JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Marekani kimeeleza kuwa #CoronaVirus ni ugonjwa mpya na bado Waatalamu wanajifunza namna unavyoenea, unaweza kuenea kwa kiwango gani na makali yake kwa binadamu.
Wataalamu katika Kituo hicho wamesema kwa sasa hawajui ikiwa Wanawake wajawazito wana nafasi kubwa ya kupata maambukizi ya COVID-19 au kuugua zaidi kuliko Watu wa kawaida wakipata maambukizi.
Ila wamebainisha kuwa Wanawake wajawazito hupata mabadiliko katika miili yao na mabadiliko hayo yanaweza kuongeza hatari yao ya kuambukizwa.
Aidha kuhusu matatizo kwenye mimba au kwa mtoto wamesema "Hatujui kwa wakati huu ikiwa #COVID19 inaweza kusababisha shida wakati wa ujauzito au kuathiri afya ya mtoto baada ya kuzaliwa".
Lapini pia wamesema hawajui kama mama naweza kumpa mtoto virusi akiwa tumboni au wakati wa kujifungua ila utafiti uliofanywa kwa Wanawake 9 wajawazito wenye maambukizi ya #covid19, unaonesha hakuna mtoto aliyepata maambukizi.
Katika utafiti huo, hakukuwa na #CoronaVirus kwenye majimaji ya amniotic (amniotic fluid) wala kwenye koo la mtoto au maziwa ya mama na hivyo kuonesha kuwa uwezo wa mtoto kupata virusi ni mdogo mno.
Amniotic fluid ni majimaji yanayomlinda mtoto tumboni yakifanya kazi kama mto wa kulalia/kalia lakini pia hutumika kuwezesha ubadilishanaji wa virutubisho na maji kati ya mama na mtoto.
Kuhusu kunyonyesha wamesema virusi huenea kupitia matone kwenye mfumo wa upumuaji hakuna ushahidi wa maziwa kuwa na virusi. Mama anashauriwa kuosha mikono na kuvaa barakoa ili kupunguza kumuweka mtoto kwenye hatari.