#COVID19 Corona: Wahudumu wa maabara Kenya watishia kugoma

#COVID19 Corona: Wahudumu wa maabara Kenya watishia kugoma

chrome

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2011
Posts
401
Reaction score
426
Sekta ya afya nchini Kenya inakabiliwa na msukusuko kutokana na mfululizo wa migomo ya wahudumu wa afya katikati ya janga la virusi vya corona.

Muungano wa wahudumu wa maabara nchini Kenya umetoa muda wa hadi Januari 4 mwaka unaokuja kwa serikali kushughulikia madai yao au wajiunge na wauguzi na maafisa wa kliniki walio kwenye mgomo kwa muda wa siku 25 hivi sasa.

Kupitia muungano wao, KNUMLO, wahudumu hao wameisuta serikali wakisema imepuuza kitengo hicho muhimu huku juhudi zao, kushirikisha mazungumzo na asasi za serikali zikigonga mwamba kama anavyoelezea katibu mkuu Chrispine Momanyi.

"Endapo siku saba kuanzia sasa, taifa lote, iwe hata ni sekta ya binafsi, shirika la umma kama CDC, tunashirikiana kusitisha huduma zozote kwa hii serikali na wananchi kwa sababu hatuchukuliwi kuwa watu muhimu."

Kiasi wahudumu wa maabara 267 wameambukizwa virusi vya Corona
 
Hivi kwani mgomo uliisha. Si walikuwa kwenye mgomo siku chache zilizopita.
Maana majirani kwa kugoma ni NAMBARI WANI.
😂😆🤣
 
Back
Top Bottom