Je vipimo vinakuwa vimeegemea kwenye aina ipi ya virusi vya Corona?

Swali hili lina turudisha kwenye uatata ule ule unao patikana maabara, pale ambapo mtu anapo pimwa kwa ajili ya HIV.

Kwa hiyo unapo kutana na aina hizi za mikanganyiko ndipo unapo jiuliza swali la msingi kabisa.

Njia hizi zinazo chukuliwa kupambana na janga hili ni sawa?

Zilihitaji kufikia kiwango hiki tunacho ona?

Ni nini kinacho Sukuma dunia nzima kufungiwa ndani?

Lakini wewe ni nani hata uwe na majibu ya maswali haya? Kuna uliowapa mamlaka wa kuamua nini kifanyike na wakati gani, hebu tuwasikilize tafadhali.

Kwahiyo kwenye hii Civid-19, hata ukipata ajali ya gari halafu baadae tukapima tukakuta kuwa ulikuwa na Korona kunayo uwezekano mkubwa wa kuandika kuwa kifo kimesababishwa na Korona na siyo ajali.

Kwanini?

Tunajenga takwimu, takwimu za kukutisha, kama tulivyo jenga hizo takwimu kwenye maradhi mengine, bila kusahau kwenye silaha za maangamizi tukamtoa Saddama, kwenye udikteta tukamtoa Ghadafi, kwenye kushirikiana na magaidi, tukaivamia Syria n.k

Hivyo hapa tutegemee namba ya wahanga wa Covid-19 kupaishwa na mashirika haya na vyombo vyao vya habari bila kujalisha ni halisi ama la, lengo ni kumfanya kila mmoja wetu afunge mdomo, anyamaze na akae ndani kisha bwana wakubwa waje kutuambia nini cha kufanya.

Doti tulizo unganisha kabla ya janga hili kutokea zote zinataja idadi ya vifo kutokea kwa mamilioni, 10, 20, 25 na hata 30. Eidha vifo hivyo vitatokea ama la, eidha vifo hivyo vitakuwa halisi ama la, zao la mwisho ni dunia ijue Covid-19 ni shida, balaa, janga, na halina utani na kila mtu atafekelewa mbali asipo chukua hatua stahiki.

Ni zipi hizo hatua stahiki?

Subiri kidogo, bwana wakubwa watakuja kutuambia soon, kama bado hujazisikia.

Kisha kelele zinaenda kupazwa kwenye uchumi. Wala hapahitaji kelele, kila mtu anaiyona hali, dunia nzima haihitaji kuwa mwana hisabati, biashara zinakwenda kusimama, kuanguka, kujikongoja … not business as usual kila kitu kina kwenda kubadilika kwenye uchumi. Ajira zitafekelewa mbali, biashara zitafungwa na huenda zisirudi uwanjani, kila mtu ndani … kimya.

Uchumi hapa siyo lengo kuu, kama ambavyo usilam hakuwa lengo kuu kwenye 9/11, lakini a means to an end, na ndivyo itakavyo kuwa uchumi kwenye hili. Uchumi utawekwa kwenye sura mbaya lakini zamu yake bado, bado kidogo, nadhani baada ya kufunga mafaili ya Covid-19 sasa ndiyo tutatizama uchumi na mfumo wake wa fedha kwa asilimia mia moja. Joto la uchumi unalo lihisi hivi sasa ni kuwalazimisha walimwengu, serikali, watu mmoja mmoja nk kupaza sauti

‘KORONA INATUHARIBIA UCHUMI’

‘KORONA INAUWA AJIRA’

‘KORONA INAUA BIASHARA ZETU’

‘TU LETEENI TIBA YA KORONA’

‘LETENI CHANJO YA KORONA HATA KWA MKOPO’

‘KORONA IONDOKE!’

IN NEXT.jpg


Hapo ndipo tunapo takiwa kufikishwa, eidha kwa data za kupikwa au za ukweli, eidha kwa kuporomosha uchumi, kupora ajira za watu, kudumaza uchumi nk, lakini hapo ndiyo kituo chetu.

Ikiwa hicho ndicho kituo, na dunia nzima lazima ifikishwe kwenye kituo hicho … basi ujue ‘movie’, ndiyo kwaaaanza inaanza, labda hata majina ya stelingi na maderekta bado
hayajawa-display!

... To be continued Inshallah ....
ILIYO TANGULIA
: Corona Virus; New 9/11 (Kumekucha)Prt 1
: Corona Virus; New 9/11 (Global Respond)Prt 2
 
Back
Top Bottom