Coronavirus: Namna ya kusafisha vitu na kuvipulizia dawa ya kuua vijidudu

Coronavirus: Namna ya kusafisha vitu na kuvipulizia dawa ya kuua vijidudu

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Joined
Aug 7, 2018
Posts
685
Reaction score
1,124
Vaa glovu wakati wa kusafisha na kuua vijidudu kwenye vitu. Glovu zinatakiwa kutupwa baada ya kutumika katika kila awamu ya usafi. Kama glovu zinaweza kuvaliwa tena basi ziwe ni kwa ajili ya kusafisha vitu kwa ajili ya #COVID19 tu

Kama sehemu ni chafu isafishwe kwa sabuni na maji kabla ya kuweka dawa ya kuua vijidudu. Safisha mikono yako mara tu baada ya kuvua glovu ulizotumia kufanya usafi

Kwa vifaa vya Kieletroniki kama simu, kitanza mbali (remote control), runinga na Kompyuta, ondoa kwanza uchafu unaoonekana, fuata masharti ya watengenezaji kila kifaa katika kuvisafisha

Tumia dawa ya kuua vijidudu yenye zaidi ya asilimia 70 ya kilevi ili kuvifuta au kuvinyinyizia (spray) kisha vikaushe kuzuia majimaji kuingia ndani ya vifaa hivyo
 
Upvote 0
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom