Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,509
- 3,756
Ushauri wa Wataalamu wa Afya unaeleza kuwa sio kila aina ya Barakoa (Mask) inaweza kukulinda ili usipate maambukizi ya virusi vya Corona ila Barakoa pekee inayoweza kukulinda ni ya aina ya N95.
Wanasema virusi hivyo vinaingia mwilini kupitia macho, mdomo na pua hivyo njia pekee ya kukinga na maambukizi ni kusafisha mikono mara kwa mara kwa maji tiririka na sabuni au 'sanitizer'
Unapata maambukizi endapo muathirika wa virusi hivi atakukoholea au kukupigia chafya usoni. Kumbuka virusi hivi havisambazwi kwa njia ya hewa.
Kinachotokea ni endapo muathirika atakohoa au kupiga chafya virusi hutapakaa kwenye vitu na ukija kushika na kisha kujishika unapata virusi hivyo, ndio maana unatakiwa kusafisha mikoni.
Aidha, ukiivua barakoa hutakiwi kuivaa tena na ukiwa umeivaa unatakiwa kuwa muangalifu kutoishika hata wakati wa kuivua, vua ukiwa umeshika kamba sio sehemu ya mbele.
Kumbuka, unashauriwa kutumia 'sanitizer' iwapo hauna maji tiririka na sabuni.