Corona: Ya Burundi ni somo tosha, hala hala majuto ni mjukuu

Corona: Ya Burundi ni somo tosha, hala hala majuto ni mjukuu

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Mabibi na mabwana moja kwa moja kwenye mada.

Ajabu na kweli pana watu wanakereka mno waonapo tunaandika kuasa na kukumbusha ili kwamba maisha ya watu yakiwamo na yao, yaweze kulindwa. Watu hawa waliobarikiwa mioyo ya ajabu na pia kuwa na midomo michafu iliyojaa matusi katu si wa kuwasabiria matakwa yao. Kwani kwa kufanya hivyo ni sawa na kuwafumbia macho mumiani ili wayafanye yao kwa nafasi.

Burundi ni nchi ambayo kuhusiana na Corona misimamo yake haijawa tofauti sana na yetu. Shughuli zao zote zimekuwa zikiendelea kana kwamba Corona ni ka upepo tu ambako katapita. Hawakuacha kunawa nawa mikono kwa maji tiririka na sabuni au kwa sanitizers, wala kuendekeza safari ambazo hazikuwa za lazima.

Burundi, uchaguzi wao mkuu uliendelea kana kwamba hakukuwa na janga la ugonjwa. Michezo iliendelea kama kawaida, Ibada, masoko, nk na bila shaka hata mashule hayakutatizika.

Wenzetu walipo tayari wameshaonja joto ya jiwe. Mengine tunayoambiana kuhusiana na strokes nk, hizo zinabakia kuwa ni mbwembwe tu, ambazo aghalabu hapa kwetu hizo tunajua kuzicheza zaidi.

Ndani ya siku tatu Rais wa Burundi ni marehemu (RIP), mama yake naye anasemekana kuwa tayari ni marehemu (RIP), mkewe anatibiwa Corona na pia dada yake anatibiwa Corona. Walinzi wote 3 waliompeleka bi Denise Nkurunziza hospitali nao wanatibiwa Corona.

Kwa ujumla serikali nzima ya Burundi itakuwa kwa sasa hivi iko njia panda. Kwani hata president elect General Evarisite Ndayishimiye na hata Spika ambaye angechukua hatamu kwa sasa wanasemekana kuugulia Covid.

IMG_20200611_231855_203.jpg


Chonde chonde ndugu zetu tusifikie huko. Wala tusijidanganye kuwa haya ni ya Burundi tu. Huu ugonjwa hauna mwenyewe.

Nafasi yetu ya kuishi kama mtu mmoja mmoja inasalia kuwa pale kila mmoja wetu atakapotambua umuhimu wa maisha ya mwenziwe.

Katika imani za TANU na CCM: "binadamu wote ni ndugu zangu." Mwisho wa kunukuu.

Haya yasibakie kwenye makaratasi peke yake.
 
Pia tusisahau kuwa Nkurunzinza aliwatimua maafisa wa WHO kwa sabababu ya kilimilimi pale wakopokosoa namna Burundi inayoshughulikia janga la Corona. Kuna uwezekano kuwa Rais ajaye ataiomba msamaha WHO.
 
Hapa kwetu ni kumuachia Mungu. Ukitegemea maneno ya wanasiasa utaula wa chuya. Take care.

Fuatilia sana ushauri wa kitaalamu . Achana na ngojera za wenye kusifu na kuabudu

Taarifa zingewekwa wazi watu wakajua shida iko wapi zaidi, mtu ungejipanga wapi pa kujitahidi ku avoid.
 
Pia tusisahau kuwa Nkurunzinza akawatimua maafisa wa WHO kwa sababubu ya kilimiilimi pale wakopokosoa namna Burundi inayoshughulikia janga la Coronakuna uwezekano kuwa rais ajaye ataiomba msamaha WHO.

Kazi kubwa. Tunakoelekea ajuaye mola.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Corona haipo Afrika Mashariki. Acheni kutisha watu

Mtu mzima anatishwa je mkuu?

Hata Burundi walikuwa wanasema hawakuwa na Corona. Angalia rekodi zao leo zinasema je.

Waliendelea hivyo hivyo pia hata walipokuwa wakiwatimua wale jamaa wa WHO.

Sasa hivi ni government in disarray!

Tungali na nafasi ya kutofika huko.
 
Mtu mzima anatishwa je mkuu?

Hata Burundi walikuwa wanasema hawakuwa na Corona. Angalia rekodi zao leo zinasema je.

Waliendelea hivyo hivyo pia hata walipokuwa wakiwatimua jamaa wale jamaa wa WHO.

Sasa hivi ni government in disarray!

Tungali na nafasi ya kutofika huko.
Hizo rekodi za kupikwa na mabeberu
 
Pia tusisahau kuwa Nkurunzinza aliwatimua maafisa wa WHO kwa sabababu ya kilimilimi pale wakopokosoa namna Burundi inayoshughulikia janga la Corona. Kuna uwezekano kuwa rais ajaye ataiomba msamaha WHO.
Kuna picha zinamuonesha mkulu wetu akikohoa kila baada ya sekunde tano tuwe makini.
 
Ujumbe mzuri sana na kuna cha kujifunza kweli hapo.
 
naona uko bize na corona.
Ila ubaya ni kwamba Tanzania inakupiga za CHEMBE..
Wewe hangaika tu usisahau tupo mwezi wa 6 tunaelekea wa 7.[emoji124][emoji124][emoji124][emoji124]
 
Sasa majuto kwa nani? Kwa waliokufa au waliobakia?

Ikiwa unajua maana ya neno *majuto* huwezi kuuliza maswali hayo. Na hasa ukitambua kuwa kuna maneno mengine kama wapendwa na wategemezi.

Kama huwezi kupata kamusi tembelea au wasiliana na BAKITA kwa ufafanuzi kama ni nia yako kuwa sehemu ya wengi wenye kufahamu.
 
Ikiwa unajua maana ya neno *majuto* huwezi kuuliza maswali hayo. Na hasa ukitambua kuwa kuna maneno mengine kama wapendwa na wategemezi.

Kama huwezi kupata kamusi tembelea au wasiliana na BAKITA kwa ufafanuzi kama ni nia yako kuwa sehemu ya wengi wenye kufahamu.


Swali liko wazi halina mafumbo wewe badala ya kujibu unaleta ngonjera, umesema majuto ni mjukuu, sasa majuto kwa nani kwa waliokufa au waliobakia huko Burundi?
 
naona uko bize na corona.
Ila ubaya ni kwamba Tanzania inakupiga za CHEMBE..
Wewe hangaika tu usisahau tupo mwezi wa 6 tunaelekea wa 7.[emoji124][emoji124][emoji124][emoji124]

Usikonde mkuu ninaandika kitabu kuhusiana na Corona labzima niwe bize nayo.

Kuandika kitabu yataka ufuatiliaji, uainishaji na kukomaa pia. 'Genge kwa wateja' havilamishi kuwa bize sana na Corona bali njegere na mbaazi. Au siyo mkuu.
 
Tatizo unayoyatabiri hayatokei unakuwa nabii wa UONGO.labda uwatabirie kenya.
Usikonde mkuu ninaandika kitabu kuhusiana na Corona labzima niwe bize nayo.

Kuandika kitabu yataka ufuatiliaji, uainishaji na kukomaa pia. 'Genge kwa wateja' havilamishi kuwa bize sana na Corona bali njegere na mbaazi. Au siyo mkuu.
 
Kuna picha zinamuonesha mkulu wetu akikohoa kila baada ya sekunde tano tuwe makini.

Ameendelea kuomba tumwombee. Hakika tunamwombea sana. Kwa hakika tusingependa asilani si yeye tu, bali mtu yeyote apotee kwa ugonjwa huu katika hali ambayo ingeweza kuepukika.

Eeh mola wetu utusikie sisi na kuwawezesha viongozi wetu waepuke kibri na kuwa ujasiri wa kutambua kwa vitendo kuwa kwa hakika msema kweli ni mpendwa wako.

Pokea sala zetu eeh mola wetu.
 
Vifo vilikuwepo hata kabla ya Corona.

Tuache kutiana hofu. Wewe kama hofu imekujaa sana moyoni mwako jilockdown nyumbani kwako. Sisi tunaendelea na safari.All to all utakufa tu hata kama si kwa Corona. Tunaishi kwa Neema tu Wala si kwa sababu tunajilinda sana. Daima Mungu mbele.
 
Back
Top Bottom