#COVID19 Corona Virus: Sehemu za kuepuka, sehemu za kuwa na umakini mkubwa na vitu vya kutumia kwa tahadhari

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Joined
Aug 7, 2018
Posts
685
Reaction score
1,124
NI SEHEMU GANI HATARISHI ZAIDI KWA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA #CORONA?

Sehemu za kuepuka kabisa

Sehemu za starehe kama vilabu na baa, migahawa, nyumba za mazoezi, saluni, sehemu za kuangalia michezo, majumba ya sinema, mikusanyiko ya hadhara na sherehe

Sehemu ambazo inaweza kukulazimu kwenda

Kuwa makini sana ikikulazimu kwenda sehemu hizi: Vituo vya basi, nyumba za ibada, hospitali, usafiri wa umma, benki, madukani na masokoni

Sehemu salama

Nyumbani kwako na ndani ya gari binafsi lakini kumbuka kuwa usalama huu hupungua unapoalika wageni au kuwapa watu lifti


Vitu vya kutumia kwa tahadhari

Sarafu na Noti, kuta na milango ya sehemu za umma, sehemu za pembeni ya ngazi, sehemu za kushikilia kwenye daladala, milango ya usafiri wa umma, vifaa tunavyotumia mara kwa mara kama simu, bakora au magongo ya watu wenye ulemavu

#COVID19 #JFCovid19_Updates #JamiiTalks
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…