JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Kutokana na Ugonjwa wa #COVID19 familia nyingi zimejikuta katika wakati mgumu ambapo zinatakiwa kukaa ndani ili kuzuia kuenea kwa maambukizi. Hii ni baadhi ya namna ya kukufanya ule chakula chenye virutubisho vya kutosha
1. TUNZA MATUNDA NA MBOGAMBOGA
Kununua, kutunza na kupika mbogamboga zilizokatika hali nzuri (fresh) inaweza kuwa ngumu katika kipindi cha kutotoka nje. Lakini itakavyowezekana ni muhimu kuhakikisha Watoto wanapata matunda na mbogamboga katika chakula chao. Vyakula hivyo vinaweza kugandishwa na vitatunza virutubisho vyake vingi
2. TUMIA VYAKULA VYA KUKAUSHWA AU KWENYE MAKOPO
Chakula ‘fresh’ ndio chaguo sahihi, lakini vinapokuwa havipo kuna machaguo mengine ambayo ni rahisi kuhifadhi na yenye virutubisho vya kutosha. Mfano, maharage ya kwenye kopo yenye virutubisho vingi yanaweza kukaa kwa miezi hata mwaka na yanaweza kupikwa kwa namna tofauti
Mbogamboga kama nyanya za kwenye makopo huwa zina virutubisho vichache kuliko ‘nyanya fresh’ ila ni mbadala mzuri sana kama hakuna nyanya zilizogandishwa au zile zilizo ‘fresh’
Nafaka zilizokausha kama maharage, mchele vinaweza kukaa kwa muda mrefu na vikawa chakula kizuri sana. Vyakula kama ‘Cerelac’ vikichanganywa na maziwa au Yoghurt huweza kutumika kama chakula kizuri asubuhi
3. KUWA NA AINA TOFAUTI ZA VITAFUNWA
Watoto uhitaji kula kbla ya muda wa mlo kwa watu wote. Kuliko kuwapa watoto vitu vyenye sukari unaweza kuchagua vitu vyenye virutubisho kama matunda, mayai ya kukaanga au kuchemsha au chochote kinachoweza kupikika kwa haraka na chenye virutubisho
MADOKEZO KUHUSU USAFI WA CHAKULA
Huku kukiwa hakuna uthibitisho kuwa chakula au chakula kilicho kwenye vifungashio binahusika katika kusambaza #CoronaVirus inawezekana watu wakapata virusi hivyo kwa kushika sehemu zenye virudi na kisha kushika nyuso zao
Hatari kubwa zaidi ipo wakati mtu akipokea chakula cha kuagiza au akiwa anakatakata chakula. Kila mara usafi wa chakula ni muhimu wakati kwa kushughulikia chakula kuzuia magonjwa yoyote yanayoweza kusambazwa na chakula
Ondoa vifungashio vyovyote vya chakula ambavyo si muhimu na tupa kwenye chombo cha taka chenye mfuniko. Vifungashio kama makopo yanaeeza kusafishwa na ‘disinfectant’ kabla ya kufungua. Safisha mikono yako mara moja baada ya hapo
Osha vizuri vyakula ambavyo havipo kwenye vifungashio kama matunda na mbogamboga kwa kutumia maji tiririka
Ukiwa unaandaa Chakula safisha mikono yako vizuri kwa maji tiririka na sabuni kwa zaidi ya sekunde 20. Tumia kibao tofauti kwa kukatakata nyama na samaki na picha chakula katika jotoridi linalotakiwa
Ikiwezekana weka vyakula vinavyoharibika kwenye jokofu au vigandishe na chunguza muda wake wa kuharibika (Expiry Dates). Zingatia katika kutupa uchafu vizuri ili kuepuka kuchaza uchafu na kuvutia vijidudu.
Nawa mikono yako kwa maji safi tiririka na sabuni na hakikisha kila mmoja amefanya hivyo kabla ya kula. Pia, hakikisha mnatua vyombo visafi wakati wa kula

Upvote
0