#COVID19 CoronaVirus: Madereva wa Malori wanaopita Uganda hawatakiwi kulala hotelini wala kwa Watu

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametangaza hatua mpya za kudhibiti mienendo ya madereva wa malori yanayoingia nchini humo kutoka mataifa jirani baada ya zaidi ya madereva 20 kupatikana na ugonjwa wa Covid-19.

Mataifa ya Uganda na Kenya yamekuwa yakiwafanyia vipimo wa virusi vya corona madereva wa malori katika mipaka yao hali ambayo imesababisha foleni ndefu ya magari hayo yaliopiga foleni ndefu

Madereva na wasaidizi wao upande wa Kenya wamelalamikia jinsi walivyosubiri kwa siku kadhaa kufanyiwa vipimo vya Covid-19 kabla ya kuruhusiwa kuvuka mpaka wa kuingia Uganda.

Njia ya usafirishaji mizigo kutoka bandari ya Mombasa nchini Kenya ni muhimu sana katika usafirishaji wa bidhaa muhimu kama vile chakula na dawa hadi Uganda, Rwanda, Sudan Kusini na Jamhuri ya Kidemocrasia ya Congo.

Lakini wasafirishaji wa mizigo hiyo sasa wanahofiwa huenda wakaeneza virusi vya corona katika kanda ya Afrika Mashariki.

Sasa Rais Museveni anasema hatua zaidi zitachukuliwa kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona.

Hatua hizo ni pamoja na kila lori kuwa na mtu mmoja - dereva pekee yake ambaye hataruhusiwa kulala hotelini wala nyumbani kwa watu.

Bw. Museveni pia amesema mienendo ya madereva hao itachunguzwa

rais Yoweri Museveni wa Uganda

Katika hotuba yake kwa taifa usiku wa Jumanne Rais Museveni pia aliangazia kuongezeka kwa chuki dhidi ya madereva hao kutoka kwa baadhi Waganda ambao wanahofia wataleta maambukizi ya corona niching humo.

Museveni aliongeza kwamba kusitisha usafirishaji wa bidhaa itakuwa na athari kubwa lakini alikubali kuwa madereva hao ni tishio katika mapambano ya nchi hiyo dhidi ya corona ikitoa mfano wa janga la Ukimwi la miaka ya 1980 na miaka ya tisini wakati ambapo madereva wa malori katika kanda hiyo waliaambukiza watu virus vya HIV katika kila miji waliyopitia wakiwa safarini.
 
Museveni anatesa Raia wake tu

Ufaransa wameiondosha lockdown Baada ya hali kuwa mbaya kiuchumi
 
Kafanya poa ila sasa watakula wapi, kulala wanaweza kulala kwenye magari yao, pia wanawezaje kumfuatilia mtu hadi atakapotoka nje ya mipaka yao?
 
Hayo makampuni ya maroli wangeajiri madereva pande zote mbili ..ikifika boarder wanabadilishana cha msingi kuhakikisha Kuna Usalama wa Kiafya Kwenye chumba cha Dereva... Mbona mabasi kabla ya corona wanafanya Sana...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndicho Uganda na Zambia wanakitaka wanataka kutumia fursa ya corona kutengeneza ajira kwa watu wao.

Madreva Wa Tanzania walishasema hili.mbona kuwa wazambia wanataka magari yote ya kutoka Tanzania Yale ya IT wao ndio wayapokee mpakani kupeleka Kongo

Tajiri gani atakubali kuajiri madreva wawili kwa gari Moja halafu mwingine amlipe kwa pesa za kigeni wakati akiwa na mmoja anamlipa pesa tu za Tanzania kamaliza
 
Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametangaza hatua mpya za kudhibiti mienendo ya madereva wa malori yanayoingia nchini humo kutoka mataifa jirani baada ya zaidi ya madereva 20 kupatikana na ugonjwa wa Covid-19.

Mataifa ya Uganda na Kenya yamekuwa yakiwafanyia vipimo wa virusi vya corona madereva wa malori katika mipaka yao hali ambayo imesababisha foleni ndefu ya magari hayo yaliopiga foleni ndefu

Madereva na wasaidizi wao upande wa Kenya wamelalamikia jinsi walivyosubiri kwa siku kadhaa kufanyiwa vipimo vya Covid-19 kabla ya kuruhusiwa kuvuka mpaka wa kuingia Uganda.

Njia ya usafirishaji mizigo kutoka bandari ya Mombasa nchini Kenya ni muhimu sana katika usafirishaji wa bidhaa muhimu kama vile chakula na dawa hadi Uganda, Rwanda, Sudan Kusini na Jamhuri ya Kidemocrasia ya Congo.

Lakini wasafirishaji wa mizigo hiyo sasa wanahofiwa huenda wakaeneza virusi vya corona katika kanda ya Afrika Mashariki.

Sasa Rais Museveni anasema hatua zaidi zitachukuliwa kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona.

Hatua hizo ni pamoja na kila lori kuwa na mtu mmoja - dereva pekee yake ambaye hataruhusiwa kulala hotelini wala nyumbani kwa watu.

Bw. Museveni pia amesema mienendo ya madereva hao itachunguzwa

rais Yoweri Museveni wa Uganda

Katika hotuba yake kwa taifa usiku wa Jumanne Rais Museveni pia aliangazia kuongezeka kwa chuki dhidi ya madereva hao kutoka kwa baadhi Waganda ambao wanahofia wataleta maambukizi ya corona niching humo.

Museveni aliongeza kwamba kusitisha usafirishaji wa bidhaa itakuwa na athari kubwa lakini alikubali kuwa madereva hao ni tishio katika mapambano ya nchi hiyo dhidi ya corona ikitoa mfano wa janga la Ukimwi la miaka ya 1980 na miaka ya tisini wakati ambapo madereva wa malori katika kanda hiyo waliaambukiza watu virus vya HIV katika kila miji waliyopitia wakiwa safarini.
Malori yakiacha kuingia Uganda si watakufa na njaa! Au siyo kweli mnamsingizia Museveni
 
Hawa madereva wa malori bwana sijui wao waliumbwaje ndio maana wakipata uongozi wanakuwa na maamuzi ya kishangaza kabisa katika hii dunia ya kujivukiza
 
M7 kachelewa kutangaza ..Ruanda walishatangaza mapema dereva ukiingia nchini kwao unalala kwenye kibbin mpaka urudi kwenu

Hakuna kuzunguka popote zaidi ya sehemu uliyopaki gari tena Ukiwa unataka huduma muhimu..

Ruanda walifanya kutokana na mazingira ya karantini hamna pa kuwaweka watu..kuanzia mashuleni, mahotelini na mahospitali watu wamejaa..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom