MakinikiA
JF-Expert Member
- Jun 7, 2017
- 5,104
- 6,827
Wafanyakazi wa Ikulu ya White House wameagizwa kuvaa barakoa wakati wanapoingia jengo la ofisi zake zinazofahamika kama -West Wing, baada ya wasaidizi wawili kupatwa na virusi vya corona.
Wafanyakazi wa White House wamesema kuwa wahudumu wote lazima wavae barakoa wakati wote isipokua wanapokua wameketi kwenye madawati yao ya kazi wakijitenga na wenzao.
Maagizo hayo yanakuja baada ya msaidizi wa Makamu wa rais Mike Pence na msaidisi wa Bwana Trump kuugua.
Bwana Trump anasema anahitaji sera.
Alionekana bila kuvaa barakoa katika bustani ya White House maarufu kama Rose Garden kwa ajili ya mkutano na waandishi kuhusu virusi vya corona , hata hivyo, rais alidai kuwa hahitaji kufuata maagizo hayo kwasababu hukaa "mbali sana na kila mtu", na akapuuza suala la maambukizi ya corona katika White House.
"Tuna mamia ya watu kila siku wanafika White House" kila siku, alisema. "Ninafikiri tunafanya kazi nzuri kuvidhibiti virusi."
Wajumbe watatu watatu wa White House wa kikosi kazi cha kupambana na virusi vya corona walikwenda kujitenga binafsi kwa wiki mbili baada ya kuwepo kwa uwezekano kupata maambukizi ya virusi vya corona.
Ni pamoja na Dkt Anthony Fauci, ambaye amekua maarufu katika vita dhidi ya virusi nchini Marekani.
Afisa habari wa Pence Katie Miller, mke wa mshirika wa Trump Stephen Miller, alipatwa na virusi Ijumaa.
Hii inafuatia kupatikana na ugonjwa kwa mtu anayemvalisha Trump ambaye pia alipatwa na ugonjwa.
Bwana Trump alionyesha kutojali huku akiinua mabega kuhusu kusambaa kwa virusi vya corona katika White House, akisema alikua "kimsingi mtu mmoja " ambaye alipata virusi na mtu huyo amepatikana hana virusi baada ya kupimwa.
Trump alisema nini tena ?
Bwana Trump alisema kuwa pesa zaidi zitatolewa kwa ajili ya kufanikisha ongezeko la upatikanaji wa vipimo katika majimbo
Serikali itatoa $11bn (£8.9bn) kwa majimbo ili kufikia malengo yao ya kupima mwezi huu. Majimbo yalikua yanauliza ni vipimo vingapi wanavyotumai kuvifanya mwezi Mei.
Maafisa wa ngazi ya juu wa White House ambao walikutyana mara kwa mara na Bwana Trump kwa sasa wanapimwa virusi vya corona kila siku.
Akishinikizwa na waandishi wa habari kuhusu ni lini Wamarekani wote watarajie kuweza kufanyiwa vipimo, Bwana Trump alisema: "Kama mtu anataka kupimwa sasa hivi ataweza kupimwa". Dai ambalo linapingwa
UCHAMBUZI
Donald Trump alifanya mkutano wake na waandishi wa habari kuzungumzia kuhusu kuongezeka kwa idadi ya vipimo vya virusi vya corona vilivyopo kwa ajili ya Wamarekani, lakini ni athari za janga kwa White House ambalo liliangaziwa.
Katika tukio lililofanyika katika Rose Garden wiki iliyopita, hakuna hata mmoja kati ya waliohudhuria , mkiwemo makamu wa rais Mike Pence ,aliyevaa barakoa.
Siku nne baadae, Pence ambaye mara kwa mara huwa kando ya rais -hakuonekana, afisa wake wa habari alipatikana na virusi vya corona siku chache zilizopita.
Kila aliyeshiriki ikiwa ni pamoja na mkwe wa Trump Jared Kushner, walikua na barakoa, baada ya agizo linalowataka wafanyakazi wote wa White kuvaa barakoa.
Ilikua ni amri ambayo ilimuhusu kila mmoja, isipokua rais, ambaye aliendelea kukataa kujilinda.
Hii ilikwenda kinyume kabisa na anachokizungumza , wakati akizungumzia "shauku " katika kufungua tena shughuli za kibiashara na kulegeza amri ya serikali ya kutosogeleana miongoni mwa wanajamii, masharti, ndivyo anavyokana kwamba mfumo ambao unawalinda wafanyakazi wa White House dhidi ya maambukizi umevunjika.
"Tuna watu wengi wanaoingia na kutoka'', alismema. "Tunaendesha nchi ."
Inaonyesha changamoto ya kimsingi inayoikabili Marekani katika siku zijazo. Je Marekani inaweza kupona wakati White House sio salama?
Nini kinachoendelea kuhusu kupima?
Kwa wiki kadhaa , Bwana Trump ametaka kushawishi kulegezwa kwa hatua za kukaa nyumbani kote nchini Marekani, akidai kuwa muda umefika wa kurejea kazini huku kukiwa na taarifa za kushuka kwa uchumi.
Hatahivyo, wataalamu wa afya wameonya kwamba kulegezwa kwa masharti mapema sana kunaweza kusababisha kusambaa kwa kasi kwa maambukizi na kuwepo kwa wimbi la pili la virusi vya corona.
Vituo vya Marekani vya Udhibiti wa ugonjwa vimetoa miongozo inayosema amri za kukaa nyumbani hazipaswi kulegezwa hadi pale eneo litakaposhuhudia kushuka kwa viwango vya maambukizi kwa siku 14 na kuweza kupima virusi watu 30 kati ya wakazi 1000.
Kwa mujibu wa mradi unaofuatilia maambukizi ya corona CovidTracking Project, limewafanyia vipimo kwa wastani watu 248,000 nchini Marekani siku katika wiki ya kwanza ya mwezi Mei.
Kwa mujibu wa White House, idadi imeongezeka hadi watu 300,000 kwa siku, lakini watafiti maarufu wanasema vinahitajika kufanyika vipimo walau 900,000 kila siku nchini Marekani kabla ya Marekani kufungua shughuli zake.
Hadi wiki hii, Marekani imepima asilimia 2.75% tu ya watu milioni 330 wa Marekani, na hakuna jimbo ambalo limepima 10% ya wakazi wake. Katika zaidi ya majimbo 12 ambako hatua za kukaa nyumbani ziliwekwa hatua hizo zimelegezwa mkiwemo Texas, South Carolina na Arizona, chini ya 2% ya wakazi wamepimwa virusi vya corona.
Wiki iliyopita, ikulu ya White House ilipinga muongozo wa kituo cha uchibiti wa magonjwa CDC kuhusu kufunguliwa kwa shughuli za kila siku, lakini baadhi ya majimbo yanafuata viwango vilivyotolewa.